Monday, 29 December 2014

Re: [wanabidii] MAONI YANGU HURU JUU YA WAGOMBEA WANAOTAJWA TAJWA NDANI YA CCM

Mnamuandama membe kwa mahakama ya kadhi tu au kuna mengine, kama ni kwa mahakama ya kadhi hebu jaribuni kutueleza ubaya wa mahakama za kadhi kwa mifano na si kupayuka payuka tu.

Binafsi lowasa si mkubali hana ushawishi hata kidogo zaidi ya kutumia pesa, kama anaushawishi mbona kashindwa kuishawishi jamii yake ya kimasai kufuga ufugaji wa kisasa badala yake wanatuletea fuji kwa kuvamia mashamba yetu angali, kiteo,mvomero, kilosa na kwinginepo.

Wamasai wamekuwa kama lowasa kwa kutoa rushwa, wanalisha mifugo yao ktk mashamba ukuiwazuia wanakuua then wanatoa rushwa, sasa tukimchagua jamaa wao si ndio tutateseka kabisa sisi wakilima

On Dec 21, 2014 5:22 PM, "Emma Kaaya" <emmakaaya@gmail.com> wrote:

MAONI YANGU HURU JUU YA WAGOMBEA WANAOTAJWA TAJWA NDANI YA CCM

Ninajua maoni haya yatapata tafsiri nyingi.nawajibika binafsi na maoni haya.ni yangu. Nitaorodhesha kulingana na likeability na ninavyoona uzito wa mtu.

1.LOWASSA
Mgombea huyu ana nguvu za ajabu sana katika chama kwa ujumla na hata ana nguvu na watu wake tayari na kwa muda mrefu katika media, katika makanisa, katika misikiti, na katika makundi muhimu ya kijamii.
Kama hakutakuwa na maamuzi kama yaliyofanyika wakati wa JK kwenye vikao vya uteuzi basi Lowassa ndiye atakuwa rais ajaye.
Kashfa za richmond na mabaya yanayosemwa dhidi yake wala hayamuathiri vyovyote kama akipitishwa na vikao vya chama.
Lakini kwa maoni yangu na kwa mwenendo unavyokwenda CCM vikao vya chama kupitia saduku la kura hana mpinzani ndani ya ccm kizingiti ni kamati kuu CC, NEC na mkutano mkuu ni mteremko kwa lowassa.
Changamoto ya kiafya ni kama alivyozushiwa Prof Dr kikwete kuwa mgonjwa ili hali mwenye kujuwa afya ni yeye mwenye kwa msaada wa madaktari na Mungu wake leo anamaliza awamu yake salama salimin

2. MWIGULLU
Labda mnajua kuwa huyu bwana yeye mwenyewe hajatangaza nia moja kwa moja. Anafanya hivyo kupitia kwa watu wengine
Kwa hali ilivyo sasa kama Lowassa hatapitishwa kwa namna yoyote ile, mawazo yangu ni kuwa Mwigullu aweza kuwa rais wa nchi hii.
Tunaweza kubishana juu ya umri na uwezo wa uongozi, lakini Mwigullu anaonekana ana advantage kubwa sasa kuliko wengi.na ni rahisi kambi ya lowassa kuhamia kwake.

3. MEMBE
Nje ya msaada wa familia kuu hana uwezo wowote wa kuchaguliwa na vikao vya uteuzi.
Membe hakika akipitishwa na CCM kuna uwezekano mkubwa wa upinzani kushinda maana hata kadi yake ya chama amejiunga 2003 hana uzoefu vizuri na chama kama wataweka mgombea mzuri.
Membe ana mgogoro mkubwa na wakristo kwa sababu ya mambo yake ya kutetea OIC. Ila kwa unafiki wetu tutajifanya kubishia hili.Kwa majivuno ya membe ni ngumu kuungwa mkono ndani ya ccm ndo maana hadi majuzi wafuasi wake wameanza kumdisi kwa kasi ya ajabu sana sababu anaijua yeye na wafuasi hofu yao ni ngumu kumuuza kwa wajumbe habebeiki

4.MAGUFULI
najua kuwa magufuli hajatajwa popote wazi katika wanaojitokeza. Lakini huyu ndiye mtu ambaye anaweza kuwa na nguvu kubwa kwa wananchi. Ikiwa anafaa ama la hilo ni jambo jingine.
Nimewahi kumsikia Maguful ameshaanza kuwaita wafuasi wa lowasa jimboni kwake na kuwaambia ukweli wa kwamba hatagombea uraisi isipokuwa wamsaidie kutetea ubunge wake jimboni hizi ni dalili za maguful kumuunga mkono lowasa
Lakini kwa maoni yangu binafsi Magufuli hafai kwa urais anafaa uwaziri mkuu

5.KINANA
Mnaweza kusema mi chizi. Lakini mwisho wa orodha yenu tunzeni jina hilo. Sitafafanua kwa sasa.

WASSIRA, PINDA, NGELEJA,KIGWANGALLA, SITTA, MAKAMBA na CHENGE sihitaji hata kuhangaika kuandika chochote. Hawana nafasi yoyote.

Tukutane 01/01/2015 MONDULI KWENYE SHEREHE ZA KILA MWAKA TOKEA 1996 ZA 2BOYS MEN HAWAJAKUTANA BARABARANI
SIMAMA NA UHESABIWE

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment