Hii yote ni mikakati ya kukiangusha Chama Cha mapinduzi.
Kama Rais atawasikiliza ambao hawakusikilizwa na wananchi akae akijua kuwa wananchi walilisikiliza Bunge kama wanavyosikiliza na kuangalia mpira wa Manchester.
Wanajua kilichoongelewa. Hakuna mwananchi atakayewasikiliza vijana wadogo hao ambao kwenye majukwaa ya siasa wala hawataonekana. UKAWA itakapo simama na kuwakumbusha wananchi kilichoongelewa bungeni na kuwa Rais amekipuuza huo utakuwa mwisho wa CCM. Siamini kama rais au wasaidize wake watawasikiliza hawa vijana wa vyuo hata wangekuwa na la kusema. wamechelesa na huenda ni heri wqakanyamaza.
--------------------------------------------
On Tue, 12/16/14, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] KUUNGA MKONO KAULI YA JUMUIYA YA WANAZUONI VIJANA TANZANIA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, December 16, 2014, 11:45 AM
UMOJA
WA
WANAZUONI WA VYUO VIKUU DODOMA KUUNGA MKONO KAULI YA JUMUIYA
YA WANAZUONI
VIJANA TANZANIA ILITOLEWA JANA MJINI DAR ES SALAAM.
UTANGULIZI.
SISI ni mkusanyiko wa wanazuoni wanaosoma vyuo vikuu
mbalimbali mkoani Dodoma,
tumejitokeza kuzungumza na nyinyi waandishi wa habari
kuhusiana na mambo
mbalimbali yanayofanyika nchini ikiwemo suala zima la
AKAUNTI YA TEGETA ESCROW.
Pia, tumejitokeza kuunga mkono kauli ya Jumuiya yetu ya
vijana wanazuoni juu ya
tamko lao walilolitoa kwenye vyombo mbalimbali vya habari
jana na kupewa nafasi
kubwa kwenye vyombo hivyo ikiwemo magazeti na radio.
Tunashukuru sana kwa hilo
ndugu waandishi.
AKAUNTI YA ESCROW
Kabla hatujazungumza tunapenda kuwaasa hasa wanasiasa jambo
lolote ukiwa hauna
uhakika nalo, usipende kulizungumzia mbele ya umma kwa kuwa
mwanasiasa ni mtu
makini na mwenye uelewa mpana wa mambo.
Tumekaa kwa muda mrefu tukisoma taarifa mbalimbali kwenye
magazeti na kwenye
mitandao kuhusiana na suala la akaunti ya ESCROW ili kujua
ukweli wa suala
hilo, ambalo kwa kiasi kikubwa linazidi kupotoshwa.
Tunafurahi sana kupata nafasi hiyo ya kuzungumza na nyinyi
waandishi wa habari
kwa kuwa ni watu muhimu na mtaweza kuhabarisha umma juu ya
usahihi wa
taarifa
kuhusiana na sakata hilo, baada ya kufanya utafiti wa
kutosha na kuelewa mambo
mengi.
Sisi wanazuoni tunawajibu mkubwa wa kuitetea nchi na
kuisemea pale tunapoona
kuna jambo baya limefanyika, kwa kuwa uelevu wetu umetokana
na kupata elimu
bora iliyotokana na kodi za watanzania wenzetu na hatupo
tayari kuona mambo
yakienda mrama.
Tukiwa kama wasomi vijana, tuna wajibu kwa taifa letu
kulipigania ili
kuhakikisha kuna usawa kwa kuwa Tanzania ni taifa huru na
linahitaji kuwepo kwa
wanasiasa huru na wenye maono ya kuifikisha nchi pahala
salama kwa kuwa uwezo
na maadili yao ni muhimu.
Pia, tunapaswa kuhakikisha nchi yetu inaendeshwa kwa kufuata
misingi imara ya
ukweli, uwazi, uwajibikaji na kuzingatia uhuru wa haki kwa
kila mtu na
watanzania waelewe kuwa kujiuzuru sio ushujaa au uzalendo.
Jiulize wote
waliojiuzuru ni wazalendo wa kweli wa nchi yetu?.
Wabunge wametufedhehesha, wametunyong'onyesha na
wameonyesha ni jinsi gani
wameshindwa kuwa wakweli kwenye kusimamia sheria na uhuru wa
haki wa kila
mtu(natural justice) kwa kutengeneza tuhuma na kisha kumtaka
Rais Jakaya Kikwete
awawajibishe watu hao.
Sote sie tunakumbuka kwamba hivi karibuni Ofisi ya Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) ilitoa taarifa ya uchunguzi wake wa
akaunti ya TEGETA
ESCROW kwa serikali na kwa bunge na ripoti hiyo iliweza
kuvuja kwenye mitandao
mbalimbali
Kuvuja
huko kulitusaidia sie kupata taarifa za ripoti hiyo na
kuzisoma kwa umakini,
ueledi na ufanisi mkubwa na kugundua kinachozungumzwa sasa
ni mchezo wa kisiasa
unaochezwa na wabunge wakishirikiana na wafanyabiashara
mbalimbali.
Ripoti
iliarifu juu ya hadidu za rejea 11 ilizopewa, pamoja na
kutaja ofisi mbalimbali
zilizoanza kuomba kufanyiwa uchunguzi kabla ya Ofisi ya
Bunge, ikiwemo Ofisi ya
Waziri Mkuu na Ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
Madini.
Jitihada
za ofisi hizo, zilisaidia kupatikana kwa taarifa bora na
yenye mantiki kwa
jamii na ndio maana katika uchunguzi wake, CAG hakusema kuwa
ESCROW ni fedha za
umma au la, pia alisema kuwa uchunguzi wake haukumtia
hatiani mtu au kikundi
chochote cha watu kilichohusika katika sakata hilo. Je
tujiulize yale
yanayozungumzwa kwenye mitandao na uamuzi wa kamati ya Bunge
ya Hesabu za
Serikali(PAC) imepata wapi?.
Tunatambua
kilichofanywa na PAC kugeuza ripoti ya CAG na kuitengeneza
ripoti yao isiyojaa
uzalendo wa hali ju ni kumharibia jitihada za Rais Jakaya
Kikwete kuonekana ni
kiongozi anayeongoza serikali ya kifisadi wakati sio kweli.
Rais Kikwete
amefanya mambo mengi makubwa kwa nchi hii na tutamkumbuka
kwa ukarimu wake
aliokuwa nao licha ya kuwepo kwa upuuzi, uzandiki
unaoendeshwa na watu hasa
wabunge huku yeye mwenyewe akiwa anacheka na kutoa ushahidi
wa kila jambo
kwenye vyombo vya habari.
Katika
ripoti ya CAG pamoja na viambatanisho vyake
vyote,
tumesoma na kuvirudia na hakuna iliyosema kwamba Waziri mkuu
amelisababishia
hasara Taifa au mawaziri wengine nao wameshiriki kuliletea
hasara taifa huku
wabunge wenyewe wakiwa wanafanya shughuli za kitaifa
kishabiki, kichuki,
kimaslahi binafsi bila kuzingatia ukweli na misingi ya
Utawala bora.
Ndugu
zangu, kwenye Ripoti ya CAG kumesema wazi kwamba, serikali
imefanya jitihada
stahili kuhakikisha taratibu zinafuatwa ili kujiondoa kwenye
madhara yanayoweza
kutoke baada ya pesa kufuatwa.
Ripoti
ya CAG haijamtia hatiani mtu yeyote je kinachozungumzwa na
PAC ni sahihi? Au
mapendekezo yao kwa Rais yamezingatia utawala bora?.
Haya
ni maswali ambayo PAC inapaswa kuyajibu ili umma wa
watanzania na sisi wasomi
tuelewe kuliko kukaa juu juu na kuimba wimbo wa Waziri wa
Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo ajiuzuru, au Katibu wake, Eliakim
Maswi ajiuzuru au
hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema naye
ajiuzuru. Je
kujiuzuru kwao ndio suluhisho la matatizo au ndio
uzalendo?.
Tunashindwa
kuelewa misingi ya kamati ya PAC ya kutaka kuwajibishwa kwa
watu hao bila ya
kuwa na hatia yeyote ikiwa taasisi ya ukaguzi inasema hakuna
kosa
lililofanyika, Je PAC wamepata wapi makosa?.
MAPENDEKEZO
NA MSIMAMO WETU.
Kwa
kuwa Bunge wao wamepeleka maombi yao haramu kwa Rais, nasisi
tunapeleka
mapendekezo yetu kwa Rais na kumsihi afanye
yafuatayo
1. Kwa
kuwa Swala zima la ESCROW limegubikwa na siasa, maslahi
binafsi, chuki, wivu na
kukomeshana, hivyo tunamuomba Rais asitekeleze azimio hata
moja mpaka kwanza
umma utakapoelezwa ukweli halisi wa mbivu na mbichi na kila
lililo nyuma ya
pazia kuhusiana na sakata hili
2.
Tunamuomba Rais aunde chombo huru, ili swala hili
lichunguzwe na kufanyiwa
maamuzi huru pamoja na kuviagiza vyombo vyake vya ulinzi na
usalama
viwachunguze wabunge hawa kwa kukubali kutumiwa, kuhongwa na
kununuliwa ili
kutuondolea watetezi wetu wa Rasilimali.
Mungu
ibariki Tanzania.
Imesomwa
na
Josephat
Joachim
0768-911840
………………………………………………………
Katibu
Mtendaji wa Umoja wa wanazuoni wa Vyuo Vikuu
Dodoma.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment