Thursday, 13 February 2014

Re: [wanabidii] CCM inaimarika, CHADEMA inasinyaa, CUF inakufa

Ndugu Ngurumo,

Nashukuru sana kwa maoni yako . Mimi binafsi ni muumini wa kutofautiana kimawazo katika msingi wa hoja. Siogopi hata kidogo mtu kupinga hoja zangu madamu tu anafanya hivyo kwa hoja. Hivyo naheshimu maoni yako pamoja na kwamba s ikubaliani nawe.

Nadhani utakuwa hujasoma makala zangu zote za hivi karibuni na hasa ya juzi iliyochambua matokeo ya udiwani. Nasema hivi kwa sababu nimeogopa sana unaposema najenga hoja zangu kwa hisia bila ushahidi wa takwimu. Hapana. Soma makala zangu vizuri. Mimi ni muumini wa evidence based writing na nimejitahidi sana katika makala zangu kufanya hivyo.

Makala yako ina maoni mengi, ya msingi na mengine siyo ya msingi sana kama hilo la kusema kwamba ninaandika ninavyoandika sasa hivi kwa sababu nimetoka (nimefukuzwa) CHADEMA. Hii siyo hoja ya msingi kwa sababu hata wewe unajua ukweli kwamba mimi siungi au kukosoa jambo kwa minajili ya uchama, bila kujalai mimi ni wamachama wa husika au la. Sijaanza kuikosoa CHADEMA leo. Nilliikosoa CHADEMA nilipokuwa mwanachama ndani na nje ya vikao. Tofauti pekee. Nitakukumbusha matukio machache.

i) Tarehe 20 Nov 2013 niliandika makala iliyochapishwa katika Gazeti la Raia Mwema nikijadili umuhimu wa kutokuwakatisha tamaa wanaofanya vizuri katika jamii yetu. Katika makala haya, pamoja na mambo mengine, nilikosoa tabia ya viongozi wa CHADEMA ya kumzodoa mwenzao Zitto kwa kukataa posho. Nikaeleza waziwazi kwamba Zitto anapigwa vita ndani na nje ya chama kwenye mambo ya posho. Kwenye kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 21 Nov 2013 Mhe Lema alinilalamikia kwamba kwa nini nawasema viongozi magazetini. Nikajibu kwamba mimi ninaandika kama mtu huru na kama mwanataaluma na ninapotoa mawazo yangu katika umma siangalia mambo ya vyama. Nitatoa maoni yangu kadri fikra zangu na evidence niliyo nayo zinavyonielekeza. Kwa kifupi, kama alivyowahi kusema Steve Biko, 'I write what I like'.

ii) Kwenye matokeo ya udiwani wa mwaka 2012 ambapo CHADEMA ilipata viti 5 kati ya viti 29 vilivyokuwa vinagombaniwa niliandika nikasema CHADEMA inakuwa lakini kwa kasi ndogo. Nikaeleza kwamba kasi ya ukuaji wa chama hiki ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa hamasa na mapenzi kwa chama yaliyopo mitaani. Nikajenga hoja kwamba ni muhimu kikajitathimini kwa nini hakipata kura sawasawa na aina ya hamasa iliyopo. Nikaeleza kwamba kwa kiwango hiki cha ukuaji, kinaweza kuongeza idadi ya madiwani na wabunge, lakini hakitaweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana ya kushika dola. Jambo hili nililieleza pia ndani ya Kamati Kuu lakini kwa ukali zaidi. Wenzangu hawakufurahishwa na wakasema kwamba mimi sielewi mambo ya field. Nikakubali yakaisha.

iii) Mwaka jana huohuo niliwapinga viongozi wangu wa chama ndani na nje ya vikao kuhusu kumuunga mkono Mbatia kwamba nchi yetu haina mtaala wa elimu. Niliwaeleza viongozi wangu kitaaluma jambo hili si kweli kwa sababu nchi haiwezi ikatoa elimu bila mtaala, na kwamba mtaala sio lazima uwe kwenye document moja inayoitwa mtaala. Niliandika hadi makala. Niliongea kwa simu na kiongozi wa chama akiwa Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge. Wapo walionielewa na wengine hawakunielewa.

Kwa hiyo ndugu Ngurumo unaposema kwamba nilikuwa sikosoi kabla sijatoka CHADEMA unanionea au umeamua tu kujiridhisha juu ya hoja yako.

Unasema kwamba kusema CHADEMA si mbadala bila kuonyesha mbadala ni kuwachanganya wasomaji? Kwamba nasema hivi kwa sababu ya uchungu, hasira na chuki. Yes, nina uchungu na hasira, lakini sina chuki hata kidogo. Nina uchungu na hasira kwa sababu chama ambacho nilikitegemea kijenge taswira mpya ya siasa katika nchi hii kimeshindwa. Kinafanya mambo yale yale ambayo CCM wameyafanya kwa miaka chungu nzima. Nitaeleza kidogo hili.

Vyama vingi vilipoanza, CCM walipanick sana wakawa wanawatukana sana wapinzani. Wakawapa kila aina ya majina: mbwa, wanafiki, wasaliti, n.k., kisa wanatofautiana na wao kimsimamo. Lakini leo hii baada ya upinzani (soma CHADEMA) kukua na kujipatia wafuasi nao wanaanza kufanya mambo hayohayo ya kijinga waliyofanya CCM miaka ya tisini: kukebehi, kukejeli, kuwapaka matope na kuwaita wasaliti watu wanaotofautiana nao kimwazo na misimamo. Wapinzani wamejikuta wanauvaa uCCM bila wao kujua.

Sura ya chama inajengwa katika msingi wa hoja na uadilifu wa viongozi. Mambo yote haya hayapo katika upinzani wetu. Viongozi wetu nao wanapenda matumizi ya kutanua huku wakikandia serikali katika matumizi mabaya. Viongozi wetu wanabariki na kupokea maposho ya ajabuajabu bungeni huku wafanyakazi wengine katika nchi hii wakiteseka na viujira vidogo na wakijua msingi mojawapo wa chama ni usawa. Viongozi wanatukana na kukandia mashangingi ya serikali lakini wao wenyewe wananunua hayohayo kwa pesa za uma walizokopeshwa bila riba, na wengine wanachukua mashangingi ya serikali na kutembea nayo barabarani kwa madaha. Sasa huu si ndio uCCM wenyewe au? Unataka CHADEMA ionekana tofauti kwa kuuvaa uCCM?

Tukisema mnasema tuna hasira na uchungu. Ndio tuna uchungu kwa sababu chama hiki tulichokitegemea sana kimeuvaa uCCM na haiwezekani kikaaminika na kuchagulika kwa kuendeleza utamaduni wa uCCM. Ndio maana tunahitaji mbadala. Kwamba kwa sasa hivi hatuna mbadala haimanisha tusitamani na kutafuta mbadala. Tukishakujenga hoja ya uhitaji watu wanaojua namna ya kuanzisha mbadala wataanzisha. Kazi yangu ni kutoa mchango tu na wapo wengine nao watatoa mchango wao.

Mwisho, unaandika kana kwamba maoni yako ndiyo ukweli kiasi cha kusema kwamba sisi tuliyoenda shule tunapaswa kuyajua haya unayoyaandika, ebo kwani maoni yako ndiyo yamekuwa 2+2 ndugu yangu? Maoni yako ni maoni yako kama ambavyo ya kwangu ni maoni yangu, sio sheria. Hatuna uwezo wa kulazimisha watu wakubaliane na maoni yetu. Tunachofanya ni ushawishi tu wa hoja. Wapo watakaoshawishika na wapo ambao hawatashawishika kwa sababu zao: ama kwa kuona au kutoona uzito wa hoja au kwa kuwa tu wanampenda au hawampenda mwandishi wa hoja husika. Hiyo ndiyo tabia ya hadhira na huna namna ya kubadilisha hili. Tujifunze kuheshimu maoni ya wengine bila kulazimika kukubaliana nayo. Na tujifunze pia kutokulazimisha maoni yetu kuwa ndiyo ukweli!

Ahsante

Kitila

On Thursday, February 13, 2014 2:49:26 AM UTC-8, Method Francis Ngonge wrote:
Magere "kushinda uchaguzi" katika nchi kama hii si kipimo cha kukubalika wala kutokuwa fisadi. Fisadi anaweza kutumia fedha alizofisadi kurudi ikulu. Mfano anaweza kutumia fedha hizo na madaraka aliyonayo kuvivuruga vyama vingine ikiwemo kuhonga fedha taslimu, mali, pilau na tishirt kwa maskini walalahoi wasiojua hili wala lile na hata kununua shahada za kupiga kura na akaonekana ameshinda ili aingie ikulu akafanye biashara za kuwafisadi zaidi

2014-02-12 20:13 GMT+03:00 Godfrey Ngupula <ngu...@yahoo.co.uk>:
Trueeeee,this time anaonekama ni mbinafsi zaidi na hajui kwa kuisakama CHADEMA najiua yeye mwenyewe...ni bora angeenda kuanzisha cha ma mbadala kuiko hivyo anavyofanya...na pia, mtu makini huwezi kuandaa mapinduzi ya uhaini eti ZItto awe mwenyekiti wa chama,ni bora uhaini huo angekuwa yeye ndio mwenyekiti wa chama angeleweka..Ngupula

On Wednesday, 12 February 2014, 19:50, Jovi kamuntu <jbifa...@yahoo.com> wrote:
Ngurumo nadhani umefunga mjadala huo. Kitila na Zitto ni Wasaliti leo na hata kesho. Hilo ndilo jina linalowafaa. Kama wana ushawishi waanzishe mbadala wa sisiemu wapate wafuasi.
 
Jovin Bifabusha

DIRECTOR
KWFF LTD
P. O. Box 313
Skype: jovin.bifabusha
Karagwe, Tanzania
+255 784 709200

On Wednesday, February 12, 2014 6:19 PM, Ansbert Ngurumo <ansb...@yahoo.com> wrote:
Wanabidii,

Naomba nami niseme kidogo, nitoe maoni yangu kuhusu sakata hili na maoni ya Dk. Kitila Mkumbo.

Nimekuwa namsoma Dk. Kitila Mkumbo katika mtandao huu na safu yake katika Raia Mwema. NImemjua Dk. Mkumbo akiwa bado mwanafunzi, kiongozi wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1998/9. Nilishawishika tangu wakati huo kuamini kuwa Kitila ni kijana mwenye uwezo mkuwa wa kufikiri na kujieleza. Sijabadili msimamo wangu katika hilo. Hata yeye analijua hilo.

Kwa hiyo, wengi wanaomjua au wanaomsoma Dk. Kitila wanaangukia katika kundi la mashabiki wa hoja zake, na mfumo wake wa kuziwasilisha. Naamini waathirika wa mfumo huu wapo wengi. Hata hapa nawaona.

Hata hivyo, katika siku za karibuni Dk. Kitila ninayemjua amebadilika sana. Tangu alipoingia matatani kuhusu waraka wake wa mabadiliko ndani ya Chadema, hoja zake zimekuwa na mwelekeo wa kishabiki zaidi ya kufikirisha. Ni hoja zenye kuwakilisha hisia zake zaidi badala ya uzito wa maoni mbadala.

Nitatumia makala yake haya ya sasa kujadili kidogo suala hili.

1. Anaposema Chadema si mbadala unaominika wa CCM, bila kutuletea mbadala mbadala anakuwa anafanya kazi moja tu - kuchanganya wasomaji. Na wanapogoma kuchanganywa ndipo wanapoamua kusema "ametumwa," "anafanya kazi ya watu" na kadhalika. Hakuna jambo lisilo na mbadala. Kama si Chadema, basi aseme ni nani mbadala wa CCM. Na aeleze ni lini Chadema imeacha kuwa mbadala wa CCM, maana siku zote - kabla hajafukuzwa uanachama Chadema - amekuwa akiamini hivyo. Kwa hiyo, hapa tunaona hisia. Uchungu. Chuki! 

2. Anapaswa kusema kwa majina na takwimu ufisadi wa viongozi wa chama chake cha zamani. Maana kwa jinsi tunavyojua, huo ufisadi anaoutaja kwa hao asiowataka upo pia kwa wale anaowashabikia tena kwa viwango vya juu sana. Kwa hiyo, kama angekuwa anachukia ufisadi kweli kweli, kuna watu asingewashabikia kabisa, wala singesubiri afukuzwe Chadema ndipo aseme ufisadi wa waliomfukuza.

Sitaki kumtetea mtu hapa. Lakini nataka kusisitiza kwamba hakuna popote ambapo Dk. Kitila amewahi kunukuliwa kwamba ndani ya vikao vya chama chake aliwahi kuibua hoja yoyote inayofanana na hii akakataliwa. Amekuwa kiongozi mkubwa ndani ya Chadema. Hakutaka kutumia kikao kusahihisha viongozi wenzake. Ameamua kutumia mitandao nje ya mfumo wa chama kushambulia wenzake. Ndiyo maana wakasema ni  "msaliti."

Alipaswa kuyasema yale yaliyoandikwa kwenye waraka mbele yao akiwakazia macho kama msomi. wakubali, wakatae. Lakini kusubiti waraka wao ukamatwe halafu ndipo wajifanye mashujaa, ni dalili kwamba hawakuwa na nia ya kusaidia chama chao, bali kukiangusha kwa malengo wanayojua wao, wakitumia udhaifu fulani fulani wa ndani wanaoujua. Anachofanya hapa ni character assassination ambayo vile vile haitamjenga yeye binafsi wala kumrejeshea hadi aliyokuwa nayo.

3. Chadema hawapendi kukosolewa? Tumewakosoa sana. Kama kiongozi, aliapaswa kujua kuwa amepewa fursa adhimu ya kuwakosoa ndani ya vikao au katika mazingira yanayofanana na hadhi yake, nafasi yake na ya hao anaowakosoa. Kuwashambulia hadharani au kuwachimbachimba kisirisiri kama alivyofanya na waraka wake si njia mwafaka inayoweza kukubaliwa na chama chochote, au tasisi yoyote yenye uongozi.

Kama angetoa waraka huo kwenye kikao, akafanya uchambuzi yakinifu wa nguvu, udhaifu, fursa na vikwazo vya Chadema mbele ya wajumbe wake, akawaeleza ukweli anaoujua yeye wakaukataa, na bado wakamchukulia hatua, wengi tungekuwa nyuma yake. Kama msomi fursa ya kuwa miongoni mwa viongozi wa Chadema, tena katika Kamati Kuu, ndiyo ilikuwa nguvu yake ya kutumia kurekebisha kasoro anazoziona. Hakuitumia.

Au kama waraka huo ungeandikwa na mtu ambaye si kiongozi, hana fursa yoyote ya kukutana na viongozi wa chama kuwaeleza yaliyo moyoni mwake, awe mwanachama au la, tungeelewa kwamba alikuwa na nia njema, maana ndiyo fursa iliyokuwa karibu naye. Dk. Kitila na wenzake walikuwa na fursa ya kukutana na viongozi nje na ndani ya vikao. Lakini busara ziliwaongoza kuwa uwanja mwafaka wa kuikosoa Chadema ni katika mitandao ya kijamii.

Kwa kuwa watu hawa wameenda shule, tena zionazoeleweka; kwa kuwa wana uwezo mzuri tu wa kuelewa na kuchambua masuala mengi katika jamii; binafsi nashindwa kuelewa kwamba walishindwa kuelewa kwamba mtandao wa kijamii haukuwa uwanja mwafaka wa "kushauri" chama chao.

Kila mmoja wetu ana nguo ya ndani. Anajua anakoifulia na anakoianika. Kama demokrasia ni kufua nguo za ndani hadharani na kuzianika hadharani, hilo litakuwa ni somo jipya kwa baadhi yetu. Na kwa maana hiyo hatutakuwa na sababu ya kuwa na viongozi na vikao. Tuache kila mmoja asemee anapotaka!

Na katika mazingira haya, si vigumu wenzako kukuona kama umetumwa, ni pandikizi au msaliti. Popote penye uongozi suala hili lingechukuliwa hatua. Nadhani wenzetu hawakuamini jambo lao lingegunduliwa au kama baada ya kugunduliwa wangechukuliwa hatua.

Na kwa hulka hii wanayoonyesha hapa ni kwamba kama wao ndio wangekuwa viongozi wanaoshutumiwa na viongozi wenzao kwa staili hii wangekua wakali zaidi. Maana kama wamekuwa wakali kutetea kosa lao, ingekuwaje kama wangekuwa wanatetea hadhi ya chama na vikao vya chama wanachoongoza?

4. Nahitaji muda kuelimishwa kuhusu mpasuko wanaozungumzia. Ni hivi, kila mtu ana rafiki, ndugu, mashabiki. Dk. Kitila, Zitto na wenzao wana watu hao. Lakini ushabiki huu hauitwi mpasuko wa chama. Sana sana ni msukosuko.

Mpasuko unatokea pale taasisi inapogawanyika katika makundi makubwa mawili au matatu, kama ilivyokuwa kwa NCCR-Mageuzi. Mwenyekiti huku, katibu kule. Ofisi moja huku, nyingine kule. Lakini hasira na hamaniko la watu haliwi mpasuko. Kama kamati kuu ingekatika vipande vipande, kimoja kikiunga mkono uamuzi kingine kikikataa, huo ungekuwa mpasuko. Lakini wajumbe kadhaa kuunga mkono hoja na wengine wakapinga, halafu baadaye ukafanywa uamuzi wa kikao, katika misingi ya uwajibikaji wa pamoja, ni suala la kawaida, na uamuzi ukishafanywa ni wa kikao, ni wa taasisi. Hata wale waliokuwa hawautaki hulazimika kuukubali. Hakuna uamuzi uliowahi kukubaliwa na watu wote kwa asilimia 100.

Nadhani hii dhana ya mpasuko inakuzwa na wale wale waliokuwa wamedhamiria kupasua chama katika makundi mawili kwa nia ya kutengeneza chama mbadala. Yalitokea CUF na NCCR-Mageuzi mwaka juzi na mwaka jana. Haukuwa mpasuko bali msukosuko uliotokana na sakata husika. Baadaye chama kinakuwa kimoja mnaendelea na safari.

Wasioridhika kabisa hawalazimiki kuendelea kudumu katika taasisi isiyowaamini, na ambayo wao hawaiamini. Badala ya kulaani yaliyopita, huku wakijua kuwa hawana fursa ya kuaminika, kurejeshwa na kuheshimika kama zamani, ni bora kama bado wanataka siasa, waunde hicho kinachoitwa chama mbadala wakilee, wakikuze na waonyeshe wenzao umahiri wa kujenga chama mbadala.

Siasa za mezani na siasa za uwanjani ni vitu viwili tofauti. Chadema kimejengwa na makundi mengi ya watu. Wengine hata hawakumbukwi wala hawajulikani. Mnazungumzia mchango mliotoa? Wapo walioasisi chama; wapo waliofilisika kwa sababu ya Chadema; wapo walioachika kwa sababu ya Chadema; wapo waliopata vilema kwa ajili ya Chadema; wapo waliofukuzwa shule kwa ajili ya Chadema; wapo waliopoteza kazi kwa ajili ya Chadema; wapo waliokufa kwa ajili ya Chadema.

Botra nyie mmepata hata fursa ya kuwa viongozi. Wapo waliopitia katika magumu mengi hayo na hawatapata hata fursa ya kuwa wajumbe wa nyumba kumi; na bado wanakipenda chama chao. Kila mtu ana mchango wake. Ni bora utambuliwe. Zitto na Kitila wamefanya yao. Lakini mchango wa mtu si tiketi wala kisingizio cha kuwageuka wenzako.

Yuda Iskarioti alikuwa mtunza hazina wa wafuasi wa Yesu. Alipomgeuka bosi wake akamuuza kwa vipande 30 vya fedha ameitwa msaliti hata leo. Hakuna anayekumbuka mchango wake wa miaka yote aliyoshikilia mfuko.Hata angeibuka mtaani leo, angeitwa Yuda Iskarioti Msaliti. Ndiyo anuani aliyochagua.

Na akithubutu kushambuliwa Wakristo au mitume wenzake walioshikamana na Yesu, anajua majibu atakayopata kutoka kwao. Ndiyo haki yake.

Ni kweli, inawezekana usaliti wake umesababisha matokeo mengine mazuri katika mfumo husika, lakini hiyo ndiyo anuani yake - msaliti. Tayari yupo nje ya mfumo. Na kila anachosema kinatafsiriwa kulingana na mahali alipo na hadhi aliyo nayo sasa, si ile ya zamani.

Kwa hiyo, Dk. Kitila na wenzake wanapaswa kuyajua haya. Naamini wanayajua kwa sababu wameenda shule.

Ansbert Ngurumo
Managing Editor
Free Media

P.O. Box 15261
Dar es Salaam
Tanzania

Mobile    +255 767 172 665

On Wednesday, February 12, 2014 3:24 PM, Felix Mwakyembe <fky...@gmail.com> wrote:
Hiyo filamu haiishi tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu, heee tumeshachoka nayo!!

2014-02-12 16:12 GMT+05:30 Vincent Mhangwa <vmhangwa@gmail.com>:
Hii ni hadith ya 'Sizitaki mbichi hizi'. Ukweli ni kwanba Dr. KITILA ameumia sana kuvuliwa uanachama.  Makala zoote hizi nikutaka kuonesha kuwa CDM hakikubaliki.
Yawezekana labda. Sasa suluhisho nini? Ni Kitila na wengine kuunda chama mbadala? Makala hii iko kwaajili ya kukikashifu CDM. Labda inajibu kile mwandishi amekisema kuwa CDM wametumia muda mwingi kumkashifu Zitto.
Itachukua muda mrefu sana kubaini na kuwaondoa Wahaini ndani ya vyama vya siasa. Baadhi ya wanachama ni mapandikizi tu wa CCM ndiyo maana hawachelewi kusema "bora tuendelee na CCM' sawa na wale wanachuo waliomwambia Mwl JKN kuwa 'Bora Mkolon',
Kwa hali ilivyo sasa makala zoote za Dr.Kitila zitaonekana ni chuki binafsi tu.
Vin
Hana jipya na kama alikuwa anayajua haya asingepiga magoti kuomba msamaha. Asilete hsdithi ya sungura SIZITAKI MBICHI HIZI!

From: Chadema Tanga <mabadilikochadema@gmail.com>;
To: <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: [wanabidii] CCM inaimarika, CHADEMA inasinyaa, CUF inakufa
Sent: Wed, Feb 12, 2014 10:05:48 AM

By Dr Kitila Mkumbo
Katika Makala Alioipost Jana Yenye Kichwa cha Habari'CCM is Stabilising, Chadema is Shrinking and CUF is Disappearing, Dr Kitila Mkumbo (Hon and Senior Lecture UDSM) Amesema Licha ya Chadema Kukubalika sana Mitaani na Kuwa na Mashabiki wengi LAKINI Chadema Haipati Kura za Kutosha Katika Chaguzi Kwa Sababu Kuu Nne:

1. Chadema Imeonekana Sio Mbadala Sahihi wa CCM (Chadema is not Credible Alternative of CCM).Licha ya Kwamba Chadema Imefanikiwa Kuweka wazi MABAYA ya CCM kwa Watanzania Lakini Imeshindwa Kuwashawishi Watu ya Kwamba wao ni Mbadala wa CCM.Dr Kitila Akaenda Mbali na Kusema ni Heri Kutawaliwa na Wakoloni Weusi (CCM) Kuliko Wakoloni WEKUNDU (Chadema) Maana hawa ni Zaidi ya Kudandia Meli ya Kigiriki.

2. Viongozi wa Chadema ni MAFISADI,Waroho wa Pesa na Viongozi Wenye Njaa Kali Kuliko Viongoozi wa CCM.Dr Kitila Amesema Viongozi wa Chadema Wanapenda Sana Posho Kuliko Viongozi wa CCM,Wanapenda Kutembelea Magari ya Kifahari sana Kuliko Viongozi wa CCM, Wanapenda Sana Safari za nje ya Nchi Ndio Maana Kila Siku Utasikia Freeman Mbowe na Mke wake Wameenda Kutalii Marekan,Dubai..kwa Pesa za Serikali.Kwa sababu hizo imekuwa ngumu kutofautisha Viongozi wa Chadema na wa CCM…

3. Chadema Hawataki KUKOSOLEWA na wala hawataki KUJILEKEBISHA:Dr Kitila Amesema,Ukiikosoa Chadema Hata Kama Unachokisema ni Kweli,Hawachelewi Kukuita wew ni MSALITI,Pandikizi la CCM,Umetumwa……na Mambo mengine ya Kiuchonganishi ili Wakuchafue Kisiasa.Hii ni Hatari sana kwa Chama Kichanga chenye Dhamila ya Kushika Dolla 

4. Mpasuko ndani ya Chadema:Dr Kitila Anasema,Viongozi wa Chadema Wametumia Muda mwingi wa kampeni kumchafua Zitto Kabwe na sio kuwanadi wagombea wao.Dr Kitila Amesema,Kitendo cha Chadema Kumtangaza Zitto Kabwe kama Muhaini wa Chadema na ili Hali wananchi wanajua Mchango wa Zitto katika mafanikio ya Chadema,Wananchi wamepoteza Imani kabisa na Chadema na Hawakitaki tena.

Dr Kitila Ameongezea kwamba:
Ni Bora Tuendelee Kutawaliwa na CCM Ambao Wanang'ata na Kupuliza Kuliko Hawa Viongozi wa Chadema Ambao wananjaa ya Kufa Mnyama.Hawa Wanaweza Kuiba Mpaka Tukaingia kwenye Vita ya Wenyewe kwa Wenyewe.
Dr Kitila Amemalizia kwa Kusem'Chama cha Upinzani Imara Bado Hakijazaliwa (A credible and Serious Opposition might be in the Offing) Hivyo Watanzania tuendelee kuwa na Subira na Vijana Tuache Kushabikia Chadema kwani Hakuna Chochote cha Ujenzi wa Taifa ndani ya Chadema Zaidi ya UOZO na WIZI....
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Send Emails to wana...@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com.

0 comments:

Post a Comment