Hii staili ya uongozi inabidi kuichukulia PhD.
Viongozi wengi tuliowazoea wakiwa na matatizo ndani ya nchi zao hukatisha hata ziara. Sasa wa kwetu kwa staili hii lazima akimaliza uongozi aende chuoni kuifundisha ili apate wenzake wa kumuiga.
--------------------------------------------
On Sat, 9/27/14, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Baraza la Mawaziri kubadilishwa tena?
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, September 27, 2014, 1:52 PM
Yaani
huyu rais hawezi kufanya maamuzi akiwa nyumbani? Siagi za
ugenini zinamsaidia kuamua?em
Sent from my iPhone
On Sep 27,
2014, at 4:45 AM, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
wrote:
ZIARA ndefu ya
Rais Jakaya Kikwete nchini Marekani huenda ikaibuka na
mabadiliko katika Baraza la Mawaziri au Taasisi nyeti za
serikali, Raia Mwema limeelezwa.
Rais Kikwete
aliondoka wiki iliyopita kwa ziara ya wiki mbili Marekani,
katika wakati ambao serikali yake imegubikwa na masuala
mazito yanayohitaji maamuzi yake.
Masuala hayo ni
mchakato wa Katiba na uchunguzi uliofanywa na Ofisi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja
na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
kuhusu fedha zilizochotwa kutoka katika akaunti ya Tegeta
Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania (IPTL).
Taarifa ambazo
gazeti hili linazo zinaeleza kwamba baadhi ya vigogo wa
serikali wametajwa
kuhusika katika
suala hilo linalotajwa kuwa na harufu ya ufisadi na huenda
Kikwete anatatizwa kuhusu hatua za kuchukua.
Habari hizi
zinatiwa nguvu na kauli ya Spika wa Bunge, Anne Makinda,
wiki hii kwamba endapo kusingekuwa na Bunge Maalumu la
Katiba (BMK) na badala yake ripoti ya uchunguzi wa CAG
kuwasilishwa kwenye Bunge la kawaida, kuna mawaziri
wasingepona kwenye sakata hili.
Makinda alitoa
kauli hiyo wakati wa tukio la kumuaga CAG aliyestaafu,
Ludovick Utouh, ambaye ofisi yake ndiyo iliyochunguza suala
la akaunti hiyo iliyokuwa ikihifadhi fedha za Shirika la
Umeme Tanzania (Tanesco) na kampuni ya Independent Power
Tanzania (IPTL).
Kiasi cha
shilingi bilioni 200 zinadaiwa kuchotwa kutoka katika
akaunti hiyo na kulipwa kwa kampuni ya Pan African Power
(PAP) katika mazingira ambayo vyombo hivyo vya serikali
vilikuwa vinayachunguza.
"Makinda
alisema aliyoyasema kwa sababu ameiona hiyo ripoti na anajua
kilicho ndani. Makinda yuko bungeni tangu miaka ya 1970 na
anajua ni lipi la kusema na lipi si la kusema hadharani.
Kama amesema kuna mawaziri wasingepona, ujue maana yake kuna
mawaziri wasingepona," kilisema mojawapoi ya vyanzo vya
gazeti ambavyo kwa sababu za wazi hatutaweza kutaja majina
yake.
Vyanzo vya
gazeti hili serikalini vimeeleza kwamba umekuwa utaratibu wa
kawaida wa Kikwete kukaa nje ya nchi kwa kipindi kirefu
wakati anapokuwa na mambo yanayomsumbua kichwani na
anayotaka ufumbuzi wake.
Ziara ya kwanza
ndefu ya Kikwete ughaibuni ilikuwa Oktoba mwaka 2007, wiki
chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
kiliibua iliyoitwa Orodha ya Mafisadi katika tukio
lililofanyika Septemba 15 mwaka huo.
Watu wa karibu
na Kikwete wameliambia gazeti hili kuwa "Rais alitumia
ziara hiyo katika nchi za Ulaya na Marekani kubadili upepo
na kupunguza msongo wa mawazo kwa sababu suala hilo
lilichukuliwa kwa uzito mkubwa hata na Jumuiya ya
Kimataifa".
Kikwete pia
alikuwa nje ya nchi, safari hii Afrika Kusini, mwaka 2011,
wakati Bunge lilipoamua kuchukua hatua dhidi ya aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo,
ambaye alikuwa katika kashfa ya kudaiwa kutaka kuhonga
wabunge ili wapitishe bajeti ya wizara yake.
Ni katika wakati
huo ndipo alipofanya pia mabadiliko yaliyomwondoa Jairo
pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William
Ngeleja.
Desemba 18 mwaka
jana, Kikwete alianza ziara ndefu nchini Marekani na siku
mbili baadaye akakubali kujiuzulu kwa mawaziri wanne katika
Baraza lake la Mawaziri kutokana na Operesheni
Tokomeza.
Kikwete
aliondoka nchini kwa kile kilichoelezwa kwenda Marekani kwa
ajili ya kufanyiwa matibabu ya afya yake, lakini aliporejea;
mawaziri Khamis Kagasheki, Emmanuel Nchimbi, Shamsi Vuai
Nahodha na David Matayo, walikuwa tayari waeondolewa kutoka
serikalini.
Mara hii tena
Rais Kikwete ameenda Marekani kwa wiki mbili. Hii si ziara
ya kawaida. Na ameondoka baada ya kuona ripoti za CAG na
Takukuru ambazo Makinda amesema kuna mawaziri hawatapona.
Kikwete mwenyewe ndiye anayejua nini kinafuata, alisema
mmoja wa manaibu mawaziri wa serikali ya Kikwete.
Raia Mwema: Ziara ya Kikwete Marekani
yazua mambo
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment