Saturday, 1 February 2014

Re: [wanabidii] MZEE MALECELA NA PAUL MAKONDA WAOMBE RADHI KWA VIONGOZI WA DINI

uchaguzi 2015, katiba mpya ni kipima joto tosha kwa siasa za tz


2014-02-01 Emma Kaaya <emmakaaya@gmail.com>:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARITAREHE 1 FEBRUARI 2014
MZEE MALECELA NA PAUL MAKONDA WAOMBE RADHI KWA VIONGOZI WA DINI
0.1 Kitendo alichokifanya hivi karibuni Ndugu Paul Makonda Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji pale alipoongea na vyombo vya Habari pamoja na mambo mengi aliyoyaongea kubwa zaidi ni alipotamka wazi kwa kuwatuhumu baadhi ya Viongozi wa Dini kwa kutoa maneno ya kejeri na dharau dhidi yao kuwa “MASHEIKH NA MAASKOFU WAKIWEMO NA VIJANA WANAOTAKA FEDHA ZA BURE WAENDE KWA EDWARD LOWASA” kitendo ambacho hakuwatendea haki wala adabu Viongozi hawa wa Dini.

Kitendo hicho cha kuwakejeri na kuwadhalilisha ni utovu wa Nidhamu wa hali ya juu sana, kwani kauli aliyoitoa kila Muumini ilimshitua sana, kwani ni kauli haikupaswa kutolewa na Kiongozi wa Vijana aliyekuwa katika nafasi Muhimu ya Uongozi wa Jumuiya Kitaifa, kwani kauli yake hiyo yenye ukakasi wa hali ya juu sana imempa kichefuchefu kila mmoja anaewaheshimu Viongozi wa Dini, kwani Viongozi wa Dini wanaheshima zao binafsi na kuheshimika Duniani kote na mpaka Serikali huwaomba Viongozi wa Dini kushiriki pamoja kutatua na kushauriana katika maswala mbalimbali yanayoizunguka jamii.

Kauli hiyo ni nzito sana aliyoitoa Ndugu Paul Makonda sio ya kuipuuza hata kidogo na kuicha hivi hivi nina muomba kwa Heshima na taadhima Mwenyekiti wa Vijana wa Taifa awathibitishie Watanzania kuwa kauli aliyoitoa Ndugu Paul Makonda ni ya Umoja wa Vijana au ni yake binafsi. Kwani mimi binafsi nimekuwa katika Umoja wa Vijana kama Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Shinyanga mstaafu na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Taifa lakini pia Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Umoja wa Vijana Taifa, nafahamu kauli au matamko mazito kama yaliyotolewa na Ndugu Paul Makonda hutolewa na Mkutano mkuu wa Taifa, Mkutano wa Baraza Kuu Taifa na hata kamati ya Utekelezaji Taifa.Mimi siamini kama hiyo ni Kauli ya Umoja wa Vijana kwa kadri ninavyofahamu utaratibu ndani ya Jumuiya na Chama kwa ujumla, sasa tunajiuliza huyu kijana kauli hizi nzito nzito ambazo hazilingani na umri wake na wala hadhi ya kiuongozi aliyonayo anazitowa wapi huenda tunaamini kuna kundi au genge la mahafidhina liko nyuma yake lililoamua kumtumia aidha kwa kujua au kwa kutokujua.

Jambo jingine muhimu alitutuhumu pia sisi yani mimi Khamis Mgeja, Mzee Mgana Msindai na Ndugu John Guninita kuwa alidai t--------- na Ndugu Edward Lowasa, tuhuma hizi si za kweli hata kidogo napenda Watanzania wafahamu tuhuma zote mbali mbali ambazo kijana huyu amekuwa akitushutumu si za kweli na ni za kipuuzi ninaiomba jamii kumpuuza kwani Ndugu Makonda bado mchanga kisiasa anatafuta umaarufu kwa kasi kwa kutumia migongo yetu sisi wakongwe kisiasa, kwani sisi aliotutuhumu atambue sisi ni wakongwe na ni Magwiji katika siasa za kiungwana hapa Tanzania, tunauwezo wetu binafsi wa kufikiri na kuamua kile tunachokiamini kwa maslahi ya Chama na Taifa kwa ujumla, kwa ujumla tunataka Ndugu Paul Makonda na washirika wake waache kelele ambazo wamekuwa wakilalamika mara kwa mara hii ni dalili ya kuelemewa ndio maana hawaishi kumsemasema na kumkejeri Ndugu Edward Lowasa wakati ambapo jamii inamuona kuwa ni mtu wa msaada mkubwa katika kuchagiza maendeleo kwa kushirikiana na jamii. 
Kijana Makonda atambue sisi tumewekeza jasho jingi katika chama hiki na kamwe hatutokubali kudhalilishwa na kijana mchanga wa kisiasa kama huyu, pia kama ni kuwekeza jasho sisi tuna debe ishirini yeye hata robo hajafikisha katika medani za kisiasa kwa hivyo anafanya maajabu ya kisiasa ni maajabu ya panya kufukuza paka na anacheza ngoma asiyoijuwa.Pia jamii inamuona Ndugu Edward Lowasa ni mtu muungwana, mwenye uwezo mkubwa wa kiutendaji, mwenye ushauri na ushawishi mkubwa katika machangizo ya maendeleo, sifa kubwa nyingine ya ziada ni uvumilivu na hasa kuwavumilia watu wenye kumrushia madongo kama Paul Makonda na genge lao la mahifidhina.

Kuhusu kauli aliyoitamka Ndugu Makonda ya kwamba Ndugu Edward Lowasa hawezi kuwa Rais kauli hii imetoa picha ya kuyajuwa yaliyofichika katika fikra za kundi hili la wahifidhina lakini pia watambue maamuzi yote hufanywa na Vikao halali vya chama na jumuiya zake, na wakati ukifika vikao vitaamua na si Makonda na marafiki zake.

0.2 MZEE MALECELA KUPONGEZA KAULI ZA KASHFA DHIHAKA NA KEJERI DHIDI YA VIONGOZI WA DINI Kufutia tukio la hivi karibuni la kijana Paul Makonda kutoa maneno ya kashfa kejeri na dhihaka dhidi ya viongozi wa Dini, baadhi ya wanasiasa na vijana maaajabu makubwa kutokana na kauli hizo za Makonda tumemshangaa Mzee Malecela kuibuka na kuunga mkono na kumpongeza kijana huyu mtovu wa nidhamu.

Tulitegemea kila Mtanzania kwamba baada ya kauli hizo Mzee Malecela angeibuka na kumuongoza njia sahihi na kumpa ushauri kijana huyu aliyepotea kimaadili wa kwenda kuwaomba radhi na kuwaangukia viongozi wa Dini, ndugu Edward Lowasa, Ndugu Khamis Mgeja, Ndugu Mgana Msindai, Ndugu John Guninita ikiwemo na vijana kwa ujumla.
Maajabu makubwa jambo ambalo Watanzania hawakutegemea jinsi wanavyomfahamu Mzee Samwel Malecela na heshima yake, tulitaraji kuwa Mzee angemkemea kijana huyu mtovu wa Nidhamu badala yake anampongeza na kumuunga mkono na kuwataka Watanzania wamuunge mkono kwa kauli zake za utovu wa Nidhamu ambazo hazina tija kwa Chama na maendeleo ya Taifa kwa ujumla, pia katika maajabu mengine Mzee Malecela alimshambulia mwanachama mwenzake Ndugu Edward Lowasa kwa kumtuhumu kwa tuhuma nyingi mbalimbali ambazo hana ushahidi nazo.Mzee Malecela amesahau huko nyuma yeye alishawahi kutuhumiwa kuwa alipewa fedha kutoka nchi za uarabuni na mpaka kubadilisha dini na kuitwa jina la JUMANNE ili aungwe mkono kupewa nguvu za kugombea Urais.

Kuhusu uchu wa Urais anaomtuhumu Ndugu Lowasa amesahau yeye ndiye ana uchu mkubwa sana wa Madaraka alikuwa akiomba nafasi za ndani ya Chama haswa kwa kiti cha Urais kwa awamu mbalimbali akaonekana hafai na hatoshi na mpaka jina lake likawa halipitishwi na chama baada ya kumgundua ni dhaifu na anakasoro kubwa za kimaadili na mpaka ikapelekea Baba wa Taifa akachoka kumvumilia na hatimae alimtungia kitabu “UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA” hii ni kuonyesha kuwa Mzee Malecela alikuwa sugu wa matatizo yaliyokuwa yakikiuka maadili.Jambo jingine alilokuwa nalo la uchu wa madaraka Mzee Malecela ni pale alipong’ang’ania kiti chake cha ubunge bila kujali umri wake na wananchi wa jimbo la Mtera ilifika mahala walimchoka baada ya kugundua anasinzia Bungeni na kwenye jimbo laketulishuhudia Kibajaji kikiliangusha Katapila maana yake aliangushwa ubunge na mtoto mdogo Mhe Livingstone Lusinde.Jambo jingine Mzee Malecela ameshindwa kutambua wanaokivuruga chama ni wale wanaozungumza nje ya vikao halali vya chama na jumuiya zake na kuyageuza kuwa ndio msimamo wa chama au jumuiya. 

Kwa hivyo Mzee Malecela kuendelea kutushambulia hatutendei haki kwani hakuna shughuli yoyote ya chama iliyokwama kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa kwa sababu yetu sisi.
NINAPENDA KUTOA USHAURI KWA MZEE MALECELA, MAKONDA NA WATANZANIA WENZANGU KWA UJUMLA, Tanzania kama taifa tumefika pabaya kwani kila mmoja amebaki kuwa mlalamikaji na kutuhumiana pasipokuwa na ushahidi hili jambo ni hatari kwa mustakbali wa nchi kwani hivi sasa baadhi ya watu wanamgeuza Ndugu Edward Lowasa kuwa ni agenda ya kitaifa huku wakiacha mambo muhimu ya nchi na maisha ya watanzania.kwani tulitegemea wazee wetu kama kina Mzee Malecela watushauri vipi taifa linaweza kukabiliana na changamoto zilizopo hivi sasa kwa mfano deni la taifa, mchakato wa Katiba Mpya, matatizo ya umasikini, tatizo la ajira kwa vijana, hombwe kubwa kuwahi kutokea baina walionacho na wasionacho, mauaji yanayotokea sasa maeneo mbalimbali kati ya wakulima na wafugaji ikiwemo kuchomeana nyumba, mauaji ya kikatili kule Tarime na maeneo mbalimbali nchini, ajali mbali mbali za barabarani zinazouwa nguvu kazi ya Taifa, tatizo kubwa la rushwa, uporaji wa rasilimali za Taifa na ujangili wa kutisha, Tanzania kutumika kama korido la kupitishia madawa ya kulevya na binadamu, oparasheni tokomeza, wananchi kujichukulia sheria mkononi, ubadhilifu wa mali za umma haswa ukizingatia ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na taarifa za kamati mbalimbali za bunge, jambo jingine kubwa lilipo kwa sasa ni kuhusu rasilimali ya gesi iliyovumbuliwa kwa wingi nchini wakati taifa lipo katika mchakato wa kutunga sera na sheria ya gesi na mafuta.

Mzee Malecela na wenzake hayo yaliyotajwa hapo juu ndio mambo muhimu yanayogusa nchi na sio mtu Lowasa Lowasa Lowasa tulitegemea atushauri Tanzania kama taifa tufanye nini Watanzania kwa kushirikiana na Serikali yetu kwani matatizo hayo yanahitaji ushirikishwaji baina ya wananchi na Serikali yao, Watanzania wangeyapata hayo kupitia uzoefu wake kama alivyowahi kuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Makamu wa Mwenyekiti wa CCM kuliko maajabu ya kuonyesha Flana yenye maneno ya “FRIENDS OF LOWASA” kuwa kama ndio tatizo la Taifa.

Mzee Malecela kuwaonyesha Watanzania Flana ya Lowasa ndio tatizo la taifa hii inaonyesha wazi Mzee amechoka na amefilisika kifikra na anazeeka vibaya ninapenda nimpe ushauri wa bure Mzee wangu atulie alinde heshima yake.Pia napenda nitoe ushauri kwa Mzee Malecela, Paul Makonda pamoja na washirika wao wasome alama za nyakati na waangalie mahitaji ya siasa kwa sasa na waone Watanzania wanamuhitaji Kiongozi wa namna gani wa Tanzania ya kesho, ninawaomba wakubali yaishe wasije kupinganaTanzania na nguvu ya umma na upepo wa kisisa kwa sasa na pia watambue mpaji ni MUNGU alitakalo MUNGU hakuna mwanadamu atakaelizuia.

NAWATAKIA KILA LA HERI KATIKA UJENZI WA TAIFA

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA

TAARIFA HII IMETOLEWA NA NDG KHAMIS MGEJA

………………………………………….

01/02/2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment