Kama wasemavyo wengine, ni vizuri kuzuia email za namna hii. watu sijui kama wanaelewa kuwa, ikitokea vita au mauaji familia zao nazo zitahanja kama tuonavyo wenzetu Congo, Styria, Libya wanavyohangaika na kufukiwa na vifusi vya nyumba. Vilema vya maelfu ya wananchi Msumbiji, Angola, mauaji na vita vya kila wakati South Sudan, Kivu na yanayotokea Kenya kulipuriwa na waasi wa Somalia; Miji ya Somalia baadhi kuwa maghofu tupu nao huhangainga hadi kufa katika makontaina na kutupwa bongoland ni mfano tosha. Kama kupigana nchini kwao somalia ni kuzuri-mbona wanahanja kutorokea nchi za wenzao na kuleta usumbufu. Mnaanza kupigana kisiasa vyama mbali mbali, yanaingia mapigano ya koo mbali mbali (tunayo tarime hayaishi na vyama mbali mbali vipo huko havijafanikiwa kuyamaliza), jee hivi vya kuua polisi katika makazi yao itakuwaje wananchi wakianza kutia moto nyumba zao au kuwavizia na kuwaua? Vibaka wanasikiliza na ndio maana hata kukiwa na maandamano wanayatumia kuvunja magari ya watu na kuiba, kuingia madukani kupora na kupora wapita njia. Matokeo ya huko mbele ni chama kushindwa kutokana na raia kuona kina vurugu na watu wamepoteza mali waliyoitafuta maisha yao yote na kuamua bora Jini likujualo halikuli likakwisha yakavuka mengine sasa ya kuchukua madaraka kwa mtutu. tukijituma tulipo, kuzalisha mali, kutumia benki zilizopo na uwekezaji tukalima, kufuga kisasa karne hii ya climate change, tuuze value added products weell packaged ndani na nje ya nchi, tunaepuka kuona Siasa ni kimbilio la mafao ya kipato, kupata jina na utukufu. Inakuwaje wakati watu wanatakiwa kuhesabiwa kuwe na maandamano na mihadhara? Hebu tuangalie utata tunaouingiza na mpaka kuleta misuguano na vyombo vya dola. Zima moto madhubuti za kufika haraka kila kona ya mji, miji na vijiji hatuna. Mbanano wa nyumba ni mkubwa. Ikichomwa moja, moto hauna ubaguzi au macho kusema hii ni ya CCM au Chadema, CUF niiache. Moto utalamba mji, mashule, bank, mabanda ya mifugo, huko vijijini utawasha mbuga za hifadhi na wanyana na misitu tegemezi ya maji etc-utazagaa. Hii ndio wanayotaka washabiki wa kuchoma makazi ya polisi uraiani? tunaona miji na misitu iwakavyo ulaya. Wana helikopta za zima moto lakini unawashinda unakula ma hekta na majumba, magari etc. Jee sisi wazima moto kwa kutumia ndoo kwa kupanda ngazi, mti na kipaa jirani yake? Mungu awape busara waonao moto na vita ni mchezo wa mdako. Risasi na Petroli ni vya kuchezea? petroli imeua sana nchi hii kwa uwekaji hovyo majumbani. Ni ajabu kwa mtanzania kushabikia mauaji ya nduguze.
From: Charles Misango <misangocharles@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, 29 August 2012, 12:29
Subject: Re: [wanabidii] RE: CHOMENI MAKAZI YA POLISI URAIANI
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, 29 August 2012, 12:29
Subject: Re: [wanabidii] RE: CHOMENI MAKAZI YA POLISI URAIANI
hata mimi nimeshituka na kusikitishwa na maoni ya ajabu ya kuhamasisha watu kuvunja amani. Nashawishika kuamini kuwa mtoa hoja, hakuwa anatumia akili zake za kawaida! --- On Tue, 8/28/12, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
|
0 comments:
Post a Comment