Muganda, ulichosema ni sahihi, lengo la vyama vya upinzani kama mwalimu alivyoainisha ni kukikosoa chama tawala kirudi kwenye mstari na kuchukua dola kitakapotetereka, je hayo malengo yanatimizwa? Au tunasaidiana na chama tawala kuyumbisha nchi? Mbatia atakosoaje serikali wakati yuko kwenye payrall ya nkuu wa kaya? Lipumba ataikosoaje ccm wakati wanandoa ya jinsia moja ya SUK kule Zanziber? Mbowe ataikosoaje ccm wakati anandoa ya mitaala na CUF kupitia UKAWA!
Kwa upande mwingine nakubaliana na mgonge, Kelele zote hizi kwa sababu chama cha centre party cha Norway kimepigwa mweleka na walioingia madarakani wamekuja na sera mpya wanahangaikia ya kwao zaidi.
----------
Sent from my Nokia phone
------Original message------
From: Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, July 29, 2014 10:29:24 AM GMT-0400
Subject: Re: [wanabidii] MASWALI MAGUMU YALIYOMSHINDA STEVEN WASSIRA UBUNGO PLAZA
Mngonge,
Naomba kutofautiana na wewe. Mwalimu aliamua uwepo wa vyama vya upinzani
baada ya kuona CCM inakwenda mrama bila kuwepo chombo chochote cha
marekebisho
au kuikemea. Ukifuatilia hotuba zake tangu alipostaafu, ukianza na ile ya
Singida 1986 alipokuwa anatembelea matawi ya CCM utatambua hayo. Katika
ule mkutano wa Februari 1992 Mwinyi alitaka utawala wa chama kimoja
uendelee, na Nyerere akasema mkiamua kuwa na utawala wa chama kimoja
mtaganda nao hata kama chama hicho kimegeuka kuwa kibovu. Huo ndio ulikuwa
msukumo wa Nyerere na wala si shinikizo ya "wanaume tunaowaomba."
em
2014-07-29 8:17 GMT-04:00 mngonge franco <mngonge@gmail.com>:
> Hosea Nyuma ya mambo kama haya ya ujio wa vyama vingi na uundwaji wa
> katiba kwa nchi kama ya kwetu yenye budget tegemezi huwa yana shinikizo la
> wanaume tunawaomba. Na si raisi kuwa wawazi katika hili huwa tuanjitahidi
> kutoa sababu za hapa na pale huku tukizikwepa sababu au mashinikizo yenyewe.
> Kimsingi serikali yetu ya CCm kupitia waziri wake pamoja na wabunge wa CCM
> tangu nyuma walikataa kuundwa katiba mpya kulingana na wakati wa sasa
> walisema iliyopo inatosha. Hivi mbona hawakutwambia sababu za kurejea tena
> na kukubali kuifanyia marekebisho katiba yetu? Hapa unagundua kuna
> shinikizo fulani la chini kwa chini lililowafanya na kugeuka kukubali kwa
> shingo upande kuifanyia marekebisho katiba yetu.
>
> Binafsi huwa nauliza swali moja kubwa kuhusu muundo wa serikali, hivi ni
> kweli muundo wa serikali mbili una gharama kidogo kuliko hizo tatu
> zinazopendekezwa? Utamsikia mtu akisema muundo wa serikali tatu una gharama
> kubwa bila kutufafanulia ni kwa namna gani? Nijuavyo mimi ukiondoa mambo ya
> muungano ukayapeleka kwenye muungano, serikali mbili za Zanzibar na
> Tanganyika zitabaki na mambo mache ya kushughulikia hivyo gharama zitakuwa
> zimegawanywa tu.
>
>
> Kwa sababu bado tuna nafasi ya kurekebisha muundo na uendeshajiwa serikali
> za Tanganyika na ile ya Zanzibar. Ni swala la kupitia rasimu na tukaja na
> muundo mpya utakao wapunzia madaraka na matumizi ya fedha hawa viongozi
> wawili wa Tanganyika na Zanzibar. Watuletee proposal inayoonyesha mipaka na
> matumizi ya huo muundo wa serikali tatu huku tukifananisha na haya matumizi
> ya muundo uliopo tuweze kuwa na informed decision. Siyo kutuhubiria uzushi
> na kutukaririsha maneno ya uwongo kwa maslahi binafsi. Dunia ingekuwa na
> watu wenye mawazo mgando tusingekuwa na ndege, gari, neno demokrasia, meli,
> computer na vingine vingi tu. Tuepuke kuwa dogmatised na wanasiasa wenye
> nia ya kujilimbikizia mali na madaraka
>
>
> 2014-07-29 6:30 GMT+03:00 <hosea.ndaki@gmail.com>:
>
> Hamis, tusilete siasa za pilato za wengi wape, ikumbukwe mwaka 1990 wakati
>> wa kuanzisha mfumo wa vyama vingi maoni ya wananchi wengi yaliukataa lakini
>> busara ikatumika. Hata hapa busara zinaweza tumika pia.
>>
>> Hamis, unasema shein ni amiri jeshi mkuu wa jeshi lipi? Ni command base
>> gani iliyoko zanzibar? Na kama ni wimbo wa taifa hata tff wanao, kama ni
>> mizinga hata kwenye mazishi ya koplo tunapiga tatizo liko wapi, kama
>> unadhani ni nchi huru dodoma wanatafuta nini? Siwakae hukohuko.
>>
>> Huyo mpemba wa uamsho aliuliza swali chokonozi wasira akaliona akalikwepa
>> kwa kujifanya hajalisikia. Kwanza ukumbi ulijaa wahuni huo mdahalo kwanini
>> hawa kuupeleka nkurumah hall? Wakamwalika na nape?
>>
>> Kama ni mapato 90% ya mapato yanatoka dar es salaam mbona mnyika hajadai
>> 90% yatumike dar es salaam? Kimara msewe hakuna maji, kawe barabara mbovu
>> sijui hata mkapa anaishi kawe au alishahama. Kuna mikoa ina barabara nzuri
>> umeme hadi migombani na ndio maarufu kwa ukwepaji kodi.
>>
>> 70% ya exports ni dhahabu na inatoka geita na kahama, kaone vituko huko
>> barabara zinajengwa kwa beleshi, lami inamwangwa kwa vikopo, bodaboda
>> zikipita inabanduka, barabara ya geita kahama haiwekewi lami na ndiyo yenye
>> maroli makubwa yaliyobeba sumu za migodini, badala yake inawekewa ya geita
>> nyanhwale yenye costa moja tu!
>>
>> Kaone lami inayozunguka stendi ya kahama ukikanyaga inabonyea kama
>> umekanyaga godoro la banco. Hayo hatuyaoni tunaona muungano tu.
>> ----------
>> Sent from my Nokia phone
>>
>> ------Original message------
>> From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
>> To: <wanabidii@googlegroups.com>
>> Date: Monday, July 28, 2014 8:13:31 AM GMT-0700
>> Subject: [wanabidii] MASWALI MAGUMU YALIYOMSHINDA STEVEN WASSIRA UBUNGO
>> PLAZA
>>
>>
>>
>> MASWALI MAGUMU YALIYOMSHINDA
>> STEVEN WASSIRA UBUNGO PLAZA HAYA HAPA:
>>
>> Swali la Kwanza;
>> Kama unaukataa muundo wa muungano wa Serikali tatu uliopendekezwa na
>> wananchi kupitia Tume ya Jaji Warioba kwa uchache wa Takwimu, wewe
>> unapendekeza uwepo wa Serikali mbili kwa Takwimu zipi?.
>>
>> Swali la Pili;
>> Je, gharama za kuuendesha muungano huu wa Serikali mbili za sasa ni
>> Shilingi ngapi, wananchi wa pande zote mbili tunataka ufafanuzi wa
>> Serikali
>> maana ni haki yetu ya kikatiba kufahamishwa gharama tunazotumia katika
>> kuiendeshea Serikali yetu kama walipa kodi, ili tufahamu na tulinganishe
>> na
>> gharama zilizoainishwa na Tume ya Jaji Warioba kwenye muundo wa Serikali
>> mbili kwa lengo la kupata ukweli wa hoja hii ya gharama.
>>
>> Swali la Tatu;
>> Awadhi alimuuliza Wassira kwamba, kama mgao wa mapato ndio kikwazo cha
>> muundo wa Serikali tatu kwamba Zanzibar watadai 50% ya mapato ya muungano
>> kama CCM wanavyotoa hoja, Kwani ni lini Zanzibar ilipewa 50% ya mapato
>> yote?
>> Mbona miaka yote Zanzibar inapewa 4% (asilimia nne) ya mapato yote ya
>> muungano?.
>>
>> Swali la Nne;
>> Kama muungano huu ni wa Nchi moja yenye Serikali mbili, ni kwa nini Rais
>> wa
>> Zanzibar ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Serikali ya mapinduzi ya
>> Zanzibar na ni kwa nini apigiwe mizinga ishirini na moja kama Rais wa
>> muungano?
>> Na kama hayo ni ya kweli, ni kwa nini hamtaki kukubali kwamba Tanganyika
>> ndiyo iliyovaa koti la muungano baada ya Zanzibar kutambuliwa na Katiba
>> yao
>> kama Nchi yenye mamlaka kamili?
>> Pia ni kwa nini mnakuwa ving'ang'anizi hata kwenye hoja za kweli na zenye
>> ushahidi wa wazi hata inafikia hatua hamtaki kukubali kwamba muungano huu
>> ni wa Nchi mbili zenye Serikali mbili badala ya muungano wa Nchi moja
>> yenye
>> Serikali mbili?
>>
>> Hapa hakuna muungano bali hiki ni kiini macho, tunaitaka Tanganyika yetu
>> sasa, na wazanzibar wanaitaka Zanzibar yao huru, maana nusu karne ya
>> unafiki na uongo wa CCM umefika mwisho sasa.
>>
>> Swali la Tano;
>> Kama mnaukataa muundo wa Serikali tatu, ni kwa nini Katiba hii iliyopo
>> hivi
>> sasa ya mwaka 1977 inatambua uwepo wa muundo huo wa Serikali tatu na hata
>> kufikia hatua ya kuwataja mawaziri watatu kwa kila Wizara, ikiwa na maana
>> kwamba, Waziri anayeshughulikia mambo ya muungano kwenye Wizara husika
>> ndani ya Bunge la muungano, Waziri wa Wizara husika na Waziri anayehudumu
>> kwenye Bunge la wawakilishi Zanzibar?
>>
>> Swali la Sita;
>> Tume zote zilizowahi kuundwa ili kukusanya maoni ya wananchi tangu uhuru
>> mpaka leo, nikiwa na maana ya Tume ya Jaji Kisanga, Tume ya Jaji Nyalali,
>> kundi la G55 na hii ya sasa chini ya Jaji Warioba, zote zimeleta maoni na
>> mapendekezo ya wananchi yenye muundo wa Serikali tatu.
>> Licha ya kwamba michakato yote hii ya Katiba mpya tangu enzi hizo mpaka
>> leo
>> imekuwa ikiwagharimu walipa kodi wa Taifa hili mabillioni ya Shilingi, ni
>> kwa nini kwa miaka yote hiyo mpaka leo Serikali hii ya CCM mmekuwa
>> mkiikwepa hoja hii ya msingi inayopaswa kufanyiwa kazi kwa maslahi ya
>> Taifa
>> zima.
>>
>> Lakini pia, mbona tunazo timu tatu za Taifa za mpira wa miguu?
>> Kwani Zanzibar Hilloes ni ya wapi kama sio ya Zanzibar?
>> Kwani Kilimanjaro Stars ni ya wapi kama sio ya Tanganyika?
>> Kwani Taifa Stars ni ya wapi kama sio Timu ya muungano?
>>
>> Kuna hoja gani nyuma ya pazia, inayowafanya muendelee kuifanya Zanzibar
>> kama koloni la Tanganyika?
>>
>> Nusu karne ya uongo ubabe na unafiki wa CCM na vibaraka wao, imefika
>> mwisho
>> sasa kwa sababu hiki sio kizazi cha analogia tena bali ni kizazi cha
>> digital.
>> Tunautaka ukweli na uwazi katika masuala nyeti na ya msingi kama hili la
>> kuivua Tanganyika Joho la muungano.
>>
>> Mwisho!
>>
>> Imeandaliwa na;
>>
>> Francis Boniface Garatwa,
>> Mwanaharakati wa CHADEMA,
>> Kanda ya Ziwa Mashariki,
>> Mkoa wa Mara,
>> Wilaya ya Serengeti.
>> 28/07/2014.
>> Email:francisboniface50@gmail.com
>> 0785881009/0767881009.
>> *********************
>>
>> Naomba kuwasilisha!
>>
>> Ahsanteni sana!!!
>>
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts
>> must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you
>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>>
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts
>> must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you
>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>>
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment