Siku ukiona Huyo jamaa kauchukua urais ujue Mwamnyange anaingia magogoni kuokoa jahazi lisizame
--------------------------------------------
On Wed, 10/1/14, 'Ngupula GW' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Edward Ngoyai Lowassa: Mchapa kazi mwenye nakisi ya uadilifu na falsafa
To: "'ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, October 1, 2014, 6:39 PM
Ndugu Elisa,acha kumtumia Nyerere
kama hilizi....mwalimu alifanya mema mengi,lkn pia kuna
mengi alikosea....kama mwalim angelikuwepo
leo,angempendekeza Lowassa,kwan ana kila sifa. Kwa lowassa
ujinga mwingi mlioushuhudia usingefanyika ...huyo
Salim,hebu msahau kabisaaaa,na ukitaka Tz imeguke,ni hapo
mawazo yako yatapofanyiwa kazi....na kwa kukuambia tu,kama
ikibidi mzanzibar,bas sio Salim ni Shein...ngupula
'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
>Mambo mengine mawili yanayoweza kumsumbua au
kumkwamisha kabisa Lowasa ni 1) Kukataliwa na Baba wa Taifa
1995
>2) kuwa na wapange wengi jambo linalodhibitisha
uwezekano wa kuwa na mali nyingi na pia kuashilia uwezekano
wa kuwa na liserikali likubwa kupita kawaida maana wote hao
inabidi awashukuru 'kwa kazi kubwa' wanayofanya.
>Namsubiri salimu Ahmed salim maana naye anatajwa
>--------------------------------------------
>On Thu, 9/25/14, mngonge franco <mngonge@gmail.com>
wrote:
>
> Subject: Re: [wanabidii] Edward Ngoyai Lowassa: Mchapa
kazi mwenye nakisi ya uadilifu na falsafa
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Date: Thursday, September 25, 2014, 9:48 AM
>
> Kama CCM watampitisha
> basi kawa rais moja kwa moja na pengine hakuna sababu
ya
> kupiga kura tusipompigia jeshi litachukua nchi. Maana
> tumekwishatishwa na wakubwa
>
> 2014-09-25 9:28
> GMT+03:00 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>:
> KATIKA
> makala mbili nilizoandika na kuchapishwa katika gazeti
hili
> wiki mbili zilizopita, nilijaribu kuanisha sifa za
kihaiba
> na kikazi za mwananchi anayefaa kuwa Rais wetu wa
> tano.Nashukuru
> kwa mrejesho niliopokea kutoka kwa wasomaji wengi na
> walionitia shime niendelee na makala hizi. Nawashukuru
pia
> waandishi wenzangu wa makala, akiwemo mwandishi mahiri
na
> mkongwe, Johnson Mbwambo, kwa kurejea maudhui ya
makala
> yangu katika andiko lake lililochapishwa katika gazeti
hili
> toleo Na. 370 la Septemba 10-16, 2014.Nakubaliana
> kwa kiasi kikubwa na hofu aliyoonyesha juu ya uwezekano
wa
> wagombea kukidhi sifa nilizozianisha, pamoja na
hitimisho
> lake kwamba wagombea waliokwishajitokeza hadi sasa
wana
> ombwe kubwa la kifalsafa.Nilisitisha
> kwa muda makala hizi kutokana na uzito wa maoni
niliyopokea
> kutoka kwa watu mbalimbali, wakiwemo viongozi
waliojijengea
> heshima kubwa katika nchi yetu. Wengi wa waliotoa
maoni
> walienda mbali na kunishauri niandike kitabu kuhusu
wasifu
> wa wagombea.Wengine
> waligutuka nilipohitimisha makala yangu kwa ahadi ya
kuanza
> kuwajadili wagombea mmoja baada ya mwingine, wakidhani
> kwamba nitakuwa nakwenda mbali mno! Aidha, wapambe wa
> wagombea nao wamekuwa na wasiwasi kwamba nitawabeba
baadhi
> ya wagombea na kuwaharibia wagombea wao.Baadhi
> ya wasomaji na wapambe wa wagombea wamenishauri kwamba
> niache kuwajadili wagombea na niwaachie wananchi
waamue
> wenyewe. Nimekataa ushauri wao huu wa kuwachia
wananchi
> waamue wenyewe, na hivyo naendelea na uchambuzi wangu
wa
> wagombea wote waliojitokeza na
watakaojitokeza.Nimeamua
> kujitwika jukumu hili hatarishi kama sehemu ya wajibu
wangu
> wa kijamii katika kuchangia kuiepusha nchi kupata
kiongozi
> atakayetushtukiza bila kumjua sawasawa kabla hajaingia
> madarakani. Ukimwacha Mwalimu Nyerere, marais wetu
waliopita
> na aliyepo walitushtukiza.Hatukumjua
> vizuri Mzee Mwinyi kabla hajawa Rais, na vivyo hivyo
kwa
> Mzee Mkapa. Wote hawa walipatikana kwa mtindo
unaofanana:
> waliibuliwa bila kujitutumua wao wenyewe kuutaka urais
kwa
> udi na uvumba kama ilivyo kwa wagombea wa leo.Mzee
> Mwinyi aliibuliwa na Kamati Kuu ya CCM, wakati Mzee
Mkapa
> aliibuliwa na Mwalimu Nyerere pasipo kutarajiwa.
Bahati
> nzuri waliibuliwa katika mtindo usiotia shaka sana kwa
> sababu ni uzao wa taasisi za kueleweka kwa wakti ule,
ambazo
> ni Mwalimu mwenyewe na Kamati Kuu ya CCM ya wakati huo
> ambayo isingekuwa rahisi kuitilia shaka katika maamuzi
> yake.Pengine
> tulimjua kidogo Rais Kikwete kabla ya kuingia
madarakani kwa
> sababu alijinadi vya kutosha kabla hajaingia ikulu
mwaka
> 2005. Jina la Rais Kikwete lilianza kuwika kwa upana
wake
> kwa mara ya kwanza mwaka 1995 alipochukua na kurudisha
fomu
> ya kugombea urais kwa mbwembwe, sambamba na swahiba
wake
> mkuu wa wakati huo, Ndugu Edward Lowasa.Tangu
> wakati huo tuliendelea kumwagiwa sifa kemkem juu ya
Rais
> Kikwete hadi anaingia madarakani mwaka 2005. Kwa hiyo,
> hatukujua upande wa pili wa Rais Kikwete kwa maana ya
> udhaifu wake kihaiba na kiutendaji kabla hajaingia
> madarakani. Ndiyo kusema naye kwa kiasi fulani
> alitushtukiza.Yote
> hii ni kwa sababu tumekuwa hatuna utamaduni wa
kuwadodosa
> vya kutosha watu wanaotaka kuwa viongozi wetu.
Maandishi
> mengi kuwahusu wagombea huandikwa wakati wa kampeni
> yakilenga kuwasifu wagombea fulani na 'kuwakandia'
> wagombea wengine. Hatupati uchambuzi unaotuwezesha
kuwajua
> wagombea wote kwa ukamilifu wake katika kutusaidia
kufanya
> maamuzi ya maana. Hili ndilo ombwe la ufahamu ambalo
> najaribu kuliziba katika mfululizo wa makala
zangu.Katika
> uchambuzi wangu nitajitahidi kuwa mkweli na kuzingatia
> maadili na weledi wa kitaaluma ili kuepuka kupendelea
au
> kuonea. Hata hivyo, kama yalivyo maandishi yote katika
> sayansi ya jamii, sitarajii kwamba makala hizi
hazitaibua
> hisia kali, shutuma, lawama na hata vitisho kutoka kwa
> miongoni mwa wapambe wa wagombea ambao wamejiaminisha
kwamba
> wagombea wao ndio hasa wanaofaa kuongoza nchi hii na
hakuna
> mwingine.Niwatahadharishe
> wasomaji na hasa wapambe wa wagombea kwamba
ninachokiandika
> hapa ni wasifu wa wagombea, kwa maana ya
"biography" na
> sio w
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment