Thursday, 13 February 2014

Re: [wanabidii] Wingi wa Askari wa Usalama Barabarani na Matumizi Sahihi ya Muda wa Kazi na Rasilimali Watu

Ernest, nilikuwa mwanza hivi karibuni ni yaleyale, kuna kituo cha daladala karibu na mataa hiace zinapangana hadi wanaziba barabara trafik wapo wanatizama tu, wakiona gari inamatope kidogo wanajua imetoka porini unasimamishwa na kuambiwa umevuka barabara wakati taa nyekundu inawaka cha kushangaza gari la nyuma yako litaachwa liende.

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Ernest Mmbaga <emmbaga@hotmail.com>
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, February 14, 2014 4:01:49 AM GMT+0000
Subject: RE: [wanabidii] Wingi wa Askari wa Usalama Barabarani na Matumizi Sahihi ya Muda wa Kazi na Rasilimali Watu

Mathew.
Umeandika mabo ambayo ni kweli kabisa na yanhitajika kufanyiwa kazi, askari hao ni kila mji wako hivyo ulivyoeleza mfano hapa Arusha ukitaka enda Ngaramtoni utakutana na vikundi vya askari zaidi ya vinne katika umbali mfupi sana.

natamani ulioandika yawe makala katika gazeit na yasomwe na wengi hasa wahusika , labda watashtuka na kuelewa eti .

Ernest

Date: Thu, 13 Feb 2014 22:48:15 +0300
Subject: [wanabidii] Wingi wa Askari wa Usalama Barabarani na Matumizi Sahihi ya Muda wa Kazi na Rasilimali Watu
From: mathewmndeme@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com



Siku za karibuni nimekua
nikipita Barabara ya Morogoro kuanzia Ubungo hadi Mlandizi. Huu ni umbali wa
kama 50Km hivi. Ajabu katika umbali huu kuna polisi wa usalama barabarani wengi
sana kiasi cha kufanya barabara hii ionekane kama ni ya kuogofya au kuna
ukaguzi maalum au operation tokomeza madereva wabovu. Hata hivyo, sijasikia
kabisa uwepo wa operation hii, labda kama inafanyika kiintelejensia zaidi na kwa
mwaka mzima.


Katika kushangaa
wingi wa askari hawa, nilimekua nikihesabu makundi ya askari wa usalama barabarani
ambayo yanafika zaidi ya nane (hii ni kutoa walioko mizani Kibaha). Kuna sehemu
ya kipande cha umbali wa kama 5km unapotokea Kongowe kwenda Mlandizi, kunakua
na polisi makundi hadi manne walioko umbali wa chini ya 2km kutoka kundi moja
hadi jingine.


Vituo hivi
wanaposimama polisi, kuna askari zaidi ya wawili na kuna kundi linakua na askari hadi sita. Kwa hali hii unaweza
kujikuta unasimamishwa kila baada ya 2km au 5km na kila unaposimamishwa wote
wanauliza mambo yaleyale; wanakutaka uoneshe leseni yako, kadi ya gari, fire
extinguisher, kukagua bima na road license. Kibaya zaidi ni kuwa hakuna uratibu
au mawasiliano yanayoweza kukufanya ukikaguliwa kituo hiki usikaguliwe
kinachofuata. Hivyo unaweza kunajikuta unasimamishwa na kuulizwa mambo yaleyale
na kukaguliwa vitu vilevile kila baada ya umbali mdogo sana.



Mazingira ya barabara
hii na wingi wa magari haviruhusu sana dereva kukimbiza gari kwa mwendo wa kutisha.
Lakini kuna makundi kadhaa ya askari hawa wenye tochi za kupima mwendokasi na
wanafanya hivi kwa kujificha au kuvizia.


Kwa mtazamo wangu,
huu mpangilio au matumizi ya askari unahitaji kutizamwa upya kwa sababu
zifuatazo:

1.
Moja; ninaona kama haya
ni matumizi mabaya ya nguvu kazi na rasilimali watu. Kuweka kundi kubwa namna
hili la askari wa usalama katika umbali mdogo kiasi hiki ni kutumia rasilimali watu
vibaya. Ni gharama kubwa sana kuajiri watu na kisha kukawa hakuna kazi ya
kutosha kufanya na kufanya kazi ya mtu mmoja kuwa ya watu kumi.

2.
Mbili; Askari hawa
wanatumika kwa wingi hivi sehemu moja wakati ni kweli kuwa kuna uhitaji mkubwa
sana wa ulinzi na usalama kwenye maeneo mengi wanayoishi raia. Ninadhani ndugu
zetu hawa wangeweza kutusaidia usalama maeneo mengi mengine na tukawa na jamii
ambayo iko salama na amani zaidi ya ilivyo sasa

3.
Tatu: Ninaona kama huku ni
kutesa raia na waendesha magari pale ambapo gari linasimamishwa kila baada ya
muda na umbali mfupi na kuulizwa maswali yaleyale na kukaguliwa vitu vilevile. Katika
kupita njia hii na kusimamishwa kwenye umbali usiozidi 2km, niilimuuliza askari
mmoja ni kwa nini wana utaratibu mbaya hivyo; naye akakiri kuwa ni mfumo mbaya
na anaomba tushauri njia mbadala.

4.
Nne, kwa mtazamo wangu, hali
hii inachelewesha sana maendeleo na kuongeza umaskini kwa nchi yetu. Tayari tuna
tatizo kubwa la matumizi ya muda ambalo linachangia sana umaskini katika nchi
yetu. Kulazimishwa kupoteza muda zaidi bararabara kwa mambo yasiyo na tija ni kushindwa kuthamini matumizi sahihi ya muda
kama kiungo muhim sana cha maendeleo binafsi, familia, jamii na taifa

5.
Tano; Askari wengi hawana
haraka na hawaogopi kukupotezea muda wapendavyo. Unaweza kusimamishwa ukiwa na
kila kinachotakiwa na bado ukajikuta unapotezewa muda tu na mara nyingine
kuambiwa unapelekwa kituoni kwa jambo ambalo halina ulazima huo. Wengi wa askari
hawa wanashikwa na hasira wanapokukuta huna kosa.



Ushauri kwa Jeshi la Polisi:

1. Jeshi la polisi na seriakli kwa ujumla, liwekeze zaidi
katika kutoa elimu sahihi ya usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kudhibiti upatikanaji
wa leseni bila mafunzo, ili kuhakikisha kuwa watumiaji wa barabara wana elimu
na ufahamu wa kutosha kuhusu matumizi ya barabara na hivyo kuondoa ulazima wa kutumia
nguvu kubwa kusimamia sheria



2. Jeshi la polisi wajisikie vibaya kujenga kizazi na jamii
inayotii sheria kwa woga na shuruti na badala yake ifurahie kuwa na jamii
inayotii sheria kw akupenda. Kwa minajili hiyo, isiwekeze sana katika kutoa
adhabu na kuvizia makosa ya kuadhibu, bali wawekeze katika kuelimisha, kuelekeza
na kuongoza.




3. Kuna haja ya ungozi wa jeshi la polisi kushirikiana na
wataalamu wa fani zingine kama ICT kuangalia namna nzuri, rahisi, ya kisasa na
yenye gharama nafuu katika kufanya ukaguzi wa kawaida wa magari barabarani. Kwa
mfano, kwa magari yanayokwenda mikoani (hasa madogo) kunaweza kuwekwa utaratibu
kuwa, likashakaguliwa mambo ya msingi katika kituo cha kwanza (mfano kikawa
baada ya mbezi mwisho), kunakua na alama inayoonesha gari na dereva wana vigezo
vya kutembea njia kuu bila ukaguzi hadi mwisho wa safari; isipokua tu iwapo atatenda
kosa. Hili linawezekana kabisa ikiwa ni pamoja na kuwawezesha askari wa vituo
vingine kuhakiki (validate) ukaguzi husika.




4. Pamoja na unyeti wa kazi za walinzi hawa wa usalama wetu,
ni vema wakatambua umuhimu na unyeti wa muda katika kulitoa taifa letu hapa
lilipo. Ni shida kidogo unapokwenda umbali wa 50km na kutumia masaa kadhaa kwa
sababu tu ya ukaguzi wa kila hatua chache au kwa sababu askari fulani alijisikia
vizuri kukuonesha mamalaka yake kwa kukuweka barabarani muda mrefu au kukupeleka
kituoni bila kosa




5. Polisi wetu watambue kuwa karne ya watu kujazana Dar es
Salaam imepitwa na wakati. Ni wazi kabisa kuwa kwa sasa baadhi ya watu wanaweza
kufanya kazi au shughuli zao za kipato DSM na wakaishi nje ya mji kama vile Kibaha,
Mlandizi, Ruvu, Bagamoyo, Msata Chalinze na hata Morogoro. Hii inasaidia kupunguza
msongamano ndani ya mji na kuwawezesha watu kufanya shughuli zingine za uzalishaji
hasa kilimo ambacho ni ngumu kufanya hapa mjini. Kwa mfumo wa kupotezeana muda barabarani
ulioko sasa, hili haliwezekani; sio kwa vile maeneo haya ni mbali sana au kuna
foleni; bali ni kwa sababu ya ukaguzi wa polisi ambao ungeweza kuboreshwa na kuokoa
muda.




6. Jeshi la polisi lishirikiane na wataalamu wengine nje ya
jeshi lao kuona namna ambavyo watasimamia sheria na taratibu za barabarani kwa
rasilimali watu ndogo (askari wachache) na bado wakafanikisha majukumu yao kwa
ufanisi mkubwa. Hii haitaondoa tu usumbufu na matumizi mabaya ya rasilimali watu
na muda, bali itapunguza hata shutuma na rushwa zinazohusishwa sana na askari
hawa (bila kujali ni za kweli au uongo)






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com



Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma



Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment