Saturday 30 August 2014

[wanabidii] URAIS 2015 : Edward Ngoyai Lowassa

Edward Ngoyayi Lowassa (amezaliwa 26 Agosti 1953) ni mwanasiasa nchini Tanzania. Alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kumi wa nchi hii tarehe 30 Desemba 2005 na akalazimishwa kujiuzulu tarehe 7 Februari 2008 kwa kutajwa katika kamati ya bunge ya uchunguzi wa ufisadi katika utoaji wa tenda kwa kampuni ya umeme ya Richmond kama mhusika mkuu.

Lowassa ni mwenyeji na mbunge wa Monduli katika Mkoa wa Arusha. Alisoma shahada ya kwanza katika mada ya tamthilia kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, halafu shahada ya pili katika sayansi kwenye Chuo Kikuu cha Bath (Uingereza).

Lowassa alishika vyeo mbalimbali katika serikali ya Tanzania kama vile:

  • Waziri Mkuu (2005 - 2008)
  • Waziri wa Maji na Mifugo (2000 - 2005)
  • Waziri wa ardhi na makazi (1993 - 1995)
  • Waziri mdogo wa haki na mambo ya bunge katika ofisi ya Makamu wa Rais (1990-1993)
  • Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (1989 - 1990)
  • Waziri mdogo wa mazingira na mapambano dhii ya umasini katika ofisi ya Makamu wa Rais (1988-2000)
  • Mbunge wa Monduli tangu 1990

http://sw.wikipedia.org/wiki/Edward_Ngoyai_Lowassa

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment