On Thursday, January 1, 2015 5:30:47 AM UTC-8, Godfrey Ngupula wrote:
> Jimbo la ludewa ndio linakaliwa na deo filikunjombe? kama ni hivyo jitie moyo na ukajaribu....Deo ni moja ya wabunge wazur sana wa bunge la 2010...2014...kwa mtazamo wa wengi..Ngupula
>
> 'amon mkoga' via Wanabidii <wana...@googlegroups.com> wrote:
>
>
> Una hela ya kampeni watakuchuja asubuhi tu.
>
>
>
> AMON MKOGA
>
>
>
>
>
>
>
>
> On Thursday, January 1, 2015 1:20 AM, Abdalah Hamis <hami...@gmail.com> wrote:
>
>
>
>
>
>
> TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
> WILLIAM HAULE ATANGAZA RASMI NIA YA KUGOMBEA UBUNGE MWAKA HUU 2015
> Mimi William Haule, kijana wa miaka 24, mhitimu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam katika fani ya Sayansi ya Siasa na Utawala, mwanadiplomasiamchambuzi wa masuala ya siasa, leo tarehe 01/01/2015, nachukua fursa hii kutangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Ludewa katika mwaka huu wa uchaguzi 2015.
> Hii ni mara yangu ya kwanza kutangaza kuwa nitagombea ubunge Jimbo la Ludewa, kwa kuwa nimeombwa sana na vijana, wazee wa vijiji mbalimbali vya jimbo la Ludewa, na ni mara nyingi nimekuwa nikiwaambia bado muda, lakini sasa umebaki muda mfupi hivyo niseme tu na kuwahakikishia kuwa nitagombea.
> Kwa kuwa uongozi ni mbio za kupokezana vijiti. Naaamini katika kutoa mchango wangu juu ya maendeleo ya jamii kuliko kusubiri kufanyiwa nini na Taifa langu. (kama alivyowahi kusema raisi wa zamani wa marekani Bw. John F. Kennedy).
> Kasi ya maendeleo ya Ludewa hairidhishi na matatizo mengi ya msingi hayapatiwi ufumbuzi. Kero zinazowakabili watu wa Ludewa ni nyingi na zinahitaji mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kubuni miradi mbalimbali itakayoweza kuharakisha maendeleo ya Ludewa. Wananchi wa Ludewa wanahitaji kuwa na kiongozi mwenye kupenda maendeleo, mwenye fikra mbadala na mwenye uwezo wa kuanzisha msukumo mpya wa kasi ya maendeleo kulingana na kero zao na vipaumbele vya kisera na kimikakati vya kiwilaya na kitaifa. Kuna mambo mengi hayajakamilika na utekelezaji wake unalegalega.
> Kwa kuyaangalia yote haya, nimetafakari kwa umakini na kujipima uwezo wangu, na nimeonelea nianze kwa vitendo ili niwe chachu ya mabadiliko kwa watu wa Ludewa, ambako ndipo nilipozaliwa. Charity begins at home, na ndo maana nimeamua kuwania ubunge wa Ludewa ili nishiriki kikamilifu na kwa ukaribu zaidi pamoja na wana Ludewa wenzangu katika kuzikabili changamoto za maendeleo katika jimbo la Ludewa kwa spidi na kwa ubunifu wa hali ya juu, maana mimi kila nikiiangalia Ludewa, sioni matatizo au vikwazo vya maendeleo, bali naona fursa tu za kuleta mabadiliko. Japokuwa Ludewa ina fursa nyingi, na ni mojawapo ya wilaya kongwe, kasi yake ya maendeleo haiendani na fursa zilizopo.
> Ni matarajio yangu kuwa wananchi wa Ludewa tutaungana pamoja kupata mtu stahiki anaye tambua kero na matatizo yetu lakini pia mwenye mikakati madhubuti ya kukabiriana nayo.
> Kuna umuhimu mkubwa kwa viongozi mahiri na wenye nia thabiti ya kuwatumikia watu wajitokeze popote walipo na waje kuongeza nguvu kwa taifa letu ili tuweze kupambana na maadui wanaotukabili kama vile umasikini, ujinga, magonjwa na dhuluma (rushwa, ufisadi, ukiukwaji wa haki za binadamu, n.k). Tatizo kubwa ni kwamba watu wengi wanaogopa kuingia kwenye ulingo wa siasa kwa kuwa hawajiamini katika uwezo wao wa kukabili mikiki mikiki inayoendana na siasa, wengine wanafikiri siasa ina wenyewe, wengine wanasubiri wastaafu ndiyo waingie kwenye siasa. Hivi utaweza kutawatumikia watu vizuri wakati ukiwa umechoka?
> Vijana wengi wasomi na wachapakazi wazuri kabisa wanasahau kwamba siasa ni mfumo wa maisha yao ya kila siku na kwamba hadi majumbani mwao wanafanya siasa– wengine ni watu makini sana na wangeweza kuchangia mengi kwenye kuleta maendeleo ya taifa letu. Tatizo kubwa ni kwamba watanzania ni wazuri sana wa kusema na kupanga lakini ni wavivu wa kutekeleza, hivyo tunahitaji viongozi watendaji kwenye kila sekta, popote walipo wafanye mabadiliko! Tuache kuongea na kupanga tu, sasa tuanze kuwa mabingwa wa utekelezaji! Lakini pia viongozi wengi si wabunifu, wavivu wa kufikiri na hivyo hata utendaji na usimamizi wao wa sera nzuri zilizowekwa unakuwa mbovu.
> Leo hii nimeamua kuiweka nia yangu hadharani kabisa kuwa kwa ridhaa yangu na matakwa yangu binafsi, nafsi yangu inanituma na hapa basi natangaza rasmi nia yangu kuwa, pindi wakati utakapowadia nitachukua fomu kuwania ubunge wa jimbo la Ludewa kupitia chama changu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Naomba Mwenyezi Mungu aniongoze. Amina.
> NOTHING TO FEAR THAN THE FEAR ITSELF!
> Ahsanteni!
> …………………………………….
> WILLIAM HAULE
> Mob: +255 (0) 657 878416
> E-mail: william...@yahoo.com
>
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wana...@googlegroups.com
>
>
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
KUMTOA DEO NIKUPITIA UKAWA KAMA CCM HUKO HUKO HUNA HOJA KWA DEO
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment