Tuesday, 22 August 2017

Re: [wanabidii] Re: TABIA HII YA LISU: SIKU MOJA ITALIAIBISHA TAIFA

Kwamba ameiIbika AU LA NI JUU YA KILA MTU KUAMUA.
Cha msingi ni kuwa serikali inadaiwa kwa sababu waziri mhusika (ambaye si magufuli kama Lisu anavyosema) alivunja mkataba. Kama waziri alishauriana au hakushauriana na mwanasheria mkuu ni swala la kuhoji. lakini ukimsikiliza sana Lisu anapotoa maelezo unaona hatetei ndege kukamatwa au taifa. Bali anakusanya madongo ya kumtupia magufuli. sasa hata kama anayomgonga nayo si yake ni aibu basi tutafakali



From: Henry Oppi <henryoppi@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, August 21, 2017 6:12 AM
Subject: Re: [wanabidii] Re: TABIA HII YA LISU: SIKU MOJA ITALIAIBISHA TAIFA

Wapendwa,
Kwa hili sakata la ndege kushikiriwa ameaibika Lissu au taifa?. Lissu amekuwa akisisitiza kuhusu utawala wa sheria lakini wenzetu wanatumia nguvu za mamlaka matokeo yake ndo haya.

On 16 Aug 2017 1:10 pm, "'hussein siyovelwa' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Hongera, MR. MUHINGO  kwa makala yako nzuri kuhusu Tundu Lissu. Kwa bahati mbaya nilichelewa kuisoma. Tatizo la Lissu ni ujinga uliofunikwa blanketi la weledi. anapinga kuliko aliowakuta katika upinzani. Shida ni kwamba anapinga ili kuthibitisha uaminifu wake kwa wakuu wake na si kwa ajili ya maslahi ya nchi. MI NADHANI HATALIABISHA TAIFA ISIPOKUWA ATAJIABISHA MWENYEWE NA WANAOMSHABIKIA. mfano katika suala la makinikia alijidhihirisha mwenyewe kwamba uzalendo wake ni wa kutiliwa mashaka. NI JUKUMU LETU WAZALENDO KUMZOMEA KWA HOJA KILA ANAPOTOA UONGO WAKE ILI AJUE KWAMBA ANAJIDHARAULISHA.


On Monday, 24 July 2017, 23:14, ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com> wrote:


Toka rais Magufuli alipoingia madarakani kumekuwa na sura mbili duniani.
Nje mataifa mengi yanamuunga mkono. Baadhi ya wananchi wanatamani angekuwa rais wa nchi zao.
Ndani ya nchi wananchi walio wengi wanamuunga mkono. Wanaanza kuona adha walizolalamikia zimepungua, au kuna matumaini kuwa mbele kuna matumaini.
Makundi haya mawili ni sehemu ya sura moja. Yote yana sababu zinazofanana.
Mataifa mengi hasa ya uchumi mdogo, yaani mataifa maskini wamechoshwa na Rushwa, ufisadi, wizi, ukosefu wa uwajibikaji nakadhalika. Viongozi walio wengi wamekuwa wakijilimbikiza mali na kwa kweli wakishaingia madarakani wanaanza kuishi kama wale walio katika mataifa tajiri huku wananchi wao wakiumia. Wanaumia kwa kubeba serikali kubwa na zenye marupurupu yasiyoneneka huku huduma za kijamii zikibaki chini na watawala wakisingizia hali mbaya ya umaskini.
 
Tanzania hatukupona hilo. Nisamehewe kwa kutaja mifano ya karibu. Serikali ya awamu ya nne ilipoingia madarakani ilionekana kugawa vyeo si kwa manufaa ya wananchi bali waliopata vyeo. Tukumbushane mgawanyo wa Wizara ya mambo ya ndani kwa kuanzisha wizara ya usalama wa raia. Mpaka tulipopiga kelele kwa usikivu wa rais akazirudisha zikawa moja. Lakini tumeshuhudia mgawanyo wa wilaya na mikoa huku hayo hayaleti tija bali mzigo kwa walipa kodi. Tumeshuhudia utumbuaji wa mali ya umma kupitia misafara mirefu na safari za mara kwa mara za viongozi. Tumeshuhudia watu Fulani wakiwa na uhakika kwamba hawawezi kuguswa na vyombo vya dola. Tumeshuhudia kashfa zinatokea, uchunguzi unafanyika, inaonekana wazi kuwa Fulani na Fulani wana kesi ya kujibu lakini hawashtakiwi. Ikafika mahala wengine wakataka kugombea na kutaka kulitawala taifa. Ukweli tulifika mahala maneno ya kuchochea maasi yakaanza kutoka. Nakumbuka kusoma mahala mtu akitania (au akimaanisha) kuwa kama Mwamnyange akiingia ikulu atashangilia. Tulifika mahala pabaya. Ukweli tulifika mahala watu wakadhani uchaguzi hauwezi kutusaidia kutoka kwenye shida hizi. Hayo yakiwa hapa nchini ndivyo ilivyo kwenye mataifa yote yanayomshangilia na kumpongeza magufuli.
 
Mataifa na mashirika yanayotufadhili katika miradi mbalimbali walifika mahala wakaamua kuacha kutusaidia. Ikawa viongozi watoke nje kubembeleza misaada. Wakawa wanakwenda nchi kumi wanaahidiwa sehemu mbili tu.
 
Baada ya uchaguzi, 2015 na Dr. John Magufuli kushinda Tanzania na ulimwengu tulishuhudia mabadiliko. Mtu aweza kuandika mengi; lakini napenda kuyaandika kwa muhtasari:
=             Tumeshuhudia Serikali ikipunguza kwa kiasi kikubwa matumizi yasiyo ya lazima. Safari ziliachwa na sasa zinadhibitiwa. Vikao visivyo vya lazima havifanyiki na vinavyofanyika havitumii posho za ajabu au kutumia matumizi ya anasa huku tukiwa maskini.
=             Wizi wa ajabu umedhibitiwa. Wafanyakazi hewa wameondolewa na kama wamebaki basi ni kwa kiwango kidogo sana. Mikataba iliyokuwa inatuibia imerekebishwa na kwa kweli rais amethubutu kuifumua mikataba.
=             Mafisadi, wala rushwa, na waharibifu wa mali za umma vimedhibitiwa kwa kiwango kikubwa.
=             Biashara na matumizi ya madawa ya kulevya vimeshughulikiwa kwa kiwango cha hali ya juu na si muda mrefu kuna watu watakuja kujifunza Tanzania ilifanyaje katika vita hii.
=             Nidhamu imerejea. Nani angetegemea watu kama Singasinga wa IPTL angelala rupango? Nani angefikiri Manji angelala lockup? Wafanyakazi serikalini na ofisi za umma kwa ujumla sasa ukifika unahudumiwa kwa nidhamu sana. Kuna wanaosema watu hawako huru. Nani alitarajia watu waliokuwa wanaingia ofisini na kutoka, waache tabia hiyo kwa uhuru? Ni halali walazimishwe kufika kazini na kuifanya kwa ufanisi. Kama wanalazimika sawa. Si wanalazimika kwa mujibu wa mikataba tu? Lakini nidhamu imerudi.
 
Kazi hii kubwa iliyofanywa na rais Magufuli imefanikiwa na kuonwa ndani na nje. Viongozi badala ya kusubiri rais aende kwao kuomba sasa wanakuja wenyewe na kuahidi misaada. Tumeshuhudia majuzi waziri mkuu wa India anaamua kujiunga na rais magufuli alipotembelea kibaha huku akiwa kwao. Akakatisha shughuli zake na kuhutubia mkutano wa magufuli kwa njia ya mtandao. Lini uliisikia hiyo. Tena anafanya hivyo kueleza shkrani zake na kuahidi kuisaidia Tanzania kuondokana na tatizo la maji..
Kwa wale waliokuwa wanafaidika wanaona hakuna mtu mbaya kama Magufuli. Wako tayari kufanya lolote na hii ilitarajiwa. Wako tayari kutumia mbinu yoyote ili kumyumbisha au kuyumbisha umma wa Tanzania. Wako tayari kugharimia kwa namna yoyote ile ikiwa ni pamoja na kuangalia kati yetu kuna nani wanaoweza kulipwa wakafanya wanaloweza kufanya. Nitaeleza huko mbele lakini siamini kama Tundu Lisu, kwa mfano; hayuko kwenye Pay roll ya mtu
 
Wakati hilo kundi hilo likiyaona anayoyafanya Magufuli kuna kundi la pili lililokataa si kuona tu anayofanya Magufuli bali haliko tayari kusikia ulimwengu unamsemaje. Kama watu wasio na akili wakati wengine wanamsifu wao wanakazana kuwaelimisha wengine kuwa Magufuli hafanyi chochote. Kuna mambo mengine kama unaona kitu Fulani na walio wengi wanaona kingine lazima utafute mkakati wa kuwaelimisha unachoona na namna bora ni kunyamaza kwanza. Hivi watu waliokandamizwa na hayo yote niliyoyataja wawezaje kusimama mbele za watu ukasema tunateseka kwa kukosa kibali cha kuandamana? Una akili kweli? Watu walikandamiza na rushwa na ufisadi, mzigo wa serikali kubwa, makusanyo makubwa ya kodi isiyoonekana inafanya nini. Sasa hayo yameondoka. Unasema hatuna kibali cha kuandamana. Kuandamana kudai nini? Mambo ya kufanya watu waandamane yameondolewa. Kwanza hata bila kupiga marufuku kuandamana utaandamana kupinga nini? Badala ya kwenda shambani kulima ili upitishe mazao kwenye barabara nzuri unataka utumie barabara nzuri kuandamana tena bila kudai chochote? Hii nayo inakutwa Tanzania tu.
 
Angalau wengine wamejirudi. Wanasema Magufuli anafanya vizuri lakini ======. Angalau hao unaweza kupata cha kujadiliana nao
 
Lakini tunaye mwenzetu Tundu Lisu. Sehemu ninayomfahamu ni mwanaharakati. Kwa kidogo nikijuacho anapenda kutetea haki. Hana historia ya kuhusika na Rushwa. Niliwahi kuambiwa kuwa kama angekuwa mtoa rushwa angeishakuwa mbunge zamani. Kwa sababu hiyo nilitokea kumpenda. Wakati CHADEMA Ikiwa na kiongozi (Dr. Slaa) kulikuwa na udhibiti. Mambo ya kipuuzi tunayoyaona sasa angekuwepo tusingeyaona. Wabunge wake walitamka mambo yaliyohaririwa kwa mantiki. Sasa hayupo ndipo tunashuhudia madhara yake.
Tundu lisu, mbunge wa Singida anatamka mambo mpaka UNAULIZA kama huyu alilelewa na bibi yake au alilelewa msituni tu na nyani kwa hiyo utamaduni wa binadamu anajifunza kadri anavyowazoea binadamu. Ni kweli anamchukia Dr Magufuli. Huenda ana sababu. Huwezi kujua aliahidiwa nini kama chama chake kingeshinda. Anaweza kuumia kuliko wengine. Kuna matamshi anayatamka juu ya Magufuli ukiyapima unaona yako nje ya mlolongo wa siasa. Sipendi kutamka maneno yoyote anayoyasema ili kila anayetaka atafute. Lakini matamshi yake unaweza kujiuliza taaluma yake ina maadili ya kazi? Yeye ni Rais wa TLS. Hivi humo TLS ndivyo wanavyojibizana wakitofautiana? Au hawatofautiani? Watu wengi waliitahadhalisha TLS kuhusu Lisu kuchaguliwa kuwa rais wa taasisi hiyo. Kwa ushabiki sijui niuiteje wakamchagua. Bila shaka walidhani wanamkomesha aliyewatahadhalisha. Sasa tunajiuliza TLS ina Codes of Conduct? Zinaruhusu hayo tunayoyaona Lisu akifanya? Sasa nina uhakika kuwa TLS iko njia panda: Kuendelea kukubaliana na Lisu, heshima yake ikashuka machoni pa jamii au kuamua kujitenga na Lisu. Kama Codes of Conduct zinaruhusu hayo basi ndiyo hivyo. TLS inafutika. Inajifuta.
Mwenendo huu wa Lisu usipodhibitiwa basi taifa litaingia pabaya. Mimi ninadhani hatutafika huko. Kama Serikali itashindwa, wapo wazalendo wa nchi hii watamdhibiti Tundu.
Subiri kidogo.
 
Elisa Muhingo
0767 187 507
 
--




Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@ googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@ googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/ optout.








--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@ googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@ googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/ optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment