Wednesday 31 December 2014

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] Neno La leo: Mwalimu Alisema Na Sisi Tunasema.. Tanzania Would Never Be ' Another Congo'..

Sijui kwa nini lakini nimevunjika mbavu kwa maneno haya:
...tumeumaliza mwaka kwa ugomvi mkubwa......

On Dec 31, 2014 9:57 AM, "Maggid Mjengwa" <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:


Ndugu zangu,

" Kamwe Tanzania Haitakuwa ' Congo Nyingine'. Hayo yalipata kusemwa na Mwalimu Julius Nyerere miaka ya mwanzoni mwa Uhuru. Unaweza kuyasoma kwenye kitabu kilichoandikwa na Sir Andy Chande, A Knight In Africa, Ukurasa wa 77.

Alichokiona Mwalimu miaka ile ya 60 ndicho ambacho, baadhi yetu, kwa kutanguliza maslahi yao binafsi, na hata kwa kusingizia kuwa wao ni Wazalendo zaidi kuliko wengine, hawataki kukiona.

Congo ya MwanaMapinduzi Patrice Lumumba imeangamia kutokana na laana ya rasilimali zake.

Patrice Lumumba alikuwa ni mwanamapinduzi wa kweli. Alisimama upande wa umma. Alitaka rasilimali za Congo ziwanufaishe Watu wa Congo. Mabepari hawakuupenda mtazamo huo wa Lumumba ambao ulijielekeza zaidi kwenye itikadi ya Ujamaa. Mabepari walimtumia kibaraka, Joseph Mobutu kumsaliti nduguye Lumumba na kuchukua madaraka ya nchi. Lumumba aliuawa kinyama. Mobutu hakuwahi kuwa Rais wa Watu, bali, kibaraka na zaidi Wakala wa Matajiri walio nje ya Congo.

Watanzania tumeumaliza mwaka na ' Ugomvi Mkubwa'. Kinachoitwa sakata la Escrow kimsingi ni ugomvi wenye kuhusu rasilimali. Ndio maana ya kuhusu zaidi sekta ya Nishati na Madini.

Kuna makosa yamefanyika, wenye kuhusika wawajibishwe, lakini, pamoja na Rais wa Nchi kulishughulikia tatizo na hata kuchukua hatua, kinachoogopesha ni uwepo wa nguvu za kumshinikiza Rais kuchukua hatua nyingine bila hata kuzingatia kuwa Rais kwenye nchi ni kielelezo cha Haki na Utu. Kwamba Rais wa Nchi kwenye kuyafanyia kazi yenye kuwahusu raia wake, hapaswi Kuonea wala Kupendelea.

Wakati Watanzania tukikaribia kuufunga mwaka tuna lazima ya kujiuliza; Je, nguvu za mashinikizo haya ni za ndani tu, au kuna zinazotoka nje? Na kama hilo la pili litakuwa na ukweli, tujiulize, je, wenye kushinikiza hayo ni wenye mapenzi mema na nchi yetu, au ni wenye kujali maslahi yao?

Ndio maana tunaona, kuwa kwenye hili la makampuni ya nishati ya Umeme, si IPTL tu, kuna wengine; Symbion, Agreko, Songas... . Hawa ni washindani kibiashara. Isije, ikawa ni ya ' Ugomvi wa Tembo'. Tunajua kinachoumia ni nini.

Ndugu zangu,

Hii ni Nchi Yetu. Katika yote tuyafanyao, tutangulize kwanza maslahi mapana ya nchi yetu. Maana, mengine tunayoyafanya, na kwa kutanguliza maslahi binafsi, yaweza kuwa mwanzo wa nchi kuparaganyika. Tunayaona kwa wengine.

Na tumuunge mkono Rais wetu aliye madarakani kwa ayafanyayo kwa maslahi ya nchi yetu.

Na kama Mwalimu alivyosema, nasi tuseme; " Tanzania Should Never Be ' Another Congo'.

Ni Neno La Leo.

Maggid,
Iringa.

http://mjengwablog.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye6T2wb4U6S%2BNZ8B8B3Eo5V3qU9P1vrPPDEpznbVhyz83g%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment