Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi amesema yeye pamoja na mawaziri wenzake watatu walikubali kuwajibika kutokana na makosa yaliyofanywa na askari waliokuwa wakitekeleza Operesheni Tokomeza Ujangili.
Dk Nchimbi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini (CCM), alisema kuna uhalifu wa hali ya juu katika mbuga za wanyama, ambao baada ya miaka 10 unaweza kumaliza wanyama kwenye mbuga hizo.
Akizungumza na wakazi wa Manispaa ya Songea kwenye Viwanja vya Kiblang'oma, Kata ya Lizaboni Songea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, alisema Serikali ilifanya uamuzi wa kuwasaka majangili na kuwatokomeza.
Alisema katika operesheni hiyo, wananchi wapatao 11 na askari sita waliuawa jambo lililosababisha matatizo makubwa...
"Baada ya kuonekana raia wamefariki kukatokea ushawishi wa kutaka baadhi ya watu wabebe dhamana ya askari ambao walionekana hawajatekeleza majukumu yao inavyotakiwa."
Alisema yeye na wenzake waliwajibika baada ya kutafakari kazi inayofanywa na askari katika nchi hii kwani wanalala usiku na kung'atwa na mbu kwa ajili ya wananchi, pia wanapambana na majambazi na hata kupoteza maisha wakati mwingine wakati wakilinda raia.
Hata hivyo, alimshukuru Rais Kikwete kwa kumpa heshima kubwa ya kumsaidia katika kipindi cha miaka minane na kuwatoa hofu watu wa Songea kwa kuwahakikishia kuwa kasi ya maendeleo katika jimbo lake haitapungua.
Uteuzi wa Dk Nchimbi na mawaziri wengine Khamisi Kagasheki (Maliasili na Utalii), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Dk David Mathayo (Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi) ulitenguliwa mwishoni mwa mwaka jana baada ya malalamiko ya wabunge kutokana na matatizo yaliyojitokeza kwenye Operesheni Tokomeza.
CCM Dodoma waishukia Chadema
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma, Paul Luhamo amewataka wananchi wa Dodoma Makulu kukikataa Chadema kwa madai kuwa viongozi wake wanaendekeza malumbano ndani ya chama chao.
Akizungumza katika maadhimisho hayo ya miaka 37 ya CCM katika Kata ya Dodoma Makulu, Wilaya ya Dodoma Mjini ambayo ni ngome ya Chadema, alitumia muda mwingi kuwaponda viongozi wa Chadema kuwa hawana jipya tena.
"Naomba mrudi CCM na kuweni na moyo wa kuchangia michango mbalimbali kwa ajili ya maendeleo yenu na watoto wenu hata kama Kata hii inaongozwa na Chadema," alisema Luhamo.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Dk-Nchimbi-aeleza-sababu-za-kuwajibika/-/1597296/2170542/-/do4fsg/-/index.html
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment