Tuesday, 4 February 2014

Re: [wanabidii] Sijatangaza Kugombea Ubunge jimbo la Iramba-Magharibi , George Kidindima



Natamani na kundi la ZZK angekuwa na busara kama hizi

Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

From: Emma Kaaya <emmakaaya@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 4 Feb 2014 02:17:58 -0800 (PST)
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Sijatangaza Kugombea Ubunge jimbo la Iramba-Magharibi , George Kidindima

Ndugu zangu, mapema leo asubuhi BAVICHA-IRAMBA ikisema kuwa nimetangaza rasmi kugombea UBUNGE katika jimbo la Iramba-Magharibi. Hilo haliwezi kuwa tangazo langu rasmi kwa sababu zifuatazo:-

1. Mgombea wa nafasi kubwa na nyeti kama hiyo hawezi kusemewa na yeyote ila yeye binafsi. Hivyo basi kama nia hiyo ninayo nitatangaza rasmi mimi mwenyewe muda wakufanya hivyo ukimea (ukiwadia).

2. Jumuiya ya chama (kama ilivyo Bavicha) sio haki kumuunga mkono mwanachama yeyote ambaye hata hajaidhinishwa na chama kugombea nafasi husika. Hii inaleta picha mbaya kwa yeyote mwingine mwenye nia yakugombea nafasi husika.

3. Muda wakutangaza kugombea haujafika hivyo kufanya hayo ni ukiukwaji mkubwa wa katiba ya chama pamoja na kanuni zake. Napenda ieleweke kuwa mimi kama Mwanasheria na mdau wa siasa kwa muda mrefu naielewa Sheria ya usajili wa vyama vya siasa nchini, na katiba ya CHADEMA naielewa KINDAKINDAKI ("in and out"), hivyo siwezi kuikiuka kwa namna iwayo yote.

Aidha nimesikitishwa sana na Baraza hilo la vijana la CHADEMA kwakunilisha maneno na kusema uongo kuwa nilitoa matamshi hayo pale Katala Beach Hotel, jambo hili sio la kweli.

Kwa ufafanuzi tu kuhusu hili ni kwamba miezi takribani miwili kasoro iliyopita nilialikwa hotelini hapo kwa ajili ya uzinduzi wa filamu ya "SIO KOSA LANGU" iliyoigizwa na wanafunzi wa chuo cha uhasibu (T.I.A-Singida Campus).

Pale sikuongelea suala lolote la kisiasa kama nilivyoripotiwa na BAVICHA-IRAMBA zaidi yakutoa mchango wangu na kushiriki mnada wa DVD hizo.

Nawaombeni radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza, hasa wale wenzangu wenye nia ya kugombea nafasi hiyo adhimu, nawaambia msizimie moyo mapambano yangali bado. Aidha nawashukuru nyote mliofurahishwa na tangazo hilo na kunitia moyo kuwa naweza, napenda muelewe kuwa hili ni suala la muda tu, ukifika na nia ikingali basi nitawaombeni ushirikiano.

Asanteni sana.
George Kidindima,
04/02/2014.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment