Friday, 10 October 2014

[wanabidii] Re: 50 - 50 inayoshabikiwa na kina Mama Wanaharakati inatekelezeka?

Kina Mama wanaharakati wamesikika wakisema kuwa wao wanaunga mkono katiba pendekezwa kwa sababu mambo yao yote yameingizwa! Je ndugu zangu hivi hii ni sababu ya msingi ya kuunga mkono katiba? eti unaunga mkono katiba eti kwa sababu tu mambo yako yote yameingizwa!! hivi kweli ni busara hii? Kwani ni kundi lenu tu ndio linaishi hapa Tanzania?
 
Pili, wanashabikia sana kitu kinachoitwa 50 - 50, naomba ndugu zangu tujadili kwa wale mliosoma katiba, je suala hili litawezekana? tutaweza ku-operationalized? Nionavyo, hiki ni kiini macho ili kupata support ya wanawake. Naona 50 - 50 haitawezekana kwa sababu moja: Ni kweli Mgombea binafsi ameruhusiwa lakini kuna sharti ambalo kwa upande mwingine lina discourage kugombea kama mgombea binafsi.
 
Hivyo basi, kugombea kupitia katika vyama vya siasa ndio njia pekee kubwa itakayoendelea kubaki. Swali langu: Ni wanawake asilimia ngapi ambao ni wanachama wa vyama mbalimbali? My guess ni kuwa ni asilimia ndogo sana ya wanawake ambao ni wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa, hivyo, kwa kuwa wanawake wengi si wanachama basi  hawataweza kusimamishwa na vyama mbalimbali vya siasa na wao sidhani kama njia ya kugombea kama wagombea binafsi itakuwa ni option inayofaa kwao. Sasa hiyo 50 -50 ya madiwani, wabunge n.k itapatikana vipi?? jamani si kiini macho hiki?? naomba mnisaidie.

0 comments:

Post a Comment