Friday, 14 February 2014

Re: [wanabidii] Lowassa, Sumaye, Ngeleja wajieleza Kamati ya Mangula

Nimependa majibu ya Lowassa kwamba “Mazungumzo yalikwenda vizuri. Yalikuwa na lengo la kujenga chama kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,”  aliongeza kuwa hapakuwa na kulaumiana.

Kweli Lowassa anaogopwa na yeye mwenyewe anajua kwamba wanamuogopa ndiyo maana alijiamini na kusema kilichoendelea huko ndani wakati akina Sumaye na Ngeleja waliogopa hata kusema nini kiliendelea.

Binafsi najiuliza hivi huko ndani ya hiyo kamati ya Mangula nani ana ubavu wa kumuuliza Lowassa maswali ya kumshutumu? Nani jasiri ndani ya sisiem anayeweza kudhubutu kumuuliza maswali Lowassa jabali la siasa za kuchumia tumbo, tia mchuzi hapa kwangu pakavu?

 Nafikiri Lowassa kasema ukweli kwamba kilichoendelea ni kumpoza na kumuomba awasaidie namna ya kuibuka washindi uchaguzi ujao, wala si kumuhoji kwa lolote juu ya kuvunja taratibu za chama.

Dalili hizi kweli zinaashiria kwamba hakuna zaidi ya Lowassa ndani ya sisiem na pengine wangeitwa wengine wakaohojiwa na kuonywa huku wakimuacha Lowassa aendelee na harakati zake za kuusaka upresident



2014-02-14 11:11 GMT+03:00 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>:

Waliowahi kuwa Mawaziri Wakuu; Edward Lowassa na Frederick Sumaye jana walifika mbele ya Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM kutoa maelezo juu ya tuhuma za kufanya kampeni za urais kabla ya wakati.

Mbali na wastaafu hao, mwingine ambaye jana alifika mbele ya kamati hiyo ambayo ilikuwa chini ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana ni Waziri wa Nishati wa zamani na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.

Mjumbe mwingine wa kamati hiyo aliyehudhuria kikao hicho kilichofanyika kwenye Ukumbi wa White House jana ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi. Wajumbe wengine ni Dk Maua Daftari, Shamsi Vuai Nahodha na Pindi Chana ambao hata hivyo, hawakuhudhuria.

Hata hivyo, wanachama wengine watatu, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, Waziri wa Nchi (Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira na Naibu wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba ambao wote wanatazamiwa kuitwa leo mbele ya kamati hiyo.

Vyanzo kutoka ndani ya chama hicho vilieleza kuwa Membe alikuwa katika ziara ya Rais Jakaya Kikwete na alitarajiwa kurejea nchini jana jioni.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa mahojiano ya makada hao watatu jana, Kinana alisema shughuli ya kuwahoji wengine itaendelea leo.

“Kazi haijakwisha, kesho (leo) tunaendelea.”

Waliyosema baada ya kuhojiwa

Akiwa amevalia mavazi rasmi ya CCM, Lowassa alihojiwa kwa takriban saa moja na nusu kwani aliingia katika kikao hicho saa 4:56 asubuhi na kutoka saa 6:40 mchana akiwa ametumia takriban saa moja na nusu na alitoka akiwa mwenye furaha.

Alipoulizwa kuhusu mahojiano hayo Lowassa: “Mazungumzo yalikwenda vizuri. Yalikuwa na lengo la kujenga chama kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,” alisema Lowassa huku akitabasamu.

Muda mfupi baada ya Lowassa kutoka, Sumaye aliingia kuanzia saa 6:46 na kutoka saa 8:05.

Baada ya kutoka, Sumaye pia hakuwa tayari kuzungumzia kuhusu mahojiano hayo... “Tunawasubiri wakubwa watakavyotoa jawabu.” Alipoulizwa sababu za kutumia muda mwingi katika kikao hicho alisema: “Tulikuwa tunakunywa chai.”

http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Lowassa--Sumaye--Ngeleja-wajieleza-Kamati-ya-Mangula/-/1597296/2205862/-/obn6qn/-/index.html

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment