Friday, 31 August 2012

Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA

Ahsante sana Mobhare, kama kawaida yako, UMEFUNGA KAZI, sina cha kuongeza! Umeyasema mengi yaliyoko moyoni mwangu. Tutake tusitake, Kiingereza ni muhimu! LKK

Sent from my iPad

On 31 Ago 2012, at 9:37 alasiri, Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com> wrote:


Wachangiaji,

Kwa kuwa mimi ndiye niliyekuja na hoja kwamba Kiingereza kibovu na uandishi mbovu wa ile barua ya serikali ya mtaa wa Oysterbay ni kielelezo cha jinsi elimu yetu ilivyoanguka, basi naomba niseme mengine machache kwa mara ya pili ili kuondoa mkoroganyo wa mambo uliojitokeza ambao nao ninaamini pia ni zao la kuanguka kwa elimu yetu.

Narudia tena: KIINGEREZA NI TATIZO TANZANIA KWA SABABU ELIMU YETU IMEKUFA.

Kwa Nini?

Kwa sababu Kiingereza si lugha ya kigeni kama wachangiaji wengine wanavyotaka kujiaminisha bali Kiingereza ni lugha rasmi ya Tanzania – official language – ambayo hutumika kwenye shughuli za kiserikali, kibiashara, kimahakama, kitabibu, kijeshi, n.k. Kiingereza ni lugha ya kufundishia mashuleni kuanzia sekondari hadi vyuo vikuu na vyuo vyote hapo katikati. Kozi za juu jeshini mwetu hivi sasa nazo zinafanywa kwa Kiingereza. Aidha, hukumu za mahakama za juu huandikwa kwa Kiingereza na masuala yote ya kimataifa Tanzania inaposhiriki hutumia Kiingereza. Kwa hiyo, tofauti na alivyosema dada yangu mmoja, Kiingereza si lugha ya kigeni Tanzania kwa maana ya neno halisi "kigeni" bali ni lugha ya nchi ama watu wa nje lakini yenye jukumu kubwa katika taifa letu. Ndiyo maana gazeti la serikali hutumia Kiingereza, miswada ya sheria huja kwa Kiingereza, n.k. Kubishia hili nadhani ni suala la kutokujua tu – kwa lugha ya kiungwana tunaitaje?

Nini Maana Yake?

Ni mzaha kukikwepa Kiingereza ama kudai kuwa kutokukijua vema si tatizo au eti mtu akisema kwamba Kiingereza kibovu ni matokeo ya kuanguka kwa elimu basi labda ana kasumba. Kiingereza ni lugha yetu ya pili baada ya Kiswahili ambacho kina hadhi mbili: Lugha Rasmi (official) na Lugha ya Taifa. Kiingereza si lugha ya taifa lakini ni rasmi na kama hamjui basi poleni sana. Kwa hiyo, Mtanzania anayefanya kazi za kiserikali, ama kibiashara, n.k. anapaswa kukijua Kiingereza na kama hakijui basi lazima kutakuwa na sababu. Sababu hiyo ni kufa kwa elimu kwa kuwa Kiingereza ni somo kuanzia darasa la tatu hadi darasa la saba; kisha kinakuwa lugha ya kufundishia kuanzia sekondari hadi mwisho wa elimu na huko sekondari ni somo hadi kidato cha nne. Kumbukeni kuwa hatujifunzi mathalani Kichina ama Kifaransa kwa namna hii ambazo ndizo lugha za kigeni kwa maana halisi hapa Tanzania. Kwa kuwa hatuna walimu wazuri wa Kiingereza, na mfumo mzima wa elimu umekufa, ndiyo maana sisi Watanzania hatujui lugha hii ya wakoloni ambayo ni ya pili nchini mwetu. Kwa kifupi, Kiingereza nchini Tanzania kina hadhi kubwa kuliko lugha ya kabila lolote na sidhani kama mtu mwenye ufahamu wa kazi na hadhi za lugha anaweza kubishia jambo hili.

Kwa Nini Kiingereza Kibovu Kilaumiwe?

Kwa kuwa ni rahisi zaidi kumdaka mtu mwenye Kiingereza kibovu pale anapoingia kwenye mtego wa mawasiliano. Makosa madogo madogo si hoja sana lakini kuvurunda kuanzia juu hadi chini ni tatizo. Watanzania hufanya makosa kwenye Kiswahili pia lakini si kwa kiwango cha yaliyomo kwenye Kiingereza kwa kuwa Kiswahili ndiyo lugha inayotawala maisha yetu – lingua franca – mbali ya kuwa lugha ya taifa na lugha rasmi na lugha ya kujifunzia masomo shule za msingi. Makosa ya Kiswahili yanaongezeka siku hizi kwa kuwa elimu imekufa na kimsingi watu wa taifa hili hatujui kuandika hata pale lugha inapokuwa si tatizo kwa kuwa elimu yetu ni marehemu. Kiukweli, hatujui vitu vingi vinavyopatikana shuleni ila tu hatuna nafasi ya kupima kirahisi kama ilivyo kwenye Kiingereza.

Upo ukweli kwamba kuna tofauti kubwa kati ya enzi waliposoma wazee wetu na hivi leo kwenye ubora wa elimu na si lugha pekee; lakini pia nchi zingine zenye lugha ya Kiingereza na lugha nyingine yoyote zinatuzidi kwa kuwa elimu yao ni safi na wana walimu wazuri wa Kiingereza, mfano Morisi (Mauritius), Bara Hindi (India), Pakistan, Kenya, Afrika Kusini, Nigeria, n.k. Juu ya hapo, nchi ambazo hazikitumii Kiingereza katika jambo lolote, mathalani, nchi nyingi za Ulaya, watu wake wanajifunza Kiingereza mashuleni na wanatuzidi Watanzania mbali kabisa, mfano watu wa Skandinavia (anayebisha akatembelee balozi zao Jumatatu). Nchi zilizoamua kutumia lugha nyingi kama Laksimbaga ya Ulaya, Uswisi pia, watu wake wanatuzidi kwa Kiingereza. Hali kadhalika, visiwa vya Karibeani vinavyotumia lugha zaidi ya moja kikiwemo Kiingereza zinatuzidi mno, mfano Aruba. Kama hamjatembea au kufanya utafiti mdogo au niite upekuzi, basi msiwe wabishi.

Kwa hiyo, ni haki kupigia kelele hili tatizo la Kiingereza kuwa tatizo Tanzania, hata kama tutaamua kutumia Kiswahili hadi vyuo vikuu, bado hatutakuwa tumejibu suala hili; hata kama tutabisha, badi ukweli utabaki kuwa kuanguka kwa elimu yetu kunaathiri Kiingereza ambayo ni lugha ya pili Tanzania.

Kulilia kwamba kujua lugha ya kigeni si kipimo cha elimu ni njia ya kujitetea kama si kushindwa kuelewa mjadala ni nini hasa. Iwapo lugha ya kigeni ina hadhi kama kilivyo Kiingereza hapa Tanzania, na inafundishwa mashuleni, halafu watu hawaijui, basi ni hakika kuna tatizo.

Kufa kwa elimu yetu kunaua Kiswahili pia na uthibitisho ni mwingi mno; naomba mnaolalamikia hoja kwamba kufa kwa elimu kunachangia Kiingereza kuwa uozo siku nyinginge mseme kuwa kujua Kiswahili siyo kipimo cha ubora wa elimu. Kama lugha inakubalika nchini, inatumika, inafundishwa vema, kwa nini basi tusiijue? Tatizo ni nini kama siyo mfumo wa elimu?

Kama ni lazima nitaendelea tena na hoja hii, lakini narejea tena, suala la utetezi wa Kiswahili halina ukaribu wowote na hoja kwamba kuna uhusiano kati ya kufa kwa elimu na ubovu wa Kiingereza Tanzania. Liko wazi kabisa, ni kama ilivyo kwenye Hesabu ambapo zaidi ya 80% ya wanafunzi wa kidato cha IV wanafeli.

Matinyi.


 

Date: Fri, 31 Aug 2012 05:35:28 -0700
From: mutembei@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
To: wanabidii@googlegroups.com

Matinyi

Katika mtandao huu, kuna watu (ukitaka nitakutajia majina) huandika Kiswahili kibovu sana. Sana tu!
Nimekuwa nikikusanya uandishi wao, na namna wanavyoyawasilisha mawazo na hoja zao (kwa sababu za kitaaluma).
Sijasikia mtu akilalamika kuhusu uandishi wao.
Pamoja na yote uliyoyaeleza, ukweli unabaki pale pale kuhusu Kasumba.
Ni KASUMBA TU!
Mtu akiandika vibaya kiinglish, atachekwa, atasimangwa, ataonekanekana HAKUSOMA. Kwa ujumla ataonekana HANA ELIMU.
Mtu yule yule akibananga Kiswahili, sababu kibao zitatolewa, lakini miongoni mwa hizo hakuna zitakazohusiana na Elimu, Maarifa au Uelewa wa mambo kwa ujumla.

Ninadhani hatujitendei haki sisi wenyewe, ukiachilia mbali maarifa yetu.
Mtu akikosea, amekosea.
Ninaunga mkono yale yaliyosemwa kumhusu mwandishi wa ule ujumbe ambao alidhani anaandika Kiingereza.

Tunaomfahamu (toka enzi za Pan Africa) tunajua jinsi anavyojitahidi kupanga hoja zake kwa Kiswahili, kuongea na kushswishi; ndio maana BARUA YAKE (niliyoipata siku alipoitoa) NILIIWEKA KATIKA MBAO ZA MATANGAZO HAPA CHUONI NA KUHOJI:

Je ilikuwa ni lazima kuandika haya kwa kiinglish?

Aldin

 
Aldin K. Mutembei   (PhD)                         Aldin Mutembei (PhD)
Mkurugenzi                                                  Director
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili                  Institute of Kiswahili Studies
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam                   University of Dar es Salaam, TANZANIA
+255 222 410 757     [Ofisini]                     +255 222 410757 (Day time-Office)
+255 715 426 162      [Kiganjani]                +255 715 426 162  (Cell)
b-pepe: kaimutembei@gmail.com                Alternative e-mail: <kaimutembei@gmail.com>


From: Lutgard Kagaruki <lutgardk@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, August 31, 2012 11:53 AM
Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA

Nakumbuka miaka ile (47!!) nikiwa darasa la sita nilivyomwandikia Baba barua ya kiingereza; aliifurahia na kunipongeza sana. Mtoto wa darasa la saba inabidi aweze kuandika barua ya Kiingereza inayoeleweka. Jamani wacheni kutetea kitu cha wazi. Kama hajui, basi hafai kuwa kiongozi!!
 
Lutgard




From: Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com>
To: Wanabidii Mawazo <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, August 31, 2012 11:38 AM
Subject: RE: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA

Lakini tumejiuliza kwamba amesoma mpaka kidato gani huyu Bwana?
Inawezekana ni darasa la saba na nivyo barua hiyo inaendana na kiwango chake cha elimu!
 

Date: Fri, 31 Aug 2012 06:49:49 +0100
From: ekunyaranyara@yahoo.co.uk
Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
To: wanabidii@googlegroups.com

Matinyi,
Sina lolote la kusema kwenye hii barua ila inaumiza sana kwa lugha kama hii.
 
K.E.M.S.

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com
Sent: Thursday, 30 August 2012, 10:16
Subject: RE: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA

0 comments:

Post a Comment