Tuesday, 29 July 2014

Re: [wanabidii] RATIBA YA UCHAGUZI WA NDANI YA CHADEMA

Kama kweli hizi sababu ni za kweli basi uchaguzi wa kanda na taifa uwekwe kiporo hadi hayo marekebisho ya katiba yafanyike, iwapo uchaguzi wa taifa utatangulia basi uwezekano wa ngazi ya taifa hasa mwenyekiti katibu na kamati kuu watakuwa na nguvu ya kushawishi matokeo.

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, July 29, 2014 2:45:18 AM GMT-0700
Subject: [wanabidii] RATIBA YA UCHAGUZI WA NDANI YA CHADEMA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RATIBA YA UCHAGUZI WA NDANI YA CHAMA

Ndugu wanahabari

Tunaomba kuanza press conference hii kwa kuendelea kuwashukuru kwa
ushirikiano wenu mnaotupatia kila mnapokuwa mkitimiza wajibu na majukumu
yenu kwa jamii.

Leo tunapenda kutoa kwa umma kupitia vyombo vya ratiba ya uchaguzi ya
uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea nchi nzima kwa sasa, kama
ilivyoazimiwa na Kamati Kuu iliyoketi Julai 18-20, mwaka huu jijini Dar es
Salaam.

Itakumbukwa kuwa wakati tulipokutana nanyi hapa Julai 20, mwaka huu baada
ya kikao hicho, tulisema kuwa kwa sababu Kamati Kuu iliazimia masuala
mengi, itakuwa vyema tukiyawasilisha kwa wanachama na umma wa Watanzania
hatua kwa hatua.

Katika kikao hicho, Kamati Kuu ilipokea taarifa ya sekretarieti, kujadili
kuhusu zoezi la uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea nchi nzima, na
kuazimia kama ifuatavyo;

1.2.1 Kamati Kuu iliazimia kuwa uchaguzi wa Baraza la wazee Taifa
utafanyika mapema zaidi ili kuwawezesha kusimamia uchaguzi wa viongozi
ngazi ya Taifa kwa mujibu wa katiba ya chama.

1.2.2 Kamati Kuu iliazimia kuwa uchaguzi ngazi ya Kanda utafanyika baada ya
uchaguzi wa ngazi ya Taifa, ili kuwezesha Mkutano Mkuu kufanya maboresho ya
Katiba kwa ajili ya kuwezesha ngazi hiyo kufanya uchaguzi kwa ufanisi zaidi

1.2.3 Kamati kuu imepitisha ratiba ya uchaguzi wa ndani ya chama kama
ilivyopendekezwa na Sekretariati, kama ifuatavyo;

Hadi tarehe 30/07/2014- kukamilika uchaguzi wa kata
Hadi tarehe 15/08/2014- kukamilika chaguzi za majimbo/wilaya
Hadi tarehe 30/08/2014- kukamilika chaguzi za mikoa
Tarehe 6/09/2014- Uchaguzi wa Baraza la Wazee
Tarehe 10/09/2014- Uchaguzi BAVICHA
Tarehe 11/09/2014- Uchaguzi BAWACHA
Tarehe 12/09/2014- Kamati Kuu
Tarehe 13/09/2014- Baraza Kuu
Tarehe 14/09/2014- Mkutano Mkuu
Tarehe 15/09/2014- Baraza Kuu
Tarehe 16/09/2014- Kamati Kuu Mpya

1.2.4 Kamati kuu imeagiza kuundwa kwa kamati ya kusimamia uchaguzi wa ndani
ya chama kwenye ngazi za Mikoa, Wilaya na Majimbo kwa mujibu wa Katiba ya
Chama Ibara ya
1.2.5 Kamati kuu inaagiza kuwa zoezi la kufanya ukaguzi wa uongozi ndani ya
chama na utekelezaji wa Chadema ni Msingi ni endelevu.
1.2.6 Kamati Kuu imeiagiza Sekretariati kufanyia maboresho ya fomu za
uchaguzi wa ndani ya chama na kuanza kuzisambaza kwenye ngazi husika kwa
ajili ya kutumika katika uchaguzi Mkuu ujao wa ndani ya chama . Aidha Miiko
ya Kikanuni kwa wagombea mbalimbali iwekwe kwenye fomu za kuomba kugombea
uchaguzi kama sehemu ya fomu husika.

PATA FOMU YA KUGOMBEA HAPA

1. UONGOZI WA KITAIFA WA CHAMA BOFYA HAPA
2. UONGOZI WA KITAIFA WA BAWACHA BOFYA HAPA
3. UONGOZI WA KITAIFA WA BAVICHA BOFYA HAPA
4. UONGOZI WA CHAMA NGAZI YA MKOA BOFYA HAPA
5. UONGOZI WA CHAMA NGAZI YA JIMBO/WILAYA BOFYA HAPA

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment