TAMKO LA VIJANA NCHINI KUMSIHI MWENYEKITI FREEMAN MBOWE AGOMBEE TENA NAFASI HII YA UENYEKITI WA CHAMA CHETU.
Tamko hili ni la vijana wote wa CHADEMA nchi nzima. Linasomwa hapa mbele ya hadhara hii kwa niaba ya vijana hao ambao wanayo hamu kubwa ya kumuona Mwenyekiti Freeman Mbowe akiwania tena nafasi hiyo ili akiongoze chama kwa miaka mingine mitano.
Vijana wa CHADEMA kwa moyo mmoja, kwa ari kubwa na dhamira njema kabisa ikichochewa na mapenzi makubwa kwa chama chetu kinachobeba matumaini ya Watanzania, tumeamua kuwaunga mkono Wazee wa Kigoma ambao walituwahi katika kumchukulia fomu Mwenyekiti Mbowe ili kumshawishi na kumuomba agombee tena.
Kama vijana bado tunaona haja ya kumtaka Mh Freemani Aikael Mbowe kuendelea kukilea chama na kukiongoza hadi tutakapo fikia malengo ya kushika dola kwani msukumo wetu ni uhalali wake kuongoza lakini pia mafanikio makubwa ambayo yameendelea kuonekana katika juhudi zake kama mwenyekiti wa CHADEMA hadi sasa.
Sisi vijana ndani ya Chama chetu tumekuwa tukitafakari sana kipindi hiki ambacho chama kinapitia katika wakati mgumu kutokana na juhudi kubwa za serikali kuhujumu demokrasia na kujenga hofu kwa wanachadema, pamoja na uwepo wa wengi wenye nia ya kukiongoza chama bado tunahitaji weledi na ujasiri wa Mheshimiwa Mbowe kuwa Mwenyekiti wetu hadi hapo tutakapofikia malengo yetu makubwa ya kushika dola na kuwakomboa watanzania kutoka katika serikali ya kidhalimu ya sasa.
Hadi tunafikia kutoa tamko hili tunatambua Uongozi ni utumwa lakini pia tunatambua sana Mheshimiwa Freeman Mbowe amekuwa akifanya kazi za chama kwa kujituma na hivyo ni haki yake kuhitaji msaada kwa sasa ili pia apate fursa ya kupumzika, lakini kama vijana bado tuna uhitaji mkubwa wa kuona chama kinazidi kung'ara hadi kufikia malengo ya kuwakomboa watanzania, hivyo tumefikiri kwa kina kama vijana na kuona kuna haja ya kutoa wito kwa Mwenyekiti wetu wa Chama Mheshimiwa Freeman Mbowe kuona umuhimu wake kwa sasa katika kipindi hiki ambacho chama kinapita katika misukosuko ya kushambuliwa na watawala kwa visa vya kutaka waendelee kubaki madarakani, pamoja na kutambua haki yake ya kutokugombea nafasi hiyo, lakini kama vijana ambao tumekuwa inspired na kuingia katika harakati hizi za siasa na tumejikuta tukishiriki katika kutetea maslahi ya umma, tunaona ni sahihi kabisa kwa mheshimiwa Mbowe kusikia kilio chetu na kuweza kukubali kuingia katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi hiyo ya uenyekiti wa chama ili aweze kuifikisha chadema tunaponuia ifike kwa maana ya kushika dola.
Sisi vijana tunarejea rekodi kubwa ambayo mwenyekiti wa chama chetu ameivunja katika utendaji wake uliotukuka ndani ya CHADEMA hususani mafanikio makubwa tuliyonayo sasa kwa chama kusambaa nchini kote, ongezeko la wabunge na madiwani, katika chaguzi za mwaka 2005 na 2010 lakini pia ustahimilivu wa chama kama taasisi ya kisiasa pamoja na mafanikio haya ndio msukumo wetu kuhitaji uwepo wake kama mwenyekiti wetu kwani pamoja na kelele za watawala kudai CHADEMA kitakufa ifikapo 2015 lakini aliendelea kuwa kiongozi imara huku chama kikizidi kuimarika kila kona ya nchi.
Tunatoa wito kwa vijana wote kote nchini wenye nia na mapenzi ya dhati watafakari yote yaliyofanywa kwenye uongozi wa mwenyekiti Mbowe na wapime kwa busara iliyojaa hekima kwa mustakabali wa chama chetu.
Vijana wa CHADEMA kwa sasa tunasema "kwa CHADEMA,Mbowe anatosha kwa sasa"
Emmanuel Masonga,
Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Njombe.
Kny; Vijana wa CHADEMA nchi nzima.
-- Tamko hili ni la vijana wote wa CHADEMA nchi nzima. Linasomwa hapa mbele ya hadhara hii kwa niaba ya vijana hao ambao wanayo hamu kubwa ya kumuona Mwenyekiti Freeman Mbowe akiwania tena nafasi hiyo ili akiongoze chama kwa miaka mingine mitano.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment