Tuesday, 30 December 2014

Re: [wanabidii]

Na huyu katoka wapi?
em

Sent from my iPhone

> On Dec 29, 2014, at 4:34 PM, "'Muhammedkhatib' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> FALAKI
> (Dkt. Muhmmed Seif Khatib)
>
> Ulimwengu ni vitu vyote vilimo ndani ya dunia na nje ya dunia.Miongoni mwa vitu vilivyoumba ulimwengu ni sayari - umbile lilioko angani na kuelea ambalo
> huzunguka jua.Dunia yetu ni moja kati ya sayari zieleazo angani bila kuanguka au
> kugongana.Ulimwengu ni pamoja na nyota ionekanayo kama mpira ambayo ni gesi
> inayoungua na kutoa mwanga usiku.Lipo jua ambalo ni nyota itoayo mwangaza
> mchana na kuipa joto dunia.Upo mwezi kitu kinachong'ara na kutoa mwangaza usiku.
> Mwezi huizunguka dunia kwa siku ishirini na nane.Vitu vyote ikiwemo majini,mashetani,binadamu,wanyama,wadudu,viumbe vya bahari,miti,mimea na vyengine ambavyo tujuavyo na tusivyovijua kwa ujmla wake ndiyo ulimwengu.Mwanadmu ni kiumbe
> mwenye maarifa na ujuzi.Anatambuwa uwepo wa ulimwengu,wakaazi wake na yeye
> ndiye mmiliki wa yote.Moja ya taaluma na maarifa yahusuyo misimu na namna nyota
> zinavyochukua maumbo mbalimbali na maana yake huitwa falaki. Mienendo hiyo ya nyota na sayari wapo wanaoamini na kuhuhusisha na matokeo mbalimbali ya mwanadamu.
> Mwaka wenye miezi kumi na mbili unafikia ukingoni.Katika mwaka uliopita matukio
> mengi yametokea na kuathiri minenendo ya watu.Katika uwanja wa siasa vifo kadha
> wa kadha. vimetokea.Msemo kufa kufaana ulijiri.Madiwani kama binadamu walipoteza maisha
> kwa mfulilizo wa vifo.Chaguzi katika awamu mbili ulitokea.'Chopper' tatu
> na viti vitatu vilivyodonolewa na chama cha upinzani huku chama tawala kujizolea
> kwa mzo.Awamu ya pili uchaguzi wa madiwani waliofanyika.Wenye 'Chopper',
> nao waliporomoka na wa Chama cha Mapinduzi kikapaa.
> Chaguzi maalum za katika majimbo katika awamu mbili zikendeshwa.Wenye 'Chopper'
> wakapaa lakini hawakufika katika eneo la Wingu litakiwalo.Kama kawaida chama
> cha CCM kikafanya kazi na kuzoa viti vingi vya ubunge.Genge la vyma vya siasa
> vya upinzani vikasarambatika huku wakabaki hawaamini yaliyojiri.Ni kama kawaida
> yao hawakuacha kulalamika.Kwa yale maeneo machache walioshinda uchaguzi
> ulikuwa huru na haki. Maeneo waliyogaragazwa uchaguzi umechakachuliwa.
>
> Bunge la Katiba likachukua nafasi yake.Mijadala mizito ikaibuka tokea ya Hati
> ya Muungano kuwa haipo hata kufika kuumbuliwa kwa waasisi wa Taifa letu
> Nyerere na Karume.Kura ya siri na dhahiri ikaleta kichfuchefu. Mwisho muundo
> wa serekali mbili na tatu ukalipasua bunge.Kambi ya vyama vinne tu vya upinzani
> ikaachia ngazi ya bunge wakabaki kipiga makelele kupitia madirishani,katika majukwa,
> makongamano na warsha.Safari ya kuisaka Katiba inayopendekezwa ikapamba
> moto. Msituko ukatokea pale kura za Zanzibar na Bara zikaikubali katiba inayopendekezwa.Wapinzani walioko nje ya bunge wakashuka mabega na Chkupwelewa..Ndani ya bunge chama cha CCM na makundi mengine wakaongoza.Katiba
> inopendekezwa inasubiri Kura ya Maoni mwezi April mwakani.Kugua kwa vidole kwa
> vyama vya upinzani katika siasa havikuacha kulumbana na CCM.
> Uchaguzi wa
> Serekali za Mitaa,vijiji na vitongoji vikahitimisha safari ya mwaka mzima ya
> la upinzani kuingia katika korongo.Zipo sehemu wameendeshwa mrisi! Zipo
> sehemu wamekwenda kapa!Kedi na viburi vyao vimekwisha.Bakora za ushindi
>
> zimewachapa wapinzani kila mahali.Bado wanaendelea kulia kwa kwikwi na kite!Kwakutumia taaluma ya falaki wajiulize kwa nini wamdoda kwa kila tukio kwa mwakahuu unaokwisha?Chaguzi za madiwani wamegaragazwa.Chaguzi za wabunge wamekula mtama.
> Katiba inopendekezwa wameachwa solemba! Uchaguzi wa serekali za mitaa,
> vijiji na vitongoji wapo katika chumba cha wagonjwa mahututiz!
> Kwa kuwa mwaka
> unakwishwa tufumbe macho.Tuinuwe mikono yetu juu kuwaombea duwa na sala
> wapinzani, ' Mungu uwajaaliye kwa mwaka mpya wa 2015 uwe na nuhusi kwao.Wanguke katika kila uchaguzi.Kila wanalolitaka wasilipate.Mungu uwajaaliye wawe wanagombana
> na kipigana wenyewe kwa wenyewe - AMIN'
>
>
>
>
>
> Sent from my iPad
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment