Wanabidii,
Naomba nami niseme kidogo, nitoe maoni yangu kuhusu sakata hili na maoni ya Dk. Kitila Mkumbo.
Nimekuwa namsoma Dk. Kitila Mkumbo katika mtandao huu na safu yake katika Raia Mwema. NImemjua Dk. Mkumbo akiwa bado mwanafunzi, kiongozi wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1998/9. Nilishawishika tangu wakati huo kuamini kuwa Kitila ni kijana mwenye uwezo mkuwa wa kufikiri na kujieleza. Sijabadili msimamo wangu katika hilo. Hata yeye analijua hilo.
Kwa hiyo, wengi wanaomjua au wanaomsoma Dk. Kitila wanaangukia katika kundi la mashabiki wa hoja zake, na mfumo wake wa kuziwasilisha. Naamini waathirika wa mfumo huu wapo wengi. Hata hapa nawaona.
Hata hivyo, katika siku za karibuni Dk. Kitila ninayemjua amebadilika sana. Tangu alipoingia matatani kuhusu waraka wake wa mabadiliko ndani ya Chadema, hoja zake zimekuwa na mwelekeo wa kishabiki zaidi ya kufikirisha. Ni hoja zenye kuwakilisha hisia zake zaidi badala ya uzito wa maoni mbadala.
Nitatumia makala yake haya ya sasa kujadili kidogo suala hili.
1. Anaposema Chadema si mbadala unaominika wa CCM, bila kutuletea mbadala mbadala anakuwa anafanya kazi moja tu - kuchanganya wasomaji. Na wanapogoma kuchanganywa ndipo wanapoamua kusema "ametumwa," "anafanya kazi ya watu" na kadhalika. Hakuna jambo lisilo na mbadala. Kama si Chadema, basi aseme ni nani mbadala wa CCM. Na aeleze ni lini Chadema imeacha kuwa mbadala wa CCM, maana siku zote - kabla hajafukuzwa uanachama Chadema - amekuwa akiamini hivyo. Kwa hiyo, hapa tunaona hisia. Uchungu. Chuki!
2. Anapaswa kusema kwa majina na takwimu ufisadi wa viongozi wa chama chake cha zamani. Maana kwa jinsi tunavyojua, huo ufisadi anaoutaja kwa hao asiowataka upo pia kwa wale anaowashabikia tena kwa viwango vya juu sana. Kwa hiyo, kama angekuwa anachukia ufisadi kweli kweli, kuna watu asingewashabikia kabisa, wala singesubiri afukuzwe Chadema ndipo aseme ufisadi wa waliomfukuza.
Sitaki kumtetea mtu hapa. Lakini nataka kusisitiza kwamba hakuna popote ambapo Dk. Kitila amewahi kunukuliwa kwamba ndani ya vikao vya chama chake aliwahi kuibua hoja yoyote inayofanana na hii akakataliwa. Amekuwa kiongozi mkubwa ndani ya Chadema. Hakutaka kutumia kikao kusahihisha viongozi wenzake. Ameamua kutumia mitandao nje ya mfumo wa chama kushambulia wenzake. Ndiyo maana wakasema ni "msaliti."
Alipaswa kuyasema yale yaliyoandikwa kwenye waraka mbele yao akiwakazia macho kama msomi. wakubali, wakatae. Lakini kusubiti waraka wao ukamatwe halafu ndipo wajifanye mashujaa, ni dalili kwamba hawakuwa na nia ya kusaidia chama chao, bali kukiangusha kwa malengo wanayojua wao, wakitumia udhaifu fulani fulani wa ndani wanaoujua. Anachofanya hapa ni character assassination ambayo vile vile haitamjenga yeye binafsi wala kumrejeshea hadi aliyokuwa nayo.
3. Chadema hawapendi kukosolewa? Tumewakosoa sana. Kama kiongozi, aliapaswa kujua kuwa amepewa fursa adhimu ya kuwakosoa ndani ya vikao au katika mazingira yanayofanana na hadhi yake, nafasi yake na ya hao anaowakosoa. Kuwashambulia hadharani au kuwachimbachimba kisirisiri kama alivyofanya na waraka wake si njia mwafaka inayoweza kukubaliwa na chama chochote, au tasisi yoyote yenye uongozi.
Kama angetoa waraka huo kwenye kikao, akafanya uchambuzi yakinifu wa nguvu, udhaifu, fursa na vikwazo vya Chadema mbele ya wajumbe wake, akawaeleza ukweli anaoujua yeye wakaukataa, na bado wakamchukulia hatua, wengi tungekuwa nyuma yake. Kama msomi fursa ya kuwa miongoni mwa viongozi wa Chadema, tena katika Kamati Kuu, ndiyo ilikuwa nguvu yake ya kutumia kurekebisha kasoro anazoziona. Hakuitumia.
Au kama waraka huo ungeandikwa na mtu ambaye si kiongozi, hana fursa yoyote ya kukutana na viongozi wa chama kuwaeleza yaliyo moyoni mwake, awe mwanachama au la, tungeelewa kwamba alikuwa na nia njema, maana ndiyo fursa iliyokuwa karibu naye. Dk. Kitila na wenzake walikuwa na fursa ya kukutana na viongozi nje na ndani ya vikao. Lakini busara ziliwaongoza kuwa uwanja mwafaka wa kuikosoa Chadema ni katika mitandao ya kijamii.
Kwa kuwa watu hawa wameenda shule, tena zionazoeleweka; kwa kuwa wana uwezo mzuri tu wa kuelewa na kuchambua masuala mengi katika jamii; binafsi nashindwa kuelewa kwamba walishindwa kuelewa kwamba mtandao wa kijamii haukuwa uwanja mwafaka wa "kushauri" chama chao.
Kila mmoja wetu ana nguo ya ndani. Anajua anakoifulia na anakoianika. Kama demokrasia ni kufua nguo za ndani hadharani na kuzianika hadharani, hilo litakuwa ni somo jipya kwa baadhi yetu. Na kwa maana hiyo hatutakuwa na sababu ya kuwa na viongozi na vikao. Tuache kila mmoja asemee anapotaka!
Na katika mazingira haya, si vigumu wenzako kukuona kama umetumwa, ni pandikizi au msaliti. Popote penye uongozi suala hili lingechukuliwa hatua. Nadhani wenzetu hawakuamini jambo lao lingegunduliwa au kama baada ya kugunduliwa wangechukuliwa hatua.
Na kwa hulka hii wanayoonyesha hapa ni kwamba kama wao ndio wangekuwa viongozi wanaoshutumiwa na viongozi wenzao kwa staili hii wangekua wakali zaidi. Maana kama wamekuwa wakali kutetea kosa lao, ingekuwaje kama wangekuwa wanatetea hadhi ya chama na vikao vya chama wanachoongoza?
4. Nahitaji muda kuelimishwa kuhusu mpasuko wanaozungumzia. Ni hivi, kila mtu ana rafiki, ndugu, mashabiki. Dk. Kitila, Zitto na wenzao wana watu hao. Lakini ushabiki huu hauitwi mpasuko wa chama. Sana sana ni msukosuko.
Mpasuko unatokea pale taasisi inapogawanyika katika makundi makubwa mawili au matatu, kama ilivyokuwa kwa NCCR-Mageuzi. Mwenyekiti huku, katibu kule. Ofisi moja huku, nyingine kule. Lakini hasira na hamaniko la watu haliwi mpasuko. Kama kamati kuu ingekatika vipande vipande, kimoja kikiunga mkono uamuzi kingine kikikataa, huo ungekuwa mpasuko. Lakini wajumbe kadhaa kuunga mkono hoja na wengine wakapinga, halafu baadaye ukafanywa uamuzi wa kikao, katika misingi ya uwajibikaji wa pamoja, ni suala la kawaida, na uamuzi ukishafanywa ni wa kikao, ni wa taasisi. Hata wale waliokuwa hawautaki hulazimika kuukubali. Hakuna uamuzi uliowahi kukubaliwa na watu wote kwa asilimia 100.
Nadhani hii dhana ya mpasuko inakuzwa na wale wale waliokuwa wamedhamiria kupasua chama katika makundi mawili kwa nia ya kutengeneza chama mbadala. Yalitokea CUF na NCCR-Mageuzi mwaka juzi na mwaka jana. Haukuwa mpasuko bali msukosuko uliotokana na sakata husika. Baadaye chama kinakuwa kimoja mnaendelea na safari.
Wasioridhika kabisa hawalazimiki kuendelea kudumu katika taasisi isiyowaamini, na ambayo wao hawaiamini. Badala ya kulaani yaliyopita, huku wakijua kuwa hawana fursa ya kuaminika, kurejeshwa na kuheshimika kama zamani, ni bora kama bado wanataka siasa, waunde hicho kinachoitwa chama mbadala wakilee, wakikuze na waonyeshe wenzao umahiri wa kujenga chama mbadala.
Siasa za mezani na siasa za uwanjani ni vitu viwili tofauti. Chadema kimejengwa na makundi mengi ya watu. Wengine hata hawakumbukwi wala hawajulikani. Mnazungumzia mchango mliotoa? Wapo walioasisi chama; wapo waliofilisika kwa sababu ya Chadema; wapo walioachika kwa sababu ya Chadema; wapo waliopata vilema kwa ajili ya Chadema; wapo waliofukuzwa shule kwa ajili ya Chadema; wapo waliopoteza kazi kwa ajili ya Chadema; wapo waliokufa kwa ajili ya Chadema.
Botra nyie mmepata hata fursa ya kuwa viongozi. Wapo waliopitia katika magumu mengi hayo na hawatapata hata fursa ya kuwa wajumbe wa nyumba kumi; na bado wanakipenda chama chao. Kila mtu ana mchango wake. Ni bora utambuliwe. Zitto na Kitila wamefanya yao. Lakini mchango wa mtu si tiketi wala kisingizio cha kuwageuka wenzako.
Yuda Iskarioti alikuwa mtunza hazina wa wafuasi wa Yesu. Alipomgeuka bosi wake akamuuza kwa vipande 30 vya fedha ameitwa msaliti hata leo. Hakuna anayekumbuka mchango wake wa miaka yote aliyoshikilia mfuko.Hata angeibuka mtaani leo, angeitwa Yuda Iskarioti Msaliti. Ndiyo anuani aliyochagua.
Na akithubutu kushambuliwa Wakristo au mitume wenzake walioshikamana na Yesu, anajua majibu atakayopata kutoka kwao. Ndiyo haki yake.
Ni kweli, inawezekana usaliti wake umesababisha matokeo mengine mazuri katika mfumo husika, lakini hiyo ndiyo anuani yake - msaliti. Tayari yupo nje ya mfumo. Na kila anachosema kinatafsiriwa kulingana na mahali alipo na hadhi aliyo nayo sasa, si ile ya zamani.
Kwa hiyo, Dk. Kitila na wenzake wanapaswa kuyajua haya. Naamini wanayajua kwa sababu wameenda shule.

Ansbert Ngurumo
Managing Editor
Managing Editor
Free Media
P.O. Box 15261
P.O. Box 15261
Dar es Salaam
Tanzania
Mobile +255 767 172 665
Tanzania
Mobile +255 767 172 665
www.freemedia.co.tz
On Wednesday, February 12, 2014 3:24 PM, Felix Mwakyembe <fkyembe@gmail.com> wrote:
Hiyo filamu haiishi tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu, heee tumeshachoka nayo!!
2014-02-12 16:12 GMT+05:30 Vincent Mhangwa <vmhangwa@gmail.com>:
Hii ni hadith ya 'Sizitaki mbichi hizi'. Ukweli ni kwanba Dr. KITILA ameumia sana kuvuliwa uanachama. Makala zoote hizi nikutaka kuonesha kuwa CDM hakikubaliki.Yawezekana labda. Sasa suluhisho nini? Ni Kitila na wengine kuunda chama mbadala? Makala hii iko kwaajili ya kukikashifu CDM. Labda inajibu kile mwandishi amekisema kuwa CDM wametumia muda mwingi kumkashifu Zitto.Itachukua muda mrefu sana kubaini na kuwaondoa Wahaini ndani ya vyama vya siasa. Baadhi ya wanachama ni mapandikizi tu wa CCM ndiyo maana hawachelewi kusema "bora tuendelee na CCM' sawa na wale wanachuo waliomwambia Mwl JKN kuwa 'Bora Mkolon',Kwa hali ilivyo sasa makala zoote za Dr.Kitila zitaonekana ni chuki binafsi tu.
Vin--
Hana jipya na kama alikuwa anayajua haya asingepiga magoti kuomba msamaha. Asilete hsdithi ya sungura SIZITAKI MBICHI HIZI!--
From: Chadema Tanga <mabadilikochadema@gmail.com>;
To: <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: [wanabidii] CCM inaimarika, CHADEMA inasinyaa, CUF inakufa
Sent: Wed, Feb 12, 2014 10:05:48 AM
--By Dr Kitila MkumboKatika Makala Alioipost Jana Yenye Kichwa cha Habari'CCM is Stabilising, Chadema is Shrinking and CUF is Disappearing, Dr Kitila Mkumbo (Hon and Senior Lecture UDSM) Amesema Licha ya Chadema Kukubalika sana Mitaani na Kuwa na Mashabiki wengi LAKINI Chadema Haipati Kura za Kutosha Katika Chaguzi Kwa Sababu Kuu Nne:1. Chadema Imeonekana Sio Mbadala Sahihi wa CCM (Chadema is not Credible Alternative of CCM).Licha ya Kwamba Chadema Imefanikiwa Kuweka wazi MABAYA ya CCM kwa Watanzania Lakini Imeshindwa Kuwashawishi Watu ya Kwamba wao ni Mbadala wa CCM.Dr Kitila Akaenda Mbali na Kusema ni Heri Kutawaliwa na Wakoloni Weusi (CCM) Kuliko Wakoloni WEKUNDU (Chadema) Maana hawa ni Zaidi ya Kudandia Meli ya Kigiriki.2. Viongozi wa Chadema ni MAFISADI,Waroho wa Pesa na Viongozi Wenye Njaa Kali Kuliko Viongoozi wa CCM.Dr Kitila Amesema Viongozi wa Chadema Wanapenda Sana Posho Kuliko Viongozi wa CCM,Wanapenda Kutembelea Magari ya Kifahari sana Kuliko Viongozi wa CCM, Wanapenda Sana Safari za nje ya Nchi Ndio Maana Kila Siku Utasikia Freeman Mbowe na Mke wake Wameenda Kutalii Marekan,Dubai..kwa Pesa za Serikali.Kwa sababu hizo imekuwa ngumu kutofautisha Viongozi wa Chadema na wa CCM…3. Chadema Hawataki KUKOSOLEWA na wala hawataki KUJILEKEBISHA:Dr Kitila Amesema,Ukiikosoa Chadema Hata Kama Unachokisema ni Kweli,Hawachelewi Kukuita wew ni MSALITI,Pandikizi la CCM,Umetumwa……na Mambo mengine ya Kiuchonganishi ili Wakuchafue Kisiasa.Hii ni Hatari sana kwa Chama Kichanga chenye Dhamila ya Kushika Dolla4. Mpasuko ndani ya Chadema:Dr Kitila Anasema,Viongozi wa Chadema Wametumia Muda mwingi wa kampeni kumchafua Zitto Kabwe na sio kuwanadi wagombea wao.Dr Kitila Amesema,Kitendo cha Chadema Kumtangaza Zitto Kabwe kama Muhaini wa Chadema na ili Hali wananchi wanajua Mchango wa Zitto katika mafanikio ya Chadema,Wananchi wamepoteza Imani kabisa na Chadema na Hawakitaki tena.Dr Kitila Ameongezea kwamba:Ni Bora Tuendelee Kutawaliwa na CCM Ambao Wanang'ata na Kupuliza Kuliko Hawa Viongozi wa Chadema Ambao wananjaa ya Kufa Mnyama.Hawa Wanaweza Kuiba Mpaka Tukaingia kwenye Vita ya Wenyewe kwa Wenyewe.Dr Kitila Amemalizia kwa Kusem'Chama cha Upinzani Imara Bado Hakijazaliwa (A credible and Serious Opposition might be in the Offing) Hivyo Watanzania tuendelee kuwa na Subira na Vijana Tuache Kushabikia Chadema kwani Hakuna Chochote cha Ujenzi wa Taifa ndani ya Chadema Zaidi ya UOZO na WIZI....
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:
Post a Comment