Thursday, 28 August 2014

[wanabidii] Uchaguzi wa CHADEMA Mkoa wa Mara waibua mazito

Uchaguzi wa CHADEMA Mkoa wa Mara waibua mazito.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mara, jana Tarehe 27/08/2014 kilifanya uchaguzi wa ngazi ya Mkoa na kupata viongozi wapya watakaoongoza jahazi la kuing'oa CCM madarakani 2014/2015.

Uchaguzi huo ulifanyika katika ukumbi wa "Musoma Club" uliopo ndani ya mtaa wa Mkendo, manispaa ya mji wa Musoma, mkabala na Jengo la Ofisi za Uhamiaji Mkoa.

Uchaguzi ulikuwa wa Uhuru na Haki kwa nafasi zote zilizofanya uchaguzi, isipokuwa nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa iliyoahirishwa kutokana na badhi ya wagombea wa nafasi hizo kuwekewa pingamizi zilizotokana na tuhuma mbalimbali zilizopaswa kushughulikiwa na ngazi za juu za Chama.

Miongoni mwa wagombea waliowekewa pingamizi hizo ni Mwita Waitara ambaye ni Kiongozi mwandamizi wa Chama Makao Makuu.

Waitara anakabiriwa na tuhuma ya;
* Kuhusika na sakata la madiwani wa Shinyanga waliokisaliti Chama na baadae kuomba radhi.

* Kuwa anahusika na sakata la usaliti wa akina Zitto, Kitila Mkumbo na Mwigamba, maana kwenye shitaka hilo lililowasilishwa kwenye Kamati na kusomwa na Mwanasheria wa Kanda ya Ziwa Mashariki, mlalamikaji anadai kwamba anao ushahidi wa kudhibitisha pasi na shaka kwamba Mwita Waitara ndiye M2 aliyewahi kutajwa kwenye waraka wa akina Zitto Kabwe.

* Kuwa alikutwa akitoa rushwa ya fedha, vyakula na nauli za safari kwa wapiga kura.

* Kuwatukana na kuwakashifu wagombea wenzake bila sababu.

NB:Tuhuma hizi ni kwa mujibu wa ushahidi wa Sauti iliyorekodiwa na Picha zinazoonyesha na kuakisi matukio hayo.

Nafasi nyingine iliyoachwa wazi ni nafasi ya Katibu wa Vijana kutokana akidi ya kura kutotimia angalau nusu ya wapiga kura wa nafasi hiyo.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment