Wednesday, 23 August 2017

[wanabidii] PROF. BRIAN VAN ARKADIE ATOA SOMO MAPINDUZI YA KILIMO MHADHARA WA ESRF

Habari za asubuhi,

Tafadhali pokea CODES hapa chini

TAASISI ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imefanya mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara.

Katika mhadhara huo msemaji Mkuu alikuwa Prof. Brian Van Arkadie, majadiliano yalitanguliwa Prof Samuel Wangwe na Aloyce Hepelwa

Akiwasilisha mada yake aliwataka wataalamu kubadilika katika namna ya kusaidia kuongeza tija katika kilimo na kuachana na dhana za zamani kwamba wakulima wameshindwa kubadilika na kukwamisha maendeleo.

Amesema katika mjadala huo wa hadhara kuhusu maendeleo ya kilimo kutoka wakati wa uhuru hadi sasa katika jengo la mikutano la ESRF mjini hapa alisema kwamba tafiti nyingi zimekuwa zikishutumu wakulima kwa kuwa na muono mdogo na kubisha mabadiliko yanayohitaji kuongeza uzalishaji.

[caption id="attachment_2742" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.[/caption]

Aidha alisema kwamba kumekuwepo na tafiti zinazoonesha kwamba kilimo kimekwama katika uasili wake na kuhitajika tafiti za kuona namna bora ya kukikwamua.  Hata hivyo alisema profesa huyo, kumekuwepo na mabadiliko ya maana katika uchumi wa vijijini, hasa kwa kuangalia uhalisia wa uchumi kwa kuzingatia fursa za kiuchumi na masoko katika maisha ya wanakijiji.

Alisema kutokana na mabadiliko hayo ni dhahiri kusema kwamba wakulima hawabadiliki ni kushindwa kwa wataalamu ambao ndio walibuni na kupanga mipango ambayo haikuweza kuwanufaisha wakulima.

Profesa Brian Van Arkadie ambaye pia alishawahi kuwa Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es salaam na miongoni mwa watafiti ESRF anasema kuna hatua mbalimbali zilizofikiwa na wakulima wa Tanzania tangu uhuru na kwamba kuna uhusiano kati ya kilimo na maendeleo yaliyopo sasa.

Alisema katika mkutano huo wa hadhara ulilenga kuchambua masuala muhimu yanayojitokeza katika kilimo cha Tanzania na kuona namna bora ya kukabiliana na changamoto hizo kwa maendeleo ya taifa, kuwa kuanzia miaka ya 1970 mazao kwa ajili ya masoko ya nje yaliporomoka sana na kusababisha taifa kutafuta njia nyingine ya kurekebisha hali hiyo ikiwamo kuanzishwa kwa mradi wa kubadili kilimo wa SAGCOT.

[caption id="attachment_2743" align="aligncenter" width="1404"] Prof. Brain Van Arkadie ambaye ni msemaji mkuu wa mhadhara mkubwa ulishirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara akiwasilisha utafiti wake katika mkutano huo ulioandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.[/caption]

Ingawa mazao hayo ya kilimo yameonakana kuporomoka kutoka miaka hiyo, kumekuwepo na ongezeko kubwa la pengo la kipato kati ya watu wa mijini na vijijini huku ukuaji wa vijijini ukikumbwa na  udumavu. Pamoja na ukweli huo amesema profesa huyo, kuna mabadiliko ya kutosha katika maeneo ya vijijini na katika kilimo kwamba kusema hakuna maendeleo si kitu sahihi.

Alisema zipo sababu za kupungua kwa uzalishaji wa mazao makuu kama kahawa, tumbaku, mkonge na  hilo linatokana na serikali kuingilia kati mfumo wa masoko ambao haukuwa unaswihi. Profesa huyo alisema hata hivyo, kwa miaka 50 kilimo cha Tanzania kimefanikiwa kulisha taifa kwa kuwezesha watu wa mijini na vijijini kupata vyakula hasa vile vya msingi ingawa wakati mwingine ukame ulileta usumbufu.

Huku Tanzania ikiwa na ongezeko la watu kutoka milioni 12.3 kwa mwaka 1967 hadi milioni 44.9 kwa mwaka 2012 ni dhahiri ukuaji wa kilimo umesaidia kuiweka nchi katika hali bora zaidi ya upatikanaji wa chakula ingawa ifikapo mwaka 2030 watu wa mijini watakuwa wameongezeka kwa asilimia 37 na kuweka shinikizo ambalo kwa namna nyingine linaweza kuwa na maana kwa kuwa mazao ya chakula yatakuwa ndiyo ya biashara na hivyo kuacha kutegemea yale ya asili kama kahawa na tumbaku.

[caption id="attachment_2745" align="aligncenter" width="1404"] Mtafiti mshiriki mwandamizi wa ESRF Prof Samuel Wangwe akijadili mada iliyowasilishwa na Prof Brian Van wakati wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.[/caption]

Katika utafiti mwaka 2007, imeonekana kwamba  nusu ya mapato ya watu wa Dar es salaam yamekuwa yakitumika kwa ajili ya kununua chakula na kufanya kiasi kikubwa cha kazi za kilimo katika mazao ya chakula kuwa biashara nzuri kwa wakulima.Katika mada yake profesa huyo alisititiza kwamba hakuna shaka  maendeleo nchini katika kilimo yapo lakini tafiti nyingi zimeshindwa kuelekeza kisahihi maendeleo hayo na ukweli wa kutoneemeka kwa wakulima.

Akijadili mada hiyo ya Prof. Brian Van Arkadie, Mtafiti mshiriki mwandamizi wa ESRF Prof Samuel Wangwe ameshauri serikali kutonakili mikakati na sera za nchi zilizoendelea wakati wa utekelezaji wa mikakati ya kugeuza nchi kuwa taifa la uchumi wa kati linalotegemea viwanda.

Alisema hayo katika mhadhara kuhusu kilimo nchini kwamba si sawa kunakili sera na mikakati ya nchi zilizoendelea kama Uingereza, Asia ama Marekani katika kutekeleza sera ya viwanda bali ibuni yenyewe kwa kuzingatia hali iliyopo.

[caption id="attachment_2746" align="aligncenter" width="1404"] Mhadhiri mwandamizi kitengo cha kilimo uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof Aloyce Hepelwa akijadili mada iliyowasilishwa na Prof Brian Van wakati wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.[/caption]

Akizungumza  wakati akijadili mada iliyowasilishwa na Prof Brian Van Arkadie kutoka Uingereza kuhusu mazao ya chakula kama ndio mazao ya biashara katika mikakati ya muda mrefu ya kubadili kilimo cha Tanzania na athari za kisera, Prof Samuel Wangwe alisema kila nchi ina njia yake ya kufikia ustawi na neema ya viwanda na hivyo Tanzania lazima ifuate njia yake na sio kunakili.

"Hatuwezi kupita njia ambayo nchi kama Uingereza, Japan, au nchi za Ulaya zimepita wakati wakikua kiviwanda, lakini tuwe na njia yetu katika kuelekea uchumi wa viwanda . Kama hatutakuwa makini hatutafanikiwa," alisema.

Prof Wangwe pia alisema kwamba mapinduzi ya Kilimo lazima yapewe kipaumbele kama taifa linataka kuwa na uchumi wa viwanda. Akikaribisha  wadau kushiriki katika mhadhara huo Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema kwamba  mhadhara huo ulikuwa ni njia muafaka ya kubadilisha maarifa ili kuboresha kilimo cha Tanzania kwa kukipatia kilimo hicho mkakati wa muda mrefu wa kubadilika.

[caption id="attachment_2747" align="aligncenter" width="1404"] Picha juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa wanazuoni mbalimbali wakiwasilisha maoni yao wakati wa mhadhara wa kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliondaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.[/caption]

Alisema katika kuimarisha kilimo hicho ni vyema masuala yanayogusa mazao ya chakula na yale ya kupeleka nje na sera  kuangaliwa kwani masuala hayo yana athari za muda mrefu katika ukuaji wa kilimo.

Katika hadhira hiyo aliwataka washiriki kuangalia kwa makini historia ya kilimo nchini, sera na kuona athari za muda mrefu na fupi za sera zilizopo na kama kweli wataalamu wametekeleza wajibu wao katika kutafuta suluhu ya wakulima au kuendelea kudai kwamba wakulima hawako tayari kubadilika.

Dk. Kida alisema kwa kuangalia historia ya kilimo Tanzania wataalamu hao watakuwa na nafasi kubwa ya kuchangia katika kuendeleza kilimo ambacho ni msingi mkubwa wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, kwani wapo asilimia 80 wakitegemea kilimo na taifa ambalo linataka kwenda katika uchumi wa viwanda ambavyo mali ghafi zinategemewa kutoka katika sekta ya kilimo.

Aidha alimshukuru Prof. Brain Van Arkadie ambaye ndiye alikuwa msemaji mkuu kwa utafiti alioufanya ambao aliuwasilisha mbele ya mkutano wa wasomi mbalimbali.

Prof. Van Arkadie ambaye ni veteran ambaye alishawahi kushiriki katika mpango wa miaka mitano wa kwanza wa maendeleo mwaka 1963. Na kufanyakazi katika maeneo mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki na Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

[caption id="attachment_2749" align="aligncenter" width="1404"] Mwenyekiti wa mhadhara huo Profesa wa Kilimo Uchumi kitengo cha Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Lucian Msambichaka akiendesha mhadhara huo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida na kushoto ni Prof. Brain Van Arkadie ambaye ni msemaji mkuu wa mhadhara huo.[/caption]

[caption id="attachment_2750" align="aligncenter" width="1404"] Prof. Brain Van Arkadie ambaye ni msemaji mkuu wa mhadhara huo akifafanua jambo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.[/caption]

[caption id="attachment_2751" align="aligncenter" width="1404"] Pichani juu na chini ni sehemu ya wanazuoni na wadau kutoka taasisi mbalimbali walioshiriki kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara katika mhadhara huo ulioandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.[/caption]

[caption id="attachment_2756" align="aligncenter" width="1404"] Picha ya pamoja ya washiriki wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara ambao uliandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.[/caption]

[caption id="attachment_2757" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akibadilishana mawazo na wageni waalikwa baada ya kumalizika kwa mhadhara huo ulioandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.[/caption]

KAWAIDA

TAASISI ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imefanya mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara.

Katika mhadhara huo msemaji Mkuu alikuwa Prof. Brian Van Arkadie, majadiliano yalitanguliwa Prof Samuel Wangwe na Aloyce Hepelwa

Akiwasilisha mada yake aliwataka wataalamu kubadilika katika namna ya kusaidia kuongeza tija katika kilimo na kuachana na dhana za zamani kwamba wakulima wameshindwa kubadilika na kukwamisha maendeleo.

Amesema katika mjadala huo wa hadhara kuhusu maendeleo ya kilimo kutoka wakati wa uhuru hadi sasa katika jengo la mikutano la ESRF mjini hapa alisema kwamba tafiti nyingi zimekuwa zikishutumu wakulima kwa kuwa na muono mdogo na kubisha mabadiliko yanayohitaji kuongeza uzalishaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Aidha alisema kwamba kumekuwepo na tafiti zinazoonesha kwamba kilimo kimekwama katika uasili wake na kuhitajika tafiti za kuona namna bora ya kukikwamua.  Hata hivyo alisema profesa huyo, kumekuwepo na mabadiliko ya maana katika uchumi wa vijijini, hasa kwa kuangalia uhalisia wa uchumi kwa kuzingatia fursa za kiuchumi na masoko katika maisha ya wanakijiji.

Alisema kutokana na mabadiliko hayo ni dhahiri kusema kwamba wakulima hawabadiliki ni kushindwa kwa wataalamu ambao ndio walibuni na kupanga mipango ambayo haikuweza kuwanufaisha wakulima.

Profesa Brian Van Arkadie ambaye pia alishawahi kuwa Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es salaam na miongoni mwa watafiti ESRF anasema kuna hatua mbalimbali zilizofikiwa na wakulima wa Tanzania tangu uhuru na kwamba kuna uhusiano kati ya kilimo na maendeleo yaliyopo sasa.

Alisema katika mkutano huo wa hadhara ulilenga kuchambua masuala muhimu yanayojitokeza katika kilimo cha Tanzania na kuona namna bora ya kukabiliana na changamoto hizo kwa maendeleo ya taifa, kuwa kuanzia miaka ya 1970 mazao kwa ajili ya masoko ya nje yaliporomoka sana na kusababisha taifa kutafuta njia nyingine ya kurekebisha hali hiyo ikiwamo kuanzishwa kwa mradi wa kubadili kilimo wa SAGCOT.

Prof. Brain Van Arkadie ambaye ni msemaji mkuu wa mhadhara mkubwa ulishirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara akiwasilisha utafiti wake katika mkutano huo ulioandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Ingawa mazao hayo ya kilimo yameonakana kuporomoka kutoka miaka hiyo, kumekuwepo na ongezeko kubwa la pengo la kipato kati ya watu wa mijini na vijijini huku ukuaji wa vijijini ukikumbwa na  udumavu. Pamoja na ukweli huo amesema profesa huyo, kuna mabadiliko ya kutosha katika maeneo ya vijijini na katika kilimo kwamba kusema hakuna maendeleo si kitu sahihi.

Alisema zipo sababu za kupungua kwa uzalishaji wa mazao makuu kama kahawa, tumbaku, mkonge na  hilo linatokana na serikali kuingilia kati mfumo wa masoko ambao haukuwa unaswihi. Profesa huyo alisema hata hivyo, kwa miaka 50 kilimo cha Tanzania kimefanikiwa kulisha taifa kwa kuwezesha watu wa mijini na vijijini kupata vyakula hasa vile vya msingi ingawa wakati mwingine ukame ulileta usumbufu.

Huku Tanzania ikiwa na ongezeko la watu kutoka milioni 12.3 kwa mwaka 1967 hadi milioni 44.9 kwa mwaka 2012 ni dhahiri ukuaji wa kilimo umesaidia kuiweka nchi katika hali bora zaidi ya upatikanaji wa chakula ingawa ifikapo mwaka 2030 watu wa mijini watakuwa wameongezeka kwa asilimia 37 na kuweka shinikizo ambalo kwa namna nyingine linaweza kuwa na maana kwa kuwa mazao ya chakula yatakuwa ndiyo ya biashara na hivyo kuacha kutegemea yale ya asili kama kahawa na tumbaku.

Mtafiti mshiriki mwandamizi wa ESRF Prof Samuel Wangwe akijadili mada iliyowasilishwa na Prof Brian Van wakati wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Katika utafiti mwaka 2007, imeonekana kwamba  nusu ya mapato ya watu wa Dar es salaam yamekuwa yakitumika kwa ajili ya kununua chakula na kufanya kiasi kikubwa cha kazi za kilimo katika mazao ya chakula kuwa biashara nzuri kwa wakulima.Katika mada yake profesa huyo alisititiza kwamba hakuna shaka  maendeleo nchini katika kilimo yapo lakini tafiti nyingi zimeshindwa kuelekeza kisahihi maendeleo hayo na ukweli wa kutoneemeka kwa wakulima.

Akijadili mada hiyo ya Prof. Brian Van Arkadie, Mtafiti mshiriki mwandamizi wa ESRF Prof Samuel Wangwe ameshauri serikali kutonakili mikakati na sera za nchi zilizoendelea wakati wa utekelezaji wa mikakati ya kugeuza nchi kuwa taifa la uchumi wa kati linalotegemea viwanda.

Alisema hayo katika mhadhara kuhusu kilimo nchini kwamba si sawa kunakili sera na mikakati ya nchi zilizoendelea kama Uingereza, Asia ama Marekani katika kutekeleza sera ya viwanda bali ibuni yenyewe kwa kuzingatia hali iliyopo.

Mhadhiri mwandamizi kitengo cha kilimo uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof Aloyce Hepelwa akijadili mada iliyowasilishwa na Prof Brian Van wakati wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Akizungumza  wakati akijadili mada iliyowasilishwa na Prof Brian Van Arkadie kutoka Uingereza kuhusu mazao ya chakula kama ndio mazao ya biashara katika mikakati ya muda mrefu ya kubadili kilimo cha Tanzania na athari za kisera, Prof Samuel Wangwe alisema kila nchi ina njia yake ya kufikia ustawi na neema ya viwanda na hivyo Tanzania lazima ifuate njia yake na sio kunakili.

"Hatuwezi kupita njia ambayo nchi kama Uingereza, Japan, au nchi za Ulaya zimepita wakati wakikua kiviwanda, lakini tuwe na njia yetu katika kuelekea uchumi wa viwanda . Kama hatutakuwa makini hatutafanikiwa," alisema.

Prof Wangwe pia alisema kwamba mapinduzi ya Kilimo lazima yapewe kipaumbele kama taifa linataka kuwa na uchumi wa viwanda. Akikaribisha  wadau kushiriki katika mhadhara huo Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema kwamba  mhadhara huo ulikuwa ni njia muafaka ya kubadilisha maarifa ili kuboresha kilimo cha Tanzania kwa kukipatia kilimo hicho mkakati wa muda mrefu wa kubadilika.

Picha juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa wanazuoni mbalimbali wakiwasilisha maoni yao wakati wa mhadhara wa kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliondaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema katika kuimarisha kilimo hicho ni vyema masuala yanayogusa mazao ya chakula na yale ya kupeleka nje na sera  kuangaliwa kwani masuala hayo yana athari za muda mrefu katika ukuaji wa kilimo.

Katika hadhira hiyo aliwataka washiriki kuangalia kwa makini historia ya kilimo nchini, sera na kuona athari za muda mrefu na fupi za sera zilizopo na kama kweli wataalamu wametekeleza wajibu wao katika kutafuta suluhu ya wakulima au kuendelea kudai kwamba wakulima hawako tayari kubadilika.

Dk. Kida alisema kwa kuangalia historia ya kilimo Tanzania wataalamu hao watakuwa na nafasi kubwa ya kuchangia katika kuendeleza kilimo ambacho ni msingi mkubwa wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, kwani wapo asilimia 80 wakitegemea kilimo na taifa ambalo linataka kwenda katika uchumi wa viwanda ambavyo mali ghafi zinategemewa kutoka katika sekta ya kilimo.

Aidha alimshukuru Prof. Brain Van Arkadie ambaye ndiye alikuwa msemaji mkuu kwa utafiti alioufanya ambao aliuwasilisha mbele ya mkutano wa wasomi mbalimbali.

Prof. Van Arkadie ambaye ni veteran ambaye alishawahi kushiriki katika mpango wa miaka mitano wa kwanza wa maendeleo mwaka 1963. Na kufanyakazi katika maeneo mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki na Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Mwenyekiti wa mhadhara huo Profesa wa Kilimo Uchumi kitengo cha Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Lucian Msambichaka akiendesha mhadhara huo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida na kushoto ni Prof. Brain Van Arkadie ambaye ni msemaji mkuu wa mhadhara huo.
Prof. Brain Van Arkadie ambaye ni msemaji mkuu wa mhadhara huo akifafanua jambo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Pichani juu na chini ni sehemu ya wanazuoni na wadau kutoka taasisi mbalimbali walioshiriki kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara katika mhadhara huo ulioandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Picha ya pamoja ya washiriki wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara ambao uliandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akibadilishana mawazo na wageni waalikwa baada ya kumalizika kwa mhadhara huo ulioandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment