Friday, 31 August 2012

Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA

Matinyi,
Umeileza vizuri hii. Mimi nakubaliana na wewe.
Kwa kusema ule ukweli sijawahi kuelewa, sio kwa kushindwa kujaribu, nimejitahidi sana kuelewa hoja za watu wanatetea mtu kasoma hadi chuo kikuu lakini hawezi kuandika na kuzungumza kiingereza, nimeshindwa kuelewa tatizo ni nini hasa. Hiyo mitihani alifanyaje?

Hapa sio kasumba, tunaangalia mtu alifanya hiyo mitihani? Wengine ni wale wamesoma masomo ya sanaa(sayansi ya jamii), uchumi, sayansi ya siasa nk

Sasa unajiuliza: tangu darasa la tatu hadi kidato cha 4/6 mtu anasoma masomo yote kwa kiingereza anaongeza miaka kuanzia 3 ya chuo kikuu atashindwaje kujua kiingereza? Wapo tunawajua na kuwasoma, tunafanya nao kazi.

Hapa mtu asije na kusema kuwa mtu anaweza soma miaka yote hiyo asijue hiyo lugha. Kawaida lugha ngeni mtu unajifunza ndani ya mwaka mmoja ukiwa makini.

Siri ya kujua lugha yoyote ni kuizungumza, kuiandika ili upate misamiati mipya.

Hayo yanawezekana kama tunasoma vitabu, huko ndio tunakuta sentensi, sarufi za kutusaidia kutumia kwa matumizi yetu ya baadae na kuongeza misamiati.

Wengi wetu hata magazeti yetu ya kiigereza hatusomi, hata kama yana kopi na kupesti habari za wenzao kutoka kwenye mitandao.Huu ndio ukweli, tuanze na hilo kwanza maana hata tukiamua kutumia kiswahili tatizo bado ni hilo, elimu yetu taabu sana!

Wengi wetu wanachukua Guardian na Daily News kama mtu anatafuta kazi sio kusoma.

Usiku mwema,
LR
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

-----Original Message-----
From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
Date: Fri, 31 Aug 2012 18:37:40
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: RE: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA

Wachangiaji,
Kwa kuwa mimi ndiye niliyekuja na hoja kwamba Kiingereza kibovu na uandishi mbovu wa ile barua ya serikali ya mtaa wa Oysterbay ni kielelezo cha jinsi elimu yetu ilivyoanguka, basi naomba niseme mengine machache kwa mara ya pili ili kuondoa mkoroganyo wa mambo uliojitokeza ambao nao ninaamini pia ni zao la kuanguka kwa elimu yetu.
Narudia tena: KIINGEREZA NI TATIZO TANZANIA KWA SABABU ELIMU YETU IMEKUFA.
Kwa Nini?
Kwa sababu Kiingereza si lugha ya kigeni kama wachangiaji wengine wanavyotaka kujiaminisha bali Kiingereza ni lugha rasmi ya Tanzania - official language - ambayo hutumika kwenye shughuli za kiserikali, kibiashara, kimahakama, kitabibu, kijeshi, n.k. Kiingereza ni lugha ya kufundishia mashuleni kuanzia sekondari hadi vyuo vikuu na vyuo vyote hapo katikati. Kozi za juu jeshini mwetu hivi sasa nazo zinafanywa kwa Kiingereza. Aidha, hukumu za mahakama za juu huandikwa kwa Kiingereza na masuala yote ya kimataifa Tanzania inaposhiriki hutumia Kiingereza. Kwa hiyo, tofauti na alivyosema dada yangu mmoja, Kiingereza si lugha ya kigeni Tanzania kwa maana ya neno halisi "kigeni" bali ni lugha ya nchi ama watu wa nje lakini yenye jukumu kubwa katika taifa letu. Ndiyo maana gazeti la serikali hutumia Kiingereza, miswada ya sheria huja kwa Kiingereza, n.k. Kubishia hili nadhani ni suala la kutokujua tu - kwa lugha ya kiungwana tunaitaje?
Nini Maana Yake?
Ni mzaha kukikwepa Kiingereza ama kudai kuwa kutokukijua vema si tatizo au eti mtu akisema kwamba Kiingereza kibovu ni matokeo ya kuanguka kwa elimu basi labda ana kasumba. Kiingereza ni lugha yetu ya pili baada ya Kiswahili ambacho kina hadhi mbili: Lugha Rasmi (official) na Lugha ya Taifa. Kiingereza si lugha ya taifa lakini ni rasmi na kama hamjui basi poleni sana. Kwa hiyo, Mtanzania anayefanya kazi za kiserikali, ama kibiashara, n.k. anapaswa kukijua Kiingereza na kama hakijui basi lazima kutakuwa na sababu. Sababu hiyo ni kufa kwa elimu kwa kuwa Kiingereza ni somo kuanzia darasa la tatu hadi darasa la saba; kisha kinakuwa lugha ya kufundishia kuanzia sekondari hadi mwisho wa elimu na huko sekondari ni somo hadi kidato cha nne. Kumbukeni kuwa hatujifunzi mathalani Kichina ama Kifaransa kwa namna hii ambazo ndizo lugha za kigeni kwa maana halisi hapa Tanzania. Kwa kuwa hatuna walimu wazuri wa Kiingereza, na mfumo mzima wa elimu umekufa, ndiyo maana sisi Watanzania hatujui lugha hii ya wakoloni ambayo ni ya pili nchini mwetu. Kwa kifupi, Kiingereza nchini Tanzania kina hadhi kubwa kuliko lugha ya kabila lolote na sidhani kama mtu mwenye ufahamu wa kazi na hadhi za lugha anaweza kubishia jambo hili.
Kwa Nini Kiingereza Kibovu Kilaumiwe?
Kwa kuwa ni rahisi zaidi kumdaka mtu mwenye Kiingereza kibovu pale anapoingia kwenye mtego wa mawasiliano. Makosa madogo madogo si hoja sana lakini kuvurunda kuanzia juu hadi chini ni tatizo. Watanzania hufanya makosa kwenye Kiswahili pia lakini si kwa kiwango cha yaliyomo kwenye Kiingereza kwa kuwa Kiswahili ndiyo lugha inayotawala maisha yetu - lingua franca - mbali ya kuwa lugha ya taifa na lugha rasmi na lugha ya kujifunzia masomo shule za msingi. Makosa ya Kiswahili yanaongezeka siku hizi kwa kuwa elimu imekufa na kimsingi watu wa taifa hili hatujui kuandika hata pale lugha inapokuwa si tatizo kwa kuwa elimu yetu ni marehemu. Kiukweli, hatujui vitu vingi vinavyopatikana shuleni ila tu hatuna nafasi ya kupima kirahisi kama ilivyo kwenye Kiingereza.
Upo ukweli kwamba kuna tofauti kubwa kati ya enzi waliposoma wazee wetu na hivi leo kwenye ubora wa elimu na si lugha pekee; lakini pia nchi zingine zenye lugha ya Kiingereza na lugha nyingine yoyote zinatuzidi kwa kuwa elimu yao ni safi na wana walimu wazuri wa Kiingereza, mfano Morisi (Mauritius), Bara Hindi (India), Pakistan, Kenya, Afrika Kusini, Nigeria, n.k. Juu ya hapo, nchi ambazo hazikitumii Kiingereza katika jambo lolote, mathalani, nchi nyingi za Ulaya, watu wake wanajifunza Kiingereza mashuleni na wanatuzidi Watanzania mbali kabisa, mfano watu wa Skandinavia (anayebisha akatembelee balozi zao Jumatatu). Nchi zilizoamua kutumia lugha nyingi kama Laksimbaga ya Ulaya, Uswisi pia, watu wake wanatuzidi kwa Kiingereza. Hali kadhalika, visiwa vya Karibeani vinavyotumia lugha zaidi ya moja kikiwemo Kiingereza zinatuzidi mno, mfano Aruba. Kama hamjatembea au kufanya utafiti mdogo au niite upekuzi, basi msiwe wabishi.
Kwa hiyo, ni haki kupigia kelele hili tatizo la Kiingereza kuwa tatizo Tanzania, hata kama tutaamua kutumia Kiswahili hadi vyuo vikuu, bado hatutakuwa tumejibu suala hili; hata kama tutabisha, badi ukweli utabaki kuwa kuanguka kwa elimu yetu kunaathiri Kiingereza ambayo ni lugha ya pili Tanzania.
Kulilia kwamba kujua lugha ya kigeni si kipimo cha elimu ni njia ya kujitetea kama si kushindwa kuelewa mjadala ni nini hasa. Iwapo lugha ya kigeni ina hadhi kama kilivyo Kiingereza hapa Tanzania, na inafundishwa mashuleni, halafu watu hawaijui, basi ni hakika kuna tatizo.
Kufa kwa elimu yetu kunaua Kiswahili pia na uthibitisho ni mwingi mno; naomba mnaolalamikia hoja kwamba kufa kwa elimu kunachangia Kiingereza kuwa uozo siku nyinginge mseme kuwa kujua Kiswahili siyo kipimo cha ubora wa elimu. Kama lugha inakubalika nchini, inatumika, inafundishwa vema, kwa nini basi tusiijue? Tatizo ni nini kama siyo mfumo wa elimu?
Kama ni lazima nitaendelea tena na hoja hii, lakini narejea tena, suala la utetezi wa Kiswahili halina ukaribu wowote na hoja kwamba kuna uhusiano kati ya kufa kwa elimu na ubovu wa Kiingereza Tanzania. Liko wazi kabisa, ni kama ilivyo kwenye Hesabu ambapo zaidi ya 80% ya wanafunzi wa kidato cha IV wanafeli.
Matinyi.
 
----------------
Date: Fri, 31 Aug 2012 05:35:28 -0700
From: mutembei@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
To: wanabidii@googlegroups.com

Matinyi

Katika mtandao huu, kuna watu (ukitaka nitakutajia majina) huandika Kiswahili kibovu sana. Sana tu!
Nimekuwa nikikusanya uandishi wao, na namna wanavyoyawasilisha mawazo na hoja zao (kwa sababu za kitaaluma).
Sijasikia mtu akilalamika kuhusu uandishi wao.
Pamoja na yote uliyoyaeleza, ukweli unabaki pale pale kuhusu Kasumba.
Ni KASUMBA TU!
Mtu akiandika vibaya kiinglish, atachekwa, atasimangwa, ataonekanekana HAKUSOMA. Kwa ujumla ataonekana HANA ELIMU.
Mtu yule yule akibananga Kiswahili, sababu kibao zitatolewa, lakini miongoni mwa hizo hakuna zitakazohusiana na Elimu, Maarifa au Uelewa wa mambo kwa ujumla.

Ninadhani hatujitendei haki sisi wenyewe, ukiachilia mbali maarifa yetu.
Mtu akikosea, amekosea.
Ninaunga mkono yale yaliyosemwa kumhusu mwandishi wa ule ujumbe ambao alidhani anaandika Kiingereza.

Tunaomfahamu (toka enzi za Pan Africa) tunajua jinsi anavyojitahidi kupanga hoja zake kwa Kiswahili, kuongea na kushswishi; ndio maana BARUA YAKE (niliyoipata siku alipoitoa) NILIIWEKA KATIKA MBAO ZA MATANGAZO HAPA CHUONI NA KUHOJI:

Je ilikuwa ni lazima kuandika haya kwa kiinglish?

Aldin

Aldin K. Mutembei   (PhD)                         Aldin Mutembei (PhD)
Mkurugenzi                                                  Director
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili                  Institute of Kiswahili Studies
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam                   University of Dar es Salaam, TANZANIA
+255 222 410 757     [Ofisini]                     +255 222 410757 (Day time-Office)
+255 715 426 162      [Kiganjani]                +255 715 426 162  (Cell)
b-pepe: kaimutembei@gmail.com                Alternative e-mail: <kaimutembei@gmail.com>

----------------
From: Lutgard Kagaruki <lutgardk@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, August 31, 2012 11:53 AM
Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA

Nakumbuka miaka ile (47!!) nikiwa darasa la sita nilivyomwandikia Baba barua ya kiingereza; aliifurahia na kunipongeza sana. Mtoto wa darasa la saba inabidi aweze kuandika barua ya Kiingereza inayoeleweka. Jamani wacheni kutetea kitu cha wazi. Kama hajui, basi hafai kuwa kiongozi!!

Lutgard

----------------
From: Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com>
To: Wanabidii Mawazo <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, August 31, 2012 11:38 AM
Subject: RE: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA

Lakini tumejiuliza kwamba amesoma mpaka kidato gani huyu Bwana?
Inawezekana ni darasa la saba na nivyo barua hiyo inaendana na kiwango chake cha elimu!
 
----------------
Date: Fri, 31 Aug 2012 06:49:49 +0100
From: ekunyaranyara@yahoo.co.uk
Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
To: wanabidii@googlegroups.com

Matinyi,
Sina lolote la kusema kwenye hii barua ila inaumiza sana kwa lugha kama hii.

K.E.M.S.

----------------
From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com
Sent: Thursday, 30 August 2012, 10:16
Subject: RE: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA

Dkt. Mutembei,
Kwanza nina ujumbe wa kukuandikia lakini sijapata nafasi na ni ujumbe mzuri tu wa kukushukuru.
Naomba nianze kwa kumtetea Chambi kwa kuwa yeye siye aliyetoa madai ya kuanguka kwa elimu kwenye huu mjadala bali ni mimi ndiye niliyefanya hivyo na kisha kumwomba anirushie hewani kwa kuwa Hotmail yangu ilikuwa na tatizo.
Ndiyo, mimi naiona hii barua kama tatizo la ELIMU kwanza na pengine pekee kabla ama hata bila suala la LUGHA ya Kiingereza. Kwa nini?
1. Barua hii haikufuata kanuni za uandishi barua ambalo ni suala la elimu.
2. Barua hii imeshindwa kunyoonesha na kuupanga ujumbe vema na hata kama angeandika kwa Kichaga bado angekosea tu. Ni elimu hapo.
3. Huyu bwana hajui hata jina rasmi la Tanzania kwa Kiingereza ambalo si suala la lugha bali ujuzi wa mambo ya kila siku unaochochewa na elimu kwa kuwa mtu mwenye elimu safi huwa mdadidi na anatambua uwepo na umuhimuwa majina rasmi, mathalani, hatusemi Dar es Salaam University bali University of Dar es Salaam kama jina rasmi.
4. Huyu bwana hajui hata sheria zinatajwa kivipi na sidhani kama ni suala la lugha pekee.
5. Huyu bwana hajui kuandika neno sensa kwa Kiingereza achilia neno takwimu kwa Kiingereza na hili ni suala la upeo wa elimu na si lugha.
 
Naomba nisimwandame zaidi manake ushahidi wa kwamba tatizo ni elimu na si lugha bado ni mwingi - hata uwezo wake wa kufanya maamuzi tu unatia shaka kwa kuwa mtu mwenye elimu anajitambua na hivyo hawezi kujiachia namna hii huku akijua kuwa anaandika barua rasmi ya kiofisi itakayosambaa na kuchafua jina nchi na watu wake.
 
Mwisho kuhusu mjadala wa ELIMU na KIINGEREZA, naomba niseme hivi, kwa Tanzania Kiingereza siyo lugha, siyo suala la LUGHA bali ni suala la elimu. Uthibitisho wake ninaweza nikautoa kwa:
1. Kuwaleta watoto wa Morisi ambao licha ya kuwa Kiingereza kwao ni lugha ya tatu lakini wanakijua kuliko watoto wa Tanzania.
2. Ninaweza pia nikawaleta watu wa Aruba ambao kwa wastani wanazungumza lugha nne za kujifunza darasani.
3. Ninaweza pia nikawaleta watu wa Laksimbaga ambao hujifunza Kifaransa, Kijerumani na Kiingereza shuleni na wanavijua vyote vema kabisa.
4. Ninaweza pia nikawaleta watoto wa Kenya ambao leo wanajua kusoma Kiswahili vema kuliko wa Tanzania ingawa Kiswahili Kenya bado kibichi kabisa.
5. Ninaweza pia nikalinganisha watoto wa Tanzania wa miaka ya 1960 na 1970 na wa sasa ili kuthibitisha kwamba lugha ya Kiingereza imekumbwa tu kwenye mkumbo wa kufa kwa elimu yetu na kwamba si peke yake bali hata masomo mengine nayo yameanguka kwa sababu elimu imeanguka.
 
ANGALIZO:
Aidha, hivi leo wanafunzi wanaofaulu Kiswahili nchini wameshuka kuliko wakati wowote, ndiyo kusema kwamba hata Kiswahili tutakuwa hatukijui miaka si mingi kwa kuwa kinachoanguka si lugha ya kigeni bali kila kitu kilichomo darasani.
 
Niishie hapa daktari kwa kusisitiza kwamba Watanzania tunasumbuliwa na Kiingereza kwa sababu hatuna elimu bora - na hali iko hivyo kwenye kila somo ila ni rahisi zaidi kugundua kupitia Kiingereza kwa sababu kina wajuzi wengi na ni chombo cha mawasiliano, lakini muulize huyo huyo jamaa wa ile barua kuhusu mengine uone kama hatachekesha. Niliwahi kuwahoji wanafunzi wa UDSM walioomba kazi ya uandishi pale Business Times mwaka 2000 na nilipigwa butwaa. Huwezi kuamini kwamba aliyehitimu shahada ya masuala ya kimataifa hakujua kwamba Eritea ilizaliwa baada ya kuchomoka kutoka Ethiopia; wa sheria hakulijua jina la jaji mkuu; wa siasa hakulijua jina la waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru; na aliyemaliza shahada ya kemia alishindwa kutaja gesi mfu (inert gases) tatu, na wa uchumi alishindwa kutaja makadirio ya mbali ya bajeti ya Tanzania wakati huo, yaani range kama vile kusema kwenye bilioni 10 hata kama si sahihi lakini kujua iko mitaa gani tu. Walishindwa mengi tu ila haya ni mfano, lakini wawili (Watanzania) waliotoka chuo kimoja cha Italia - baada ya kusoma shule za misheni - walipata mpaka yasiyowahusu na kila mtu aliulizwa kutegemeana na shahada yake.
 
Mobhare Matinyi.

----------------

Date: Thu, 30 Aug 2012 09:07:18 -0700
From: mutembei@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
To: wanabidii@googlegroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com

Hapo ndipo nashindwa kuelewa.
Je huku ni "...kuanguka kwa Elimu Tanzania..." au ni KUSHINDWA KWA KIINGEREZA, Tanzania???

Ningelipenda kutofautiana na Chambi.
Pamoja na kuwa ninadhani ninakielewa anachokisema, lakini ninadhani haya ni makosa ambayo ndiyo yaliyowafikisha baadhi ya Watanzania hapa.. Watu wenye mawazo hayo, wanadhani Elimu ni Kiingereza.!!!
Kwa maneno mengine, mtoto - mwingereza wa darasa la tatu nchini Uingereza, atakuwa ANA ELIMU kuliko Profesa aliyebobea kutoka Tanzania, kwakuwa Profesa huyo akijitahidi sana, atafahamu maneno mengi na dhana mbalimbali kwa Kiingereza, LAKINI hawezi kulingana na mtoto huyo kwa Kiingereza.
Tutofautishe, Lugha ya kutolea Elimu
na Elimu yenyewe.

Baada ya kusema haya, kwangu mimi NI AIBU KUBWA SANA Kwa kiongozi kama huyu kuwasiliana na wananchi wake kwa lugha MBOVU SANA kama hivi ilivyo. Je ilikuwa ni lazima kusema hayo kwa lugha aliyotumia?
Hii kasumba kuwa Kiinglish ndio kielelezo cha Elimu itakwisha lini. jamani???

Chambi, hebu nisaidie jamani.

Aldin K. Mutembei   (PhD)                         Aldin Mutembei (PhD)
Mkurugenzi                                                  Director
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili                  Institute of Kiswahili Studies
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam                   University of Dar es Salaam, TANZANIA
+255 222 410 757     [Ofisini]                     +255 222 410757 (Day time-Office)
+255 715 426 162      [Kiganjani]                +255 715 426 162  (Cell)
b-pepe: kaimutembei@gmail.com                Alternative e-mail: <kaimutembei@gmail.com>

----------------
From: Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>; "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Sent: Thursday, August 30, 2012 2:10 AM
Subject: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania

----- Forwarded Message -----
From: Mobhare Matinyi <mobhare@gmail.com>
To: Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
Sent: Wednesday, August 29, 2012 8:16 AM
Subject: Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania

Hii ni barua iliyoandikwa na Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Oysterbay
kama ilivyo bila kupunguza wala kuongeza kitu, ikiwa na makosa yake
hivyo hivyo bila hata kurekebisha nafasi kati ya maneno:

Tarehe 25/08/2012

TO
THE ALL RESIDANCE AND
RENTER AT APARTMENT,HOTEL
AND OTHERS

REF: CENSER COUNTING PEOPLE 26 AUG 2012

Refer the above mentioned Subject.

Remember the Government of Republic Union of Tanzania announce on
26.08.2012 is the day of counting people [censer] for all living
visitors in Tanzania. This is legal order for Beural Statistics No: 1
of 2002.

Because for this day any people who sleep at your House, Hotel, or
residence apartment on 26.08.2012 he or she must be accountable in
this censer. Also all people must answer this Question from the Censer
Officer.

ORDER
If your refuse to be countable or stop censer Officer to do the job of
counting people from 26.08.2012and 7 days more its is criminal
case,then you will be charged in the court and fine with sentenced in
prison for 6 month. Then please give all assistance Censer Officer
what he or she need.

Thanks in advance,

Peter J. Mushi,
Chairman,
Local Government.

SOURCE: Attachment.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment