Tuesday, 30 December 2014

[wanabidii] Re: [Wanazuoni] Re: Swali juu ya Bima Ya Afya



2014-12-30 22:10 GMT+03:00 Atuwene Mbelle atuwene.mbelle@gmail.com [Wanazuoni] <Wanazuoni@yahoogroups.com>:
 

Ndugu wanazuoni,
Acha nitaje wachache hata kama si waajiriwa wa serikali labda mtanijibu (kaka Adamu, Chambi,  Haule,  Straton, Beda, Baraka, Walter, Chambua  Makakala, Salim, mchungaji Chagama,mh Zito) na majina yakinijia zaidi nitataja tuu na kama sijakutaja ndio zaidi nategemea uchangie.

Siku tatu zilizopita nilituma  mail hiyo hapo juu na sikujibiwa. Leo narudia tena na nitaendelea kurudia mpaka ntakapoelimishwa.

Hivi hili suala  la waajiriwa wa serikali kulazimishwa kujiunga na mfuko wa Bima ya afya hata kama tayari wamejiunga kupitia wenzi wao mnalionaje. Je kwa upande mmoja sio suala la kijinsia?

Yaani hii couple ya Kitanzania, iweke kadi mbili zinazofanana ndani ya nyumba  zote za bima hiyohiyo wakati  hizo elfu zaidi ya 50  za  ziada wanazokatwa kila mwezi si chini ya laki 6 kwa mwaka ambayo wangeweza kulipia ada ya mtoto au kufanya kitu kingine cha maendeleo.

dada Lilian, Gloria, Jacky,  Shakila,  Leila, Vicencia, Agness, Christine, mama Demere na wengine ambao safari hii sijawataja

mnalizungumziaje suala hili?

Atuwene
 




2014-12-27 20:15 GMT+03:00 Atuwene Mbelle <atuwene.mbelle@gmail.com>:
Ndugu wanazuoni,

Ni imani yangu kuwa jukwaa hili sasa ni moja ya sehemu unayokutana na watu wa Nyanja na fani mbalimbali.

Twende kwenye mada, naomba kueleweshwa na wahusika au wenye uelewa zaidi kuhusiana na suala Zima la BIMA YA AFYA YA TAIFA (NHIF).

Je ni kweli sheria inalazimisha kila Mtanzania ambaye ameajiriwa serikalini kujiunga  na NHIF?

Kama ni kweli wahusika wanaliangaliaje hili suala kwa upande wa Watanzania ambao ni mke na mume, na wote ni waajiriwa wa serikali, watoto wao ni wale wale kwa kuwalazimisha kuwa na kadi mbili za aina moja ndani ya nyumba na kukatwa mishahara miwili wakati kiukweli inayotumika ni kadi moja?

Ninasubiria kuelimishwa.

Atuwene




__._,_.___

Posted by: Atuwene Mbelle <atuwene.mbelle@gmail.com>
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (2)

.

__,_._,___



--

Yona Fares Maro

Institut d'études de sécurité - SA


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment