Sunday 31 August 2014

[wanabidii] MAKAO MAKUU CHADEMA WAFURAHIA MBOWE KUPINGWA. WAOMBA AANGUSHWE NA MBARUKU . WASEMA NI DIKTETA

VIONGOZI NA WATUMISHI  mashuhuri kadhaa ndani ya ofisi ya MAKAO MAKUU YA CHADEMA, wameonyesha kufurahishwa na kitendo cha Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Tabora kupambana na MBOWE kwenye kugombea uenykiti wa Taifa wa CHADEMA.

wakizungumza na mtandao huu huku  wakiomba kutokutajwa majina yao humu wamesema kwa sasa watapata pa kupumulia ikiwa MBARUKU ATASHINDA.

''unajua Mbowe anatufanya sisi kama watoto wake, amekigeuza hiki chama kama chumba chake cha kujisaidia haja kubwa na ndogo, anakifanya anavyotaka, ona alivyojifedhehesha, amemtuma BENSON KIGAILA, akampa Milioni 16 kwenda kigoma kushawishi wazee, badala yake KIGAILA amerudi na wacheza ngoma wa mapigo saba wale. nimefurahi sana MBARUKU KUTANGAZA NIA. tutamsaidia chini chini auangushe huu mbuyu uliooza''. alisema

naye Afisa mwandamizi MAKAO MAKUU ya CHADEMA kwa sharti lile lile la kutokutajwa jina kwa sasa amesema '' unajua mbowe alitamani kulia aliposikia MBARUKU amechukua fomu, alipiga simu kila sehemu kutukana matusi mazito mazito, eti tumemruhusu vipi kurudisha fomu?, huyu mwenyekiti sasa anaanza kuchuja vibaya.........nakwambia asipojiangalia sawasawa, lazima aangushwe. watu mikoani wanamchukia mno, kwa kweli amekuwa DIKTETA zaidi ya IDDI AMINI. chama hakiwezi kuendeshwa kwa anavyotaka yeye''.

mtandao huu ulipojaribu kumtafuta MBOWE kuthibitisha minong'ono hiyo simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment