Nakubaliana na maelezo ya ndugu Lushinga Lutina na kuongeza kuwa tatizo kubwa hapa ni sera za nchi hazikusudii kuleta usawa katika ushiriki wa Vijana katika shughuli za kiuchumi zaidi sana kundi kubwa linaelekea kufanya Usanii wa Muziki na nyimbo za Injili ambako matajiri hawaelekezi nguvu zao huko. Nimeona katika Jiji la Copenhagen na Oslo Vijana wanapewa nafasi kubwa katika fursa za ajira hata wale wanaosoma chuo kuna kazi za muda nyingi kila anapotoka chuo ili kupata fedha ya kujikimu, kuna usawa katika kusaidiwa Elimu,Afya ,Umeme,Usafiri na Maji serikali inasaidia kwa kiwango kikubwa (75%), upatikanaji wa vitu kama vile vifaa vya umeme, simu n.k hivi wanakopeshwa kwa kulipa kidogo kidogo kila mwezi.Kila kijana anapofika umri wa miaka 18 anapewa chumba cha kupanga lakini huku Tz nyumba zinazojengwa zinauzwa tena kwa bei kubwa pamoja na kujengwa na serikali na kuitwa za kukopeshwa.Usafiri na uchukuzi ni tatizo kubwa sana ktk miji mingi mikubwa miradi inayowekwa inalenga maeneo wanapotoka wakubwa badala kuleta ufumbuzi wa matatizo katika jamii iwe daladala,taxi,treni na ndege shida tupu ,wanashindania kuwa na mashamba makubwa au miradi mingi; sasa Kijana afanye vipi pia siyo sahihi kusema wananunua kwa ajili ya anasa.Mashirika au Taasisi za mifuko ya kijamii ipo kibiashara zaidi na siyo kupunguza umaskini au kukuza ajira kwa vijana; kwa nini kuna utitiri wa mifuko ya Jamii ya Serikali kuna nini ? Udhaifu mkubwa katika mfumo wa ukusanyaji Kodi ambao ungeweza kuihakikishia Serikali mapato ya uhakika.
On Tuesday, January 20, 2015 3:47 PM, Lushengo Lutinwa <lutinwa@gmail.com> wrote:
inawezekana obligation wanazo-incur, zinazo-exhaust vimishahara vyao, ndio zinawatia pressure na kutufanya tuwe ni kizazi cha mafisadi. kwa sababu mahitaji yetu yanazidi kipato chetu.
2015-01-20 15:14 GMT+03:00 mngonge franco <mngonge@gmail.com>:
Ushauri wako ni mzuri lakini kila rika na kila mtu ana kitu ambacho akikifanya roho yake inasuuzika. Kama ulivyowaita vijana ni sahihi kabisa kufanya hivyo kwa sababu ya umri. Tupo ambao hatukukopa magari wala nini na nyumba hatukujenga. Yapo mambo mengi ambayo ukiwa kijana usipoyafanya utakuwa na kasoro nafikiri hata wewe ni mmojawapo.
Ukiyakumbuka kwa sasa unaona ulikuwa utoto, lakini kwa wakati ule yalikuwa ni ya lazima. waache wakikua wataacha wenyewe.Kujenga ni mradi wa muda mrefu na gharama yake ni kubwa kuliko gharama ya kununua gari.
Ni heri wakayanunua hayo magari roho zao zikasuuzika ili wapate kuishi miaka mingi kuliko kujibana kupindukia hadi kupunguza siku za kuishi. Hili jambo ni paradoxical ni vyema tukaliangalia kwa upana wake kuliko lilivyo--2015-01-20 14:01 GMT+03:00 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>:--VIJANA NA MAGARI YA MIKOPOVijana wengi wakiingia kwenye soko la ajira kitu cha kwanza wanachofikiria kufanya ni kununua gari. Kuna wachache wanazichanga na kununua gari lakini wengi wao wamenunua magari kwa mkopo, Vijana wengi hapa mujini wanaendesha magari ya mkopo. Utakuta mtu badala ya kuchukua mkopo ili afungue biashara ya kumuingizia kipato, wao wanakopa magari ili waonekane wapo juu kimaisha. Gari lenyewe unalolikopa badala likuingizie kipato lenyewe ndio linakukaanga, kila siku lazima uliingize sheli kununua mafuta, kila mwezi lazima mshahara wako ukatwe kulipia gari ulilokopa, gari lenyewe nalo linahitaji kufanyiwa service. Watu wanafanya kazi, wanalipwa kipato kizuri lakini mishahara yao haiwatoshi kwasababu ya magari waliokopa.Mtu unachukua mkopo wa gari wakati unaishi nyumba ya kupanga na huna hata kipande cha ardhi cha kujenga choo.. Pumbavu... Kwanini usichukue mkopo ukanunua ardhi ukaanza kujenga nyumba yako taratibu?? au kwanini usichukue mkopo ukafanya biashara ili upate njia nyingine ya kujiingizia kipato?? Shida ya vijana mlio wengi, mademu mnakopa magari kuwaringishia mashoga zenu mtaani na wanaume mnakopa magari ili muwapate kiurahisi mademu coz hapa mujini kama una gari ukitongoza demu hakatai... Wengi mnakopa magari eti kwasababu hamtaki kupanda daladala
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:
Post a Comment