Friday, 14 February 2014

Re: [wanabidii] Maoni ya Zitto Kabwe kuhusu Mashine za EDF

Magere, tunaweza tafuta competitive advantage ya kutumia mtandao huu badala ya kutisha watu na mkono wa sheria, mfano efd zinaweza kuwa programed kiasi ukiingiza taarifa ya mauzo inapiga hesubu ya kodi automatic, pia ikaunganishwa na mtandao wa mpesa unalipia kodi palepale, hivyo mfanyabiashara analipa kodi kilasiku kidogo kidogo, mfano kama mtu kodi yake ni shs elfu tisini kwa mwaka badi atalazimika kulipa shs elfu tatu kwa siku tena kwa mpesa.

Tungekuwa tunalipia maegesho ya magari kwa mwaka ingekuwa vurugu kweli lakini unalipa mia tatu kila unapoegesha hatuoni kama ni mzigo kulipa ila ukijumlisha kwa mwaka ni pesa nyingi.

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Johale Magere <johale14@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, February 14, 2014 7:44:59 AM GMT+0300
Subject: Re: [wanabidii] Maoni ya Zitto Kabwe kuhusu Mashine za EDF

Kukusanya kodi ni jambo moja na jinsi gani kodi hiyo inatumika ni jambo
lingine.mfanya biashara hawezi kulipa kodi kwa hiyari bila kuwepo sheria
inayo mbana.kuna kundi kubwa la waajiriwa ambao hawana mlango wa kukwepa
kodi na ukiangalia gross salary na take home unakuta tofauti kubwa wakati
huo wafanya biashara wananeemeka kwa kuingiza kipato kikubwa kinachotokana
na kukwepa kulipa kodi.
Wengi wetu ni mashahidi ukienda dukani unaulizwa kama unataka risit na hapo
bei itakuwa tofauti kama hutohitaji risit.hii inaonyesha wazi ni jinsi gani
wafanyabiashara wa tanzania walivozoea kukwepa kuliapa kodi.nadhani hapa
tujadili mapungufu yanayotokana na mfumo mzima wa ulipaji kodi,ikiwepmo
kiwango kikubwa ambacho ni mzigo kwa mlipakodi na sio kukataa kutumia
mashine hizi

Magere J.
On Feb 13, 2014 8:52 PM, "ELISA MUHINGO" <elisamuhingo@yahoo.com> wrote:

> Naomba nisijadili ila nitoe angalizo ambalo nalo linahitaji kujadiliwa.
> mwishoni mtoa hoja anasema 'Tutaendelea kuwa wategemezi kama hatutajenga
> utamaduni wa kulipa kodi----'
> Nimekuwa na mawazo mawili kuhusiana na ulipaji kodi wa Tanzania.
> Mapato yakiongezeka yanamsaidiaje mlipa kodi? Inategemewa kuwa kama taifa
> lililenga mathalan kukusanya trilioni 11. Kama hizi mashine zitaongeza
> mapato itarajiwe kuwa mlipakodi hutu ambaye nadhibitiwa na mashine hizi
> atafaIDI KWA kiwango cha kodi kupungua. Maana yangu kama hizi trilioni 11
> tuna uhakika wa kuzipata basi kodi ipungue huku tunazipata.
> Jingine ni matumizi ya kodi hizi. kama ongezeko la mapato likiishia
> kuongeza mapato ya wanasiasa na wakusanyaji basi anayetozwa ni dhahili
> anaumia.
> Historia inaonyesha kuwa kadri mapato ya taifa yanavyoongezeka marupurupu
> ya watawala na wengine wachache yanaongezeka na wananchi wanaendelea
> kuambiwa taifa ni maskini. Ijulikane kuwa kama barabara hazitatengenezwa
> mlipa kodi anaendelea kuumia na makusanyo yanazidi kuongezeka maana moja
> kati ya vyanzo ni vipuri vya magari ambavyo vitanunuliwa sana kwa sababu ya
> ubovu wa barabara.
> kama huduma za hospitali hazitaboreka kwa sababu watawala wanatibiwa nje
> huyu mlipa kodi anazindi kuumia.
>
> Ipo kazi ya kufikiri kwa moyo na kwa ubongo juu ya jambo hili. Matamko ya
> TRA kwa mashine hizi lazima zitumike hayatasaidia ieleweka kuwa punda mtoni
> atakwenda lakini anaweza kugoma kunywa maji.
>
>
>
> On Thursday, February 13, 2014 8:46 AM, Abdalah Hamis <
> hamisznz@gmail.com> wrote:
> EFD zilianza kutumiwa mwaka 2010 kwa jumla ya wafanyabiashara 16,000
> waliosajiliwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
>
> Mwaka wa fedha 2009/2010, kabla ya EFD, makusanyo ya kodi ya VAT yalikuwa
> tshs 791 bilioni.
>
> Mwaka 2011/2012 makusanyo yaliongezeka kwa asilimia 40 mpaka tshs 1,086
> bilioni.
>
> Mwaka 2012/2013 makusanyo yakaongezeka kwa asilimia 63 mpaka kufikia tshs
> 1,770 bilioni. Makusanyo haya ni kwa Wafanyabiashara 16,000.
>
> Iwapo awamu ya pili ya EFD itatekelezwa bila vikwazo jumla ya
> Wafanyabiashara 200,000 watafikiwa ikiwemo ni pamoja na vituo vya mafuta
> (Petrol Stations), Mahoteli na Migahawa nk. Mamlaka ya Mapato
> inatarajiakukusanya zaidi ya tshs 3,500 bilioni kutoka VAT peke yake iwapo
> EFD zitatumika.
>
> Wafanyabishara kote nchini wanalalamika. Mwanzoni hoja kubwa ilikuwa ni
> bei za mashine hizi. Hoja inayoeleweka kabisa. Kamati ya PAC iliwahi
> kushauri kuwa Wafanyabiashara wapewe bure kabisa mashine hizi (bila
> kusubiri kurejeshewa kupitia kodi. Kimsingi mashine hizi ni Bure isipokuwa
> Mfanyabiashara huikopesha TRA na TRA kumrudishia kupitia kodi ya Mapato
> katika mwaka wa kwanza wa matumizi).
>
> Leo nimesoma kwenye vyombo vya habari wafanyabiashara wanataka mashine
> hizi zisitumike kabisa, mpango mzima ufutwe. Ni kweli Wafanyabiashara wa
> Tanzania hawataki kabisa mashine hizi?
>
> Wafanyabiashara wanasema kodi ya VAT ya 18% ni kubwa mno na inakatwa bila
> kuzingatia manunuzi yao ie gharama zao za uzalishaji. Siku zote VAT
> inakatwa kutoka kwenye mauzo ghafi au kutoka faida?
>
> Hebu tujadili masuala haya na yale malalamiko ya msingi yafanyiwe kazi na
> yasiyo ya msingi yapuuzwe.
> Tutaendelea kuwa Taifa tegemezi iwapo hatutaweza kujenga utamaduni wa
> kulipa kodi. Nchi hii haina mjomba.........
>
>
> source:facebook.com/zittokabwe
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment