Wednesday, 1 October 2014

Re: [Mabadiliko] RE: [wanabidii] Mtandao wa Wanawake na Katiba Kuelimisha Katiba Inayopendekezwa

Muhimu Sele

Sent from my iPad Leila Sheikh

On 1 Okt 2014, at 9:10, Selemani Rehani <srehani@hotmail.com> wrote:

Mimi si mtaalam wa mambo ya Katiba, lakini nilikuwa nabadilishana mawazo na mtaalaam akaniambia kuwa mengi yaliyoingizwa katika katiba hii ya Chenge na Sitta ni kiini macho. Nitaeleza kwa ufupi: Wanawahadaa Watanganyika kuwa eti haki za wanawake , za wakulima, wafugaji, wachimbaji madini, vijana, wasanii zimeingizwa wakati hazikuwemo katika rasimu ya Tume ya Warioba. Mtaalamu huyo ameniambia kuwa haki hizo zimewekwa katika section ambayo huwezi kuzidai iwepo haki hizo zitaminywa au kunyang'anywa. Ni kama ambavyo baadhi ya haki hizo zipo hata katika katiba yetu ya sasa ya mwaka 1977. Ila tu huwezi kwenda mahakamani kuzidai, kwa sababu zimewekwa katika section ambayo sina jina lake, hivyo huwezi kuzidai. Naomba wataalamu mnisaidia ni section gani hiyo? hivyo kuingizwa kwa haki hizo ni kiini macho. Ni vyema NGOS, ASASI MBALIMBALI NA VYAMA VYA SIASA VIKATOA ELIMU JUU YA HILO.
 
Kinachosikitisha ni kuwa baadhi ya asasi mbalimbali bila kwenda kwa undani na kujua na kubaini hila zilizopo nyuma ya pazia ktk katika katiba hii ya CMM na Chenge, wameanza eti kuunga mkono katiba hii ya Chenge na Sitta WAKISEMA ETI KUNA HAKI ZA WAKULIMA, WAFUGAJI N.K. Maskini ni wajinga, naomba elimu iwafikie.  Lakini ni muhimu kutambua kuwa wapo wale wajinga ambao wanaunga mkono kwa kutojua lakini wengi wao wanajua ila wanamtumikia bwana. Katika nchi hii kila mtu anaimba wimbo wa watawala, tunazo NGOs ambazo hazipo serious, tunao viongozi wa dini wanawatumikia watawala, wasomi, na vyama vya siasa kama UDP, TLP n.k. ambavyo navyo ni wale wale wachumia tumbo na wanaimba wimbo ule ule wa watawala. HIVYO KAZI NI NGUMU SANA. Taifa la wanafiki na wanaojipendekeza kwa watawala. Jamani! hata viongozi wa dini? hata wasomi?? NGOs? kweli umaskini ni balaa!
 

Date: Tue, 30 Sep 2014 21:04:58 +0300
Subject: [wanabidii] Mtandao wa Wanawake na Katiba Kuelimisha Katiba Inayopendekezwa
From: mushijoa@gmail.com
To: djlukejoe@gmail.com; info@dewjiblog.com; brotherdanny5@gmail.com; drweyunga@gmail.com; subi@wavuti.com; pbuyegu2@gmail.com; wanabidii@googlegroups.com; othmanmichuzi@gmail.com; amichuzi@gmail.com; mdimuz@gmail.com; zainul.mzige21@gmail.com; jestinageorge@googlemail.com; johnbukuku@gmail.com; albertgsengo@yahoo.com; francisgodwin2004@yahoo.com; josephat.lukaza@gmail.com; uwazi@hotmail.com

[caption id="attachment_51433" align="aligncenter" width="495"]<img class="size-full wp-image-51433" alt="Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Prof. Ruth Meena akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam." src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_0138.jpg" width="495" height="480" /> Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Prof. Ruth Meena akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption]
[caption id="attachment_51431" align="aligncenter" width="480"]<img class="size-full wp-image-51431" alt="Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Usu Mallya akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam." src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_0181.jpg" width="480" height="612" /> Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Usu Mallya akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption]
[caption id="attachment_51427" align="aligncenter" width="640"]<img class="size-full wp-image-51427" alt="Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam." src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_0236.jpg" width="640" height="329" /> Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption]
[caption id="attachment_51428" align="aligncenter" width="511"]<img class="size-full wp-image-51428" alt="Baadhi ya wakichangia mada katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam." src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_0223.jpg" width="511" height="480" /> Baadhi ya wakichangia mada katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption]
[caption id="attachment_51426" align="aligncenter" width="640"]<img class="size-full wp-image-51426" alt="Baadhi ya wanachama wa mtandao wa Wanawake na Katiba, TGNP pamoja na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu wakionesha mabango yenye jumbe mbalimbali juu ya mchakato wa Katiba inayopendekezwa." src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_0245.jpg" width="640" height="359" /> Baadhi ya wanachama wa mtandao wa Wanawake na Katiba, TGNP pamoja na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu wakionesha mabango yenye jumbe mbalimbali juu ya mchakato wa Katiba inayopendekezwa.[/caption]
[caption id="attachment_51429" align="aligncenter" width="480"]<img class="size-full wp-image-51429" alt="Baadhi ya wakichangia mada katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam." src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_02141.jpg" width="480" height="572" /> Baadhi ya wakichangia mada katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption]
[caption id="attachment_51430" align="aligncenter" width="640"]<img class="size-full wp-image-51430" alt="Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam wakiwa katika kongamano hilo." src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_0211.jpg" width="640" height="427" /> Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam wakiwa katika kongamano hilo.[/caption][caption id="attachment_51435" align="aligncenter" width="640"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_0205.jpg" alt="Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam wakiwa katika kongamano hilo." width="640" height="427" class="size-full wp-image-51435" /> Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam wakiwa katika kongamano hilo.[/caption][caption id="attachment_51434" align="aligncenter" width="640"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_0208.jpg" alt="Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam wakiwa katika kongamano hilo." width="640" height="427" class="size-full wp-image-51434" /> Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam wakiwa katika kongamano hilo.[/caption]

<strong>MTANDAO</strong> wa Wanawake na Katiba, TGNP pamoja na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu wameahidi kushirikiana kutoa elimu ya uraia na uhamasishaji juu ya Katiba inayopendekezwa baada ya kutangazwa kwa muda rasmi wa kuanza kwa zoezi hilo kwa jamii ili kuelimisha zaidi wananchi juu ya Katiba nayopendekezwa. Kauli hiyo imetolewa katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha wanaharakati mbalimbali.

Akifafanua zaidi katika mada yake aliyoiwasilisha kwenye Kongamano hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi alisema endapo Bunge Maalum la Katiba Litapitisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa kwa kura nyingi za ndiyo kwa Wajumbe wa Bunge hilo, Rais Jakaya Kikwete atakabidhiwa rasimu hiyo na Kuwa Katiba Inayopendekezwa.

Alisema baada ya hapo kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba utaratibu wa utoaji wa elimu na uhamasishaji kwa Umma juu ya maudhui yaliyomo kwenye Katiba inayopendekezwa na Kampeni ya Upigaji wa Kura ya maoni utafanyika zoezi litakalofanywa na Tume husika na vyama vya siasa, vyama vya kijamii vinaruhusiwa kushiriki kutoa elimu ya uraia na uhamasishaji juu ya elimu hiyo.

"...Ratiba kamili ya muda wa kutoa elimu kwa umma kuhusu maudhui yaliyomo katika Katiba inayopendekezwa itatolewa kupitia Tanagazo la Gazeti la Serikali (Government Notice). Kwa madhumuni ya kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuhusu kuipigia kura ya maoni Katiba inayopendekezwa, Tume italazimika, na vyama vya siasa na vyama vya kijamii vinaweza kutoa elimu ya uraia na uhamasishaji juu ya Katiba inayopendekezwa kwa muda usiozidi siku thelathini kuanzia siku ya kuchapishwa katika Gazeti la Serikali," alisema Bi. Liundi.

Alisisitiza kuwa kipindi hicho ni muhimu kuwafanya wananchi wote waelewe kilichomo katika Katiba inayopendekezwa ili waweze kuona kama masuala yao ya muhimu yameingizwa katika katiba hiyo kabla ya kuipigia kura.

Aidha Mkurugenzi huyo alitoa wito hasa kwa wanawake na makundi ya pembezoni kutumia kipindi hicho kuisoma na kuielewa Katiba inayopendekezwa kwani ndiyo sheria mama na itakuwepo kwa muda mrefu kwa ajili ya jamii yote na hata ya vizazi vijavyo, hivyo ni muhimu kutambua kuwa katiba hiyo ni ya wananchi wote kwa ujumla na si ya vyama vya siasa wala kundi fulani katika jamii.

"...TGNP Mtandao wa wanawake na katiba pamoja na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu tutaendelea kutumia fursa hiyo kuendelea kuelimisha na kuraghbisha wananchi kuhusu Katiba inayopendezwa. Hii itasaidia sana wakati wa kuipigia kura ya maoni juu ya Katiba inayopendekezwa wananchi wawe wana uelewa wa kutosha kuhusu yaliyomo katika katiba hiyo na hatimaye wapige kura wakiwa na maamuzi sahihi," alisema Bi. Liundi.

Akizungumzia zoezi la kufanya mabadiliko katika katiba ya 1977, kama walivyokubaliana wajumbe wa Taasisi ya Kidemokrasia Tanzania (TCD) katika mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni kwa mujibu wa vyombo vya habari, kwamba kwa kuwa Katiba Mpya haitakuwa tayari katika uchaguzi mkuu ujao yafanyike mabadiliko muhimu kwenye katiba ya mwaka 1977 ili iweze kutumika katika uchaguzi huo.

Aliishauri serikali kutoa taarifa rasmi kutoka katika mamlaka husika za serikali kuhusu suala hili zito na nyeti kuhusu mabadiliko ya katiba ya 1977 kama sehemu ya maandalizi ya uchaguzi ujao. Aliongeza kuwa pamoja na kwamba serikali haijatoa tamko rasmi au mwongozo wa jinsi ya kuendesha zoezi hilo, baadhi ya vyama vya siasa vimesha pendekeza mabadiliko wanayotaka yafanyiwe kazi.

"...Pamoja na mapungufu hayo ya taarifa rasmi, sisi Mtandao wa Wanawake na Katiba tunatoa mapendekezo yetu ya awali kuhusu mabadiliko katiba ya 1977 endapo yatalazimika kufanyika." Akitaja mapendekezo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TGNP, alisema Mtandao wa wanawake na katiba unapendekeza uwiano wa hamsini kwa hamsini katika nafasi zote za uongozi uingizwe katika mabadiliko pamoja na uwepo wa tume huru ya uchaguzi masuala ambayo ni kilio cha muda mrefu cha wananchi.

"Tunatarajia katika marekebisho ya Katiba ya 1977 suala hili la 50/50 katika ngazi za maamuzi litapewa kipau mbele. Tunadai pia katika mabadiliko ya Katiba ya 1977 sula la mgombea huru lipewe kipaumbele kwani ni wananchi wengi hususan wanawake wenye uwezo mkubwa lakini si wanachama wa chama chochote na hawana utashi wa kujiunga na chama chochote. Iwapo suala la mgombea huru litapitishwa wanawake na wanaume wengi watapata fursa ya kugombea nafasi mbalimbali bila kufungwa na chama cha siasa. Hii itapanua demokrasia na ushiriki katika masuala ya uongozi bila vikwazo na ubaguzi."
<strong>*Imeandaliwa na www.thehabari.com</strong>

_____________________________________________________
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/DUB118-W6C2FD91CAF0507E177F9FA5B80%40phx.gbl.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment