Saturday, 15 February 2014

Re: [wanabidii] MAONI YA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU TATIZO LA UJANGILI

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, February 14, 2014 12:14:17 AM GMT-0800
Subject: [wanabidii] MAONI YA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU TATIZO LA UJANGILI

Napenda kuchukua nafasi hii kama waziri kivuli wa maliasili na utalii
katika kuishinikiza Serikali hasa waziri wa maliasili na utalii, Mhe.
Lazaro Nyalandu kutoa majibu ya maswali magumu ambayo si Tanzania tu pekee
inayahitaji lakini pia Jumuia ya kimataifa inayahitaji kuhusu kukithiri kwa
tatizo la Ujangili nchini hasa kwa wanyama jamii ya Tembo na Faru.
Hivi karibuni gazeti la Daily Mail linalochapishwa nchini Uingereza
liliripoti kuhusu biashara haramu ya pembe za ndovu ambayo inakadiriiwa
kuwa na soko la shilingi trilioni 19 za kitanzania.

Pamoja na majibu ya waziri Nyalandu ambayo yalilenga kuhaminisha watanzania
kuwa taarifa ile imelenga kuchafua Tanzania, anasahau kuwa huo ndio ukweli
halisi kuwa Tanzania sasa imejichafua yenyewe kwenye taswira ya kimataifa
kwa citendo hivyo haramu.
Labda waziri Nyalandu anasahau kuwa, ulimwengu wa sasa ni wa kiteknolojia
ambapo taarifa mbalimbali juu ya biashara haramu ya pembe za ndovu pamoja
na mauaji ya tembo, yamesambaa kila mahali hasa katika vyombo vya habari
vya ndani na nje ya nchi ikiwemo mitandao mbalimbali ya kimawasiliano.

Leo hii wakati waziri akitumia nguvu nyingi kupangua tuhuma dhidi ya
Serikali katika kushindwa kwake kuangamiza biashara hii haramu, anassahau
pia takwimu za serikali zinaonesha kuwa mwaka 2010 tembo 10000 waliuwawa
Tanzania pekee. Hii ni wastani wa tembo 37 kwa siku. Hivi sasa Tanzania ina
tembo kati ya 150,000 na 170,000 . ina maana kuwa mpaka kufikia mwaka
2017/2018 Tanzania inaweza isiwe na tembo hata mmoja. Kwa takwimu hizi,
waziri anawezaje kusema kuwa Serikali inachafuliwa?

Mara kadhaa pia, waziri Nyalandu amekua akikaririwa kuwa mtandao wa
Ujangili ni mpana na wenye nguvu za pesa, kisiasa na kimamlaka. Na pia
amekaririwa akiwasihi wanaojihusisha na shughuli za Ujangili waache mara
moja kwani serikali inawajua. Swali, unawezaje kumbembeleza mtuhumiwa huku
ukijua anavunja sheria za nchi? Je kuna watu ambao katika nchi inayojisifu
kuwa na utawala bora, wako juu ya sheria na hawaguswi na sheria?

Majibu haya ya waziri, yanadhihirisha kuwa mtandao huu unaolalamikiwa na
kuogopwa ndo unahousisha Ikulu, wanasiasa, watumishi wa Serikali, maafisa
wanyamapori,maafisa usalama, polisi, wanajeshi na wafanyabiahsara wakubwa
ambao wamekua wakihushishwa na Serikali hii ya CCM.

Kambi rasmi ya upinzani katika hotuba zake za bajeti na michango ya mara
kwa mara, imekua ikitoa msimamo wake ikiwa ni pamoja na kuwataja baadhi ya
watuhumiwa wa Ujangili na vidhibiti vinavyoonesha biashara haramu dhidi ya
tembo inavyofanywa. Je , waziri anaweza kutueleza kuwa ameshirikiana vipi
na Kambi ya Upinzani katika kushughulikia watuhumiwa hao, ikiwemo kufanya
upelelezi na kujidhihirisha kama watuhumiwa hao wana au hawana hatia?

Waziri Nyalandu, akiwa na dhamana ya kusimamia utekelezaji wa sera na
sheria za nchi katika wizara yake ya Maliasili na utalii, wamechukua
jitihada gani zaidi ya kukamata meno na pembe za ndovu au faru? Vipi kuhusu
kuzuia zaidi wanyama hao wasipotee katika sura ya taifa letu? Je waziri
anayo habari kuwa kituo cha ITV cha Uingereza, kiliweza kurekodi jinsi
mtandao wa Ujangili unavyofanya kazi katika Tanzania mpaka China? Serikali
imechukua hatua gani kufuatilia habari hiyo ya kipelelezi na kuwatia
hatiani watuhumiwa walioonekana wakifanikisha upatikanaji wa pembe za ndovu
pamoja na ahadi za kupata pembe nyengine kwa dau kubwa?

Pamoja na Serikali kuona jambo hili ni dogo, lakini wanasahau kuwa jumuia
ya kimataifa hipo makini katika kulinda viumbe hai vilivyo hatarini
kupotea. Kutokana na kitendo cha waziri mwenye dhamana kushindwa kujibu
tuhuma nzito kama zinazotolewa na vyombo vya habari za kimataifa na kuishia
kutoa maneno yasiyokuwa na ushahidi ama vielelezo vyovyote vile kwa umma ni
dalili za wazi kuwa tuhuma hizo zina ukweli na ni muendelezo wa ukweli
ambao niliutoa Bungeni mwaka 2012 kwa kutaja jina na Meli ambayo ilihusika
kubebea shehena ya Meno ya Tembo ambayo wakala wa Meli hiyo ni Katibu Mkuu
wa CCM Kinana.

Katika tuhuma hizo nzito serikali ya Tanzania imetuhumiwa kwenye mambo
mazito yafuatayo na ambayo hayajatolewa majibu na Waziri wa Maliasili na
Utalii kwa kuwa hana majibu kutokana na ukweli wa taarifa zenyewe

Tuhuma hizo nzito na ambazo ni lazima zipatiwe majibu ya kina na tunataka
kupata majibu ni kama ifuatavyo ;

1. Kuwa watu walio karibu na Mhe. Rais Kikwete wanahusika katika biashara
hii haramu ya meno ya Tembo ndio maana serikali yake haichukui hatua
stahiki katika kukabiliana na jambo hilo

2. Kuwa Ndege iliyomleta rais wa China Mwaka jana iliondoka na shehena ya
Meno ya Tembo ambayo ilipakiwa na Maafisa waliokuwamo kwenye ndege hiyo

3. CCM na serikali yake ni wanufaika wakubwa wa mradi huu kwani wanatafuta
fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao ndio maana hawachukui hatua kwa
wahusika ambao wanajulikana kwa majina na wapo mitaani wakiendelea na
biashara hiyo haramu
4. Wanasiasa wa ngazi za juu katika serikali ni wahusika wa moja kwa moja
katika biashara hii haramu na wapo Wabunge kutoka CCM ambao ni wahusika wa
biashara hii.
5. Je ni kweli kuwa vitendo vya Ujangili vimeongezeka kwa kasi katika
utawala wa Kikwete kuliko waliomtangulia?

Tunamtaka waziri Nyalandu atoe majibu ya kina na yakuridhisha kuhusiana na
tuhuma hizo nzito kwa vielelezo na sio kwa kuishia kusema hizo ni taarifa
za uongo bila kuonyesha zipi ni taarifa za kweli , na akumbuke kuwa tuhuma
hizi hazijaanza kutolewa leo au jana kwani hata mini nilizitoa kwenye Bunge
wakati nawasilisha hotuba ya waziri kivuli wa maliasili na utalii, pia kuna
ushahidi na vielelezo viilivyotolewa na kamati ya Bunge iliyoongozwa na
James Lembeli (na hapo taarifa ilisema kuna wabunge wanahusika na vigogo wa
Serikali) mbona hakuwahi kusema kuwa taarifa zote hizo zilikuwa ni za
uongo? Na mpaka sasa wamechunguza tuhuma ngapi?






*Imetolewa na …………………. Mhe. Mch. Peter S. Msigwa(MB), Waziri Kivuli wa
Maliasili na Utalii*

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment