Sent from my Nokia phone
-----Original Message-----
From: Ellay Mnyamoga
Sent: 31/08/2012 10:57:19
Subject: Re: [wanabidii] Neno La Leo: " Banda Wa Malawi, Katuvalia Ngozi Ya Simba, Kututishia Watanzania...!"
Nakushukuru kwa namna ya peke sana katika facts zako kuhusu malawi na tanzania
----------
Sent from my Nokia phone
-----Original Message-----
From: king kingu
Sent: 8/30/2012 2:49:31 PM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Neno La Leo: " Banda Wa Malawi, Katuvalia Ngozi Ya Simba, Kututishia Watanzania...!"
Salaam Maggid! Ni kweli umenigusa sana nilikuwa kiranja wa shule ya msingi Umoja Wilayani Baharamulo nikngoza mchakamchaka nilikuwa naongoza na nyimbo za Ukombozi ikiwemo hiyo ya Banda Wamalawi katuvalia ngozi ya simba, Chinja Selema! Chinja Selema Upra wake unaukoko enzi hizo.
Lakini kama utakumbuka mwaka 1963 Mwalimu Nyerere baada ya uhuru alikataa mikataba ya Heligoland ya 1890, na Banda wa malawi akaja juu lakini si yeye ni hawa mashetani waingereza! wlimchukia nyerere na hivyo wakamtumia Banda kumchokoza nyerere kama huyu banda mwanamke anavyotumiwa na wingereza kwa faida ya uingereza kuchukua mafuta ktk ziwa Nyasa. Nyerere shujaa wa Afrika kama alivyo Kagame wa Rwanda leo 'maneno kidogo vitendo vingi' alimpa Banda masaa 24 kuwa ametoa Ubalozi wake hapa Dsm. na Kumuonya asirudie tena kujitutumua kwa Tanzania!! hiyo ilikuwa Mwaka 1967...baada ya miaka mitatu Banda alimtumia Rais wa Zambia kumuombea msamaha kwa Nyerere ili arudishe uhusiano wa Kidiplomasia. Nyere alikubali na ndipo tukarudiana kidiplomasia na Malawi.
Sasa nasema kwa wamalawi wasidanganyike na vijisiasa nya ndani mwao wakadanganywa na huyo mama Banda wao! Wajue Sisi Tanzania Tuliwaokoa waafrika katika Utumwa wa Makaburu South Afrika, Zimbabwe, Namibia, Lesotho na ktk Utumwa wa Wareno Angola na Mozambique na Kisha tukawaokoa waganda katika utumwa wa Idd Amin na Leo tunaweza kuwaokoa wamalawi katika utumwa wa huyo mamaBanda wao! Wasithubutu kuchezea upole wetu kamwe!!!!
0752318726.. nitumie sms for more details!
2012/8/18 <kimdr53@gmail.com<mailto:kimdr53@gmail.com>>
Maggid ahsante sana kwa kunikumbusha wakati ule ambapo Musumbiji kulikuwa na Wareno, Zimbabwe alikuwepo Ian Smith na walowezi wakizungu, Afrika ya Kusini Makaburu, wote wakiungwa mkono na Kamuzu Banda wa Malawi. Wakati huo sisi vijana wa zamani tuliingia JKT na kuimba nyimbo hizo! Kwa uhakika tulikuwa na jaziba na molare wa hali juu. Jamaa hao walijaribu kutuchokoza nakwambia wallahi walikipata kilichomnyoa kanga manyoya.
Sasa huo wakati umepita nchi zinazungumzia umoja, ushirikiano, na mshikamano katika maeneo ya nchi husika (Regional Unity, Cooperation, Integration) km SADC, ECOWAs, MAGHERIBs, bila kusahau AU,EU nk nk. Hiyo ndiyo dira ya nchi nyingi hasa za Afrika ili tujitoe kwenye umasikini na matatizo mengi yanayozikwaza nchi zetu. Huo ndio mwelekeo tunaotaka kusikia kwa Wana Wa Malawi na Wana Wa Tanzania. Tuwatakie kheri JK na JB katika mazungumzo yao, ili tuweze kutatua matatizo yanayokabili nchi zetu hasa umasikini na siyo vita!
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRIKA
NKOSI SIKELELA AFRIKA
Idriss Mussa
Sent from my BlackBerry® smartphone from Orange Botswana
________________________________
From: maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com<mailto:mjengwamaggid@gmail.com>>
Sender: wanabidii@googlegroups.com<mailto:wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sat, 18 Aug 2012 12:03:56 +0100
To: wanabidii<wanabidii@googlegroups.com<mailto:wanabidii@googlegroups.com>>; mabadilikotanzania<mabadilikotanzania@googlegroups.com<mailto:mabadilikotanzania@googlegroups.com>>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com<mailto:wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii] Neno La Leo: " Banda Wa Malawi, Katuvalia Ngozi Ya Simba, Kututishia Watanzania...!"
.. Hatuwezi, Hatuwezi!... Mchakamchaka, Chinja, Mchaka mchaka, chinja!
Ndugu zangu,
Utotoni niliwasikia kaka na dada zangu wakiimba wimbo huu wa mchakamchaka uliojaa hisia za utaifa. Ni kwenye mchakamchaka wa shuleni kila asubuhi.
Naam, hata wakati huo kulikuwa na utata wa masuala ya mpaka kati ya Tanzania na Malawi . Zilikuwa ni enzi za Rais Kamuzu Banda.
Na Watanzania hatukuwa na ukame wa nyimbo za kebehi dhidi ya Banda. Mwingine uliimbwa hivi; " Kipara cha Banda kina ukoko!" Hakyamungu. Hata wakati huo kulikuwa na harufu ya vita baina ya ndugu wawili; WaMalawi na WaTanzania. Maana, ukweli sisi ni ndugu wa damu.
Kuna hata simulizi za kweli za Watanzania upande wa pili wa Ziwa Nyasa waliokesha kusheherekea Uhuru wa Malawi. Hivyo basi, tunaweza kabisa kidiplomasia kutamka, kuwa "Jambo la Malawi ni letu!" Ndio, shida yao ni yetu, furaha yao ni yetu.
Na tushukuru kuwa JK wetu ni mwanadiplomasia. Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa JK anaweza kutuingiza katika ' Vita vya kiwendawazimu' dhidi ya jirani na ndugu zetu wa Malawi.
Na picha hiyo hapo juu inaongea; JK na JB ( Joyce Banda), wanazungumza kwa furaha kama ndugu. Wawili hao hawatoi nafasi kwa wachonganishi wale wa enzi za ugomvi wa utotoni. Maana, utotoni ilikuwa hivi, kaka zetu walipotaka kufurahia wadogo zao tukipigana makonde, walisubiri pale mmoja anapomkasirikia mwenzake. Haraka atatokea kaka na mchanga mkononi. Atatamka kwa mmoja kati ya wawili walio mbele yake;
" Haya, puta mchanga wangu kama kweli wewe ni mwanamme!" Nani asiyetaka kuwa mwananme? Atauputa mchanga. Kisha kaka anamgeukia mwingine; " Haya sasa, nilipie ng'ombe wangu!".
Kulipa ng'ombe ilikuwa na maana ya kuanza kurusha konde. Na hapo ugomvi ulianza rasmi!
Na kuna miongoni mwetu wenye kutamani vita. Anayetamani vita ni mtu mjinga. Mwalimu alipata kutamka; " Vita si lelemama". Na katika dunia hii inasemwa; Chagua vita vyako. Vita vingine havina lazima ya kupiganwa.
Na tofauti zetu na Malawi zinaweza kutatuliwa kwa mazungumzo ya kindugu kama anavyoonekana JK pichani akiongea na dada yake; JB- Joyce Banda.
Na wala hatuwahitaji tena akina Moses Nnauye kututungia nyimbo za Mchakamchaka. Eti twende tukiimba; " Banda ( Joyce) Wa Malawi, Katuvalia Kitenge Cha Ngozi Ya Mamba, Kututishia Watanzania, Hatuwezi, Hatuwezi!".
Naama. Wakati umebadilika.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
http://mjengwablog.com
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com<http://www.mwanabidii.com>
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com<http://www.kazibongo.blogspot.com>
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com<http://www.patahabari.blogspot.com>
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com<mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

0 comments:
Post a Comment