Wednesday, 31 December 2014

[wanabidii] Salaam Za Mwaka Mpya: Mwaka 2015 Uwe Ni Wa Kusonga Mbele Zaidi..


Ndugu zangu,

Saa chache zijazo tunaingia Mwaka Mpya wa 2015.
Kwangu mwaka 2015 nadhamiria uwe ni wa kusonga mbele zaidi. Na ningependa sote tuwe na dhamira hiyo ya kusonga mbele kama watu binafsi na kama taifa. Tutangulize zaidi maslahi mapana ya nchi yetu.

Kama ilivyokuwa mwaka huu unaomalizika, mwaka 2015 nitapenda nijikite zaidi kwenye kuhamasisha juhudi za maendeleo kwa Wanawake na Vijana wa Vijijini. Nitapenda pia niimarishe Jukwaa la ' Kwanza Jamii Dialogue' kwa maana ya mijadala ya wazi kuhusiana na masuala muhimu ya kitaifa.

Ni kwa kupitia KwanzaJamii Radio pia. Ni kwa kuwahakikishia watembeleaji wa Mjengwablog na wasikilizaji wa KwanzaJamii radio mtandaoni kuwa tutakuwa wa kwanza kuwaletea habari za kichambuzi kuanzia saa kumi na moja na nusu alfajiri. Ni kwa kuwaletea magazeti ya siku husika, na kuyachambua pia. Kwenye Mjengwablog na KwanzaJamii Radio.

Hivyo basi, kuimarisha concept yetu ya ' Soko la Habari Kariakoo'.
Mapya mengine?

Tutawaletea kipindi kipya cha ' Mwangaza wa Watanzania Diaspora'. Kipindi kingine ni cha ' Football Baraza'. Yepi yatakuwamo ndani? Usikose kutufuatilia kuanzia kesho Januari Mosi, 2015.

Naam, nitapenda kujikita kwenye yale yenye pia kuibua mijadala endelevu kwa maendeleo ya nchi yetu.

Pamoja na yote hayo, mwaka 2015 nitajitahidi, kama mzazi, kutenga muda zaidi wa kuwa na familia yangu; mke wangu mpenzi na wana wangu.

Nawatakia nyote HERI YA MWAKA MPYA!
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0754 678 252

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment