Wednesday, 29 August 2012

RE: [wanabidii] RE: HOFU YA UISLAM HOMA YA SENSA/Tanzania

Bwana Amour (Wale Wale), pole pole, naona karibu utasema '' Liwalo na liwe!''
1. Si kweli kwamba Waislamu hawakuunga mkono CCM kwa sababu ya Mahakama ya Kadhi. Inategemea unamaanisha Waislamu gani. Ushahidi upo kwa sababu Mahakama hiyo ilipoanza kudaiwa kwa nguvu zaidi baada ya 2005, hoja kubwa iliyokuwa ikitolewa na Taasisi nyingi za Kiislamu ilikuwa ni kwamba kama CCM hatatekeleza suala la kuanzisha Mahakama ya Kadhi, ina maana iliweka kipengee hicho katika ilani yake ili kupata kura za Waislamu (iliwadanganya). Wote tulikuwapo na tuliisikia hoja hiyo.
Juu ya kwamba Kikwete aliitwa Mbagala Spiritual Centre mwaka 2005 na kukubaliana na "wakubwa", sasa huu ndio uongo mkubwa ambao unanifanya niamini kwamba kuna uongo unaoenezwa kwa sababu ambazo ni vigumu kuzijua. Nasema hivyo kwa sababu mimi mwenyewe nilikuwapo katika semina hiyo ya wahusika wa vyombo vya habari vya Kanisa Katoliki kutoka Tanzania nzima (haukuwa mkutano). Na ilifanyika kabla ya kuanza kwa Kampeni za uchaguzi wa 2005. Sasa kama waandishi wa habari kutoka mikoani wanaweza kuitwa "wakubwa" na wakatoa maagizo kwa Rais mtarajiwa naye akayatekeleza, ni jambo la ajabu. Ni semina iliyokuwa wazi na waandishi wa habari wa vyombo vingine tu walikuwepo!
2. Ndoa ya Dr. Slaa (Padri) haikuwa hoja ya Waislamu. Wao hoja yao ilikuwa eti alikuwa ametumwa na Vatican na Kanisa. (Rejea magazeti ya Sauti ya Waislamu)
3. Hoja ya kubaguliwa kielimu ni ajabu kwamba hata wewe uliyesoma unaiendekeza. Kuna Waislamu wangapi wasomi Tanzania? Hata humu jukwaani wamo Waislamu wasomi, tuna Maprofesa gwiji, madaktari kibao. Sasa hao walisomaje? Au ubaguzi ulikuwa kwa ajili ya baadhi tu ya Waislamu? Maksi za wanafunzi wa Kiislamu zitabadilishwaje wapewe Wakristo? Mbona kuna wnafunzi Wakristo wanaofeli vibaya? Labda mwenzetu unajua, unajuaje kwamba huyu mwanafunzi ni Mkristo na huyu ni Mwislamu katika kusahihisha mtihani? Si ni namba tu ndizo hutumika? Halafu walimu huwa kadhaa, na miongoni mwao ni Waislamu. Ikoje hii?
4. Suala la mitihani ya dini ya Kiislamu, kwa vile wewe mwenyewe umesema tume imeundwa kuchunguza, nadhani ni vyema kusubiri matokeo ya uchunguzi.
 
Hitimisho
Bwana Amour (Wale Wale), reference yako kwa Mkutano wa Kikwete na "wakubwa" pale Mbagala Spiritual Centre (kama ni ule ambao na mimi nilikuwepo) na kwamba "wakubwa"  hao walimpa maagizo, imenikwaza sana na napenda niamini kwamba it was just a slip of your pen and you did not mean it. Otherwise kama hata humu jukwaani tutakuwemo watu tunaoeneza uvumi kwa vitu serious namna hii, naelekea kuamini kuwa uongo na uzushi ni maadui wakubwa wanaolipeleka taifa hili katika maangamizi! Na hii ni hatari kubwa.
 

Date: Wed, 29 Aug 2012 04:41:23 -0700
From: abachamani@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] RE: HOFU YA UISLAM HOMA YA SENSA/Tanzania
To: wanabidii@googlegroups.com

Bwana Magobe,
Nimesoma ulichokiandika zaidi ya mara 2 bado sijakuelewa kabisa kama unalaumu,unauliza au unaelekeza.Ulichosema sitakiandika ila nitajiribu kujibu na kueleza na pengine kufafanua ninavyojua mimi.

1.Waislam hawakuunga mkono CCM kwasababu ya mahakama ya kadhi.Kumbuka suala hili lilianza mapema na lilianzishwa na Mh.Mrema alipokuwa mbunge wakati wa Mkapa.Waislam 2005 walimpinga sana Kikwetena hili linatokea kwenye matamshi yake aliyoyasema wakati ule alipoteuliwa na Mwinyi kuongoza Wizara ya Fedha kutoka kwa Prof.Malima.Alimkejeli na kumtukana shujaa wetu tukamchukia.Pengine ndiyo maana akazawadiwa nafasi ya kugombea urais kwenye CCM kilichotokea bila shaka kila mmoja anajua.
Alipoingia 2005 akajua njia ya mafanikio ipo Kanisani akaitwa pale Mbagala Spiritual Center maarufu kama Misheni akakubaliana na wakubwa kisha akaenda Mbeya kwenye sherehe za waislam na kusema kam si Kanisa angekuwa Bagamoyo anauza njugu.Akawashambulia Waislam na tangia hapo akawa anaitwa Chaguo la Mungu huku Waislam wakisema ni chaguo la Kanisa.
Baada ya kupata ushindi mkubwa bila jasho akaanza kuunda serikali lakini cha kushangaza zile Wizara nyeti akawapa Waislam mkubwa mmoja wa Wakatoliki akasema "Kiongizi Ndimi mbili Hafai" kilichoendelea baada ya hapo ni hayo unayoyaeleza ya uchaguzi wa 2010.Yakatoka maazimio ,matamko nk na Waislam wakayapinga sana kwamba Dini inachanganwa na Siasa.
Bahati mbaya hawakusikilizwa na lakini kama unavyojua adui wa adui baadhi wakaingia kumpigia kura mwaka huo na ikawa kama ilivyokuwa.

2.La ndoa ya Padri Slaa hizi ni siasa na halijaanzia kwake.1995 tuliambiwa Prof.Lipumba hakuwa na mke na hakufaa kuongoza nchi na tukaambiwa si lazima kiongozi wa nchi awe na elimu kubwa ya uprofesa nk hizo ni siasa na hamna la kuangalia humo.

3.La kadhi naomba nimnukuu Kikwete alichosema kule Dodoma.
"Mheshimiwa Mufti, Waheshimiwa Masheikh, Ndugu Zangu Waislamu;
Napenda kuwatoa hofu pia kwamba hakuna mkono wa mtu wapo mnadhania hivyo. Maana, tunajuana. Si ajabu kuna hisia kuwa huenda Kanisa limeingilia kati kuzuia au kuchelewesha. Siyo hivyo hata kidogo. Tarehe 22 Julai, 2011 nilipoalikwa kuzungumza na Maaskofu katika kikao chao cha Jukwaa la Wakristo katika risala yao kwangu kuhusu suala la Mahakama ya Kadhi walitoa ushauri ufuatao kuwa:
"Kuanzisha Mahakama ya Kadhi nchini na jambo zuri linalowahusu Waislamu. Kwa kuwa ni jambo la kidini waachiwe Waislamu wenyewe walifanye ndani ya Uislamu, pasipo kutumia hazina ya Serikali ambayo ni fedha ya walipa kodi wote nchini"
Hiyo ni nukuu kutoka ibara ya 6 ya Risala yao kuhusu Uhuru wa Kuabudu na dhana ya Udini.
Katika maelezo yangu kwao, niliwahakikishia kuwa mawazo yao yanawiana na yale ya Serikali kama ilivyoshauriwa na Tume ya Kurekebisha Sheria ambayo Mwenyekiti wake ni Profesa Ibrahim Juma. Mahakama hii itaundwa na Waislamu wenyewe ndani ya Uislamu wao na wataiendesha wenyewe na haitagharamiwa na Serikali."
Sijajua hapo ulitaka kusema nini.

4.Ni aina gani ya ushahidi unaoutaka ili uweze kuamini wewe.Maana umeishatolewa mwingi sana ambao mwisho ya yote tunaambiwa kuwa ni uongo.

5.La shule mimi hapana sina haja ya kuuliza kwani najua sababu.

6.Unapinga hata la NECTA? hivi unahabari kwamba imeundwa tume kimyakimya na tayari imeisha fanya uchunguzi na kutoa taarifa kwa Waziri ila anatafakari cha kuwambia watu au pengine asiseme kabisa.Subiri la Sensa liishe.

7.Kuhusu imani za waandishi wa magazeti na hata Waislam kwa ujumla pengine kweli ni ndogo na ndiyo maana hawawezi kufuata mafundisho yao ya dini kwamba CHINO KWA JINO tofauti na yenu kwamba ukichapwa shavu moja unageuza jingine.Leo wanfanyiwa yote haya lakini bado tunacheka vizuri na tunachati hivi kwenye mitandao nk.

8.Sina la kusema.

9.Ajenda binafsi vipi na ipi na kwa manufaa ya nani na vipi hayo manufaa.
Mbinu hii imetumiwa sana na watawala leo unasikia CHADEMA wanaambiwa wanatumiwa na wameletewa mapesa mengi kutoka nje na Zama za CUF unakumbuka kila wakati tulikuwa tukiambiwa mapesa kutoka Urabuni na mapanga ya kuua watu.Leo ndugu yangu unaimba wimbo huo huo.

10.Hizo tuhuma ni za kweli suala ni ushahidi gani unataka basi rejea no.4.

11.Kwanini tusiende mahakamani.
Kweli lakini namna nzuri ya kujua kwanini hatuendi mahakamani ni kwa kuangalia jinsi zilivyo maahakama zetu.
Waulize CHADEMA kwanini walichagua PEOPLES POWER badala ya mahakama.
Waulize Madaktari na Walimu nini kilitokea mahakamani.
Waulize Mwana Halisi kwa nini wameshindwa kwenda mahakamani.
Ni njia ndefu na ngumu zaidi ya kupitia ila hizi nyingine za nje ya mahakama zikishindikana tutaelekea huko.

12.Hatuwezi kujenga chuki na Wakristo kwani ni kinyume na mafundisho ya dini yetu lakini hili litakuwa na maana zaidi kama tutaheshimu vilevile mafundisho ya dini yetu ya kiislm yasemayo.

NI HARAMU KUDHULUMU NA NI HARAMU KUDHULUMIWA.


Walewale.


From: Telesphor Magobe <tmagobe@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, August 29, 2012 11:36 AM
Subject: Re: [wanabidii] RE: HOFU YA UISLAM HOMA YA SENSA/Tanzania

Tatizo ninaloliona ni 'suspicion'.

1. Wakati Waislamu wanaahidiwa suala lao la Mahakama ya Kadhi
lingeshughulikiwa na serikali kabla ya uchaguzi Mkuu 2010, baadhi yao
walionekana kuegemea upande wa CCM (wakidhani ilikuwa upande wao) na
wakaanza kuzusha kuwa Chadema kinafadhiliwa na Kanisa Katoliki na
kwamba Dr Slaa amewekwa na Vatican mara na maaskofu ili kumwondoa Rais
Jakaya Kikwete kwa vile ni Mwislamu. Haya nilikuwa nayasoma na
kuyasikia pia kwenye baadhi ya mihadhara Dar es Salaam.

2. Baadhi walisikika wakihamasisha waumini wao kutomchagua Dr Slaa kwa
vile ndoa yake walidai ilikuwa na utata - kwambwa amepora mke wa mtu -
na hivyo hawawezi kuongozwa na mtu asiye mwadilifu kwa mambo ya ndoa
kwa sababu atashindwa kutawala nchi pia.

3. Rais Kikwete alipokutana na viongozi wa Waislamu Dodoma na
kulitolea ufafanuzi suala la Mahakama ya Kadhi na kusema
litashughulikiwa na Waislamu wenyewe na siyo serikali na kwamba
serikali imepokea maoni ya kamati iliyokuwa imeundwa kuliona vizuri
suala hilo (ambayo mwenyekiti wake alikuwa gwiji wa sheria za Kiislamu
na senior lecturer UDSM), phrase ya 'Mfumo Kristo', ambayo ilikuwa
inatumiwa na baadhi ya magazeti na radio zilizo chini ya taasisi za
Kiislamu ikaanza kushika kasi. Sasa hivi 'Mfumo Kristo' umeshakuwa
msamiati unaoonesha Tanzania inaongozwa kulinda Maslahi ya Kanisa
Katoliki au Wakristo.

4. Mambo ambayo yalikuwa yanasemwa kwa chini chini kuhusu Waislamu
kubaguliwa kielimu na maksi zao kupewa Wakristo, yakaanza kusemwa wazi
lakini bila ushahidi wowote.

5. Yaliaanza pia maswali kwa nini shule nyingi za taasisi za Kikristo
zinafanya vizuri wakati zile za Kiislamu zinafanya vibaya kila mwaka,
kuna nini?

6. Hata mtihani wa dini ya Kiislamu (ambao walimu wake naamini siyo
Wakristo) wanafunzi walipopata maksi za chini, walisingiziwa Wakristo
walio Baraza la Mitihani kuwa wanawahujumu Waislamu.

7. Kwa bahati mbaya, mambo kama haya huwa yanasemwa na viongozi na
wanawaaminisha waumini wao kuwa wanahujumiwa na 'Mfumo Kristo' na
inabidi wapambane nao. Mpaka sasa ukisoma mambo yanayoandikwa kwa
baadhi ya magazeti yenye mtazamo dhidi ya 'Mfumo Kristo' inasikutusha
sana. Wakati mwingine huwa najiuliza kama waandishi na wahubiri wa
mambo haya wana chembechembe yoyote ya kumcha Mungu kwenye nafsi zao!

8. Katika hali hii na sasa pia kuingiza suala la sensa kwa mantiki
ileile ya kuonesha kuwa Waislamu wanahujumiwa na 'Mfump Kristo'
sidhani kuna kitu chochote cha maana tunachokijenga hapa.

9. Naamini kabisa tukitumia dini kupenyeza ajenda binafsi na kuifanya
iwe na sura ya kiimani tunamkosea Mungu.

10. Kuna mambo mengi yameandikwa kwenye magazeti na vitabu na kwenye
TVs na mengine yamerikodiwa kwenye CDs kueneza uongo kuwa Waislamu
wanahujumiwa au wananyimwa fursa za elimu na ajira na badala yake
wanapewa Wakristo.

11. Ushahidi uko wapi? Kama hayo yanayosemwa yana ukweli kwa nini
wanaolalamika wasiende mahakamani kudai kuwa wanaonewa ili mahakama
ipitie ushahidi uliopo na kulitolea hukumu suala hili?

12. Otherwise, kitu ninachokiona ni kujenga na kueneza chuki kati ya
Wakristo na Waislamu au kati ya vizazi vijavyo vya Wakristo na
Waislamu.

On 8/29/12, amour chamani <abachamani@yahoo.com> wrote:
> Laurean,
> Huo ndiyo utanzania wetu na undugu wetu ambao sisi tunadhani ungefuatwa.
> Cha kufanya ni kuwasikiliza wanachosema hawa Waislam bila ya jazba kisha
> wakaambiwa kwamba hili na hili au yote hayawezekani lakini kwa hoja siyo
> vitisho wala kubezana.
> Kama hawana hoja si basi mambo yataendelea vema.
> Na kama wana hoja tuzikubali japo inauma kidogo.
>
>
>
> Walewale.
>
>
>
>
> ________________________________
>  From: Laurean Rugambwa <rugambwa@hotmail.com>
> To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
> Cc: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
> Sent: Wednesday, August 29, 2012 11:25 AM
> Subject: Re: [wanabidii] RE: HOFU YA UISLAM HOMA YA SENSA/Tanzania
>
> Chamani
> Wewe ni ndugu yangu japo  hatujuani, wewe unapendekeza kifanyike nini? List
> what you think the government should do or  fellow Tanzanians!
>
> From LRB
>
> On 29 Ago 2012, at 9:24, "amour chamani" <abachamani@yahoo.com> wrote:
>
>> ukweli.
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.





--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment