Saturday, 22 February 2014

Re: [wanabidii] URAIS 2015 - JANUARY YUSUF MAKAMBA

Yona na wengine,

Kama alivyosema Nico, January kama raia w anchi hii anaweza kugombea uras hivyo huenda naye anautaka. Na hadi afikie maamuzi au mawazo hayo, lazima kuna vitu kadhaa ametizama yeye kama mtu binafsi na wale ambao huenda wanamshauri na kuona anaweza kujitosa. Ila natofautiana na mawazo ya Nico na Ngulupa katika hoja kuu ya email yako.

Bila kutoa maoni yangu kuhusu kufaa au kutokufaa kwake, ninaona kuna tatizo tunapohukumu watu kama hawa pale tunapokua na definitions zetu au per-conceived ideas/perception za nini chatakiwa kwa mtu kustahili kuwa kiongozi wa nchi.  Nimeona watu kadhaa wanapozungumzia watu aina ya January, wanaishia kuhukumu uzoefu, umri, na mafanikio au mabadiliko ambayo kayaleta hadi sasa. Sina hakika kama huu ni mtazamo sahihi sana maana kama ndio msingi wa kupata viongozi, basi tusingekua na kiongozi katika ngazi yeyote ile.

Labda tujiulize maswali; vijana kama akina Nassari Mbunge wa Arumeru, Mnyika wa Ubungo, Lusinde wa Mtera, Mwigulu wa Iramba, Zitto wa Kigoma North na wengine wengi walikua wana uzoefu gani au walikuwa wamefanikiwa nini hadi kupewa nafasi zile za uongozi? Nani aliwajua vema kabla ya nafasi walizonazo? Je baadhi ya vijana hawa hawafanyi kazi nzuri kuliko maprofesa na veterani wengine wanaozeekea kule bungeni? Viongozi kama DJ aliyekua rais wa Madagasca walikuwa wana uzoefu gani au wamefanikisha nini hadi watu wakawaamini kuwapa uongozi? Cameroon na Obama walikua wamefanya nini cha tofauti kama watu binafsi kabla ya kufikia ofisi walizoshika sasa? Kijana Malema wa SA ambaye anawaumiza kichwa akina JZ sasa ana nini chakuonesha kama mafanikio?

Pili, tunapohukumu watu kwa perfomance yao kama sehemu ya mchakato wa kuwaamini kuwa viongozi wetu, tujipe pia nafasi ya kujiuliza je walipokua wanalikua na mwanya kiasi gani wa kufanya mambo na kuonesha mabadiliko yenye ushawishi kwa kiasi tunachotaka kuona? Kwa mfano, nadhani nafasi aliyonayo January kwa sasa kama naibu waziri, kwa mfumo wa utendaji wa wizara ulioko, sioni ukimpa sana nafasi ya yeye kuonesha utendaji wake na mafanikio ya kiuongozi. Binafsi ninaona alipokua mbunge pekee, tuliweza kuuona utu wake, uwezo wake, nia yake na maono yake kuliko ilivyo sasa. Nakumbuka alivyokua anaongoza kamati ya Nishati na madini; nakumbuka alivyosimama bungeni bial uchama sana akiwa na hoja za makazi na issue nzima ya mortgaging na ajira kwa vijana kuliko ilivyo sasa. Labda tungekwenda pia kwa watu wa Bumbuli tuwaulize je mbunge wao ambaye ni kama mjukuu kwa mbunge aliuyemtangulia, kawasaidia nini na kafanya nini kama kiongozi kubadilisha maisha yao?

Point yangu ya msingi ni kuwa, huwezi kupima mafanikio ya kiuongozi bila kupema nafasi, mamlaka na mahali pa kuonesha uwezo wako. Nadhani kuna mambo ya msingi zaidi ya kuyatizama katika kumuaminisha mtu uongozi wa nchi yetu katika ngazi yeyote ile ambayo yana nguvu kuliko umri, uzoefu, na mafanikio ambayo keshayapata kama kiongozi. Kwa kusema hivi, simaanishi napuuza nguvu na nafasi ya uzoefu katika uongozi.

Jambo hili la kujikita kuwapa watu nafasi za uongozi kwa vile tu wana sifa ambazo sisi tumeziona kuwa ndio msingi wa uwezo wao lina athari kubwa sana kwenye nchi yetu.
  1. Kwanza, limewafanya watu wengi sana wenye nia njema na mawazo mazuri kabisa ambayo huenda yangebadili hali iliyoko, kuogopa sana kuingia kwenye siasa au uongozi wa ushindani, wakiogopa kuambiwa waoneshe hizo sifa na wasiwe nazo au zisiwe dhahiri kama ilivyotegemewa. Imewafanya wale waliotangulia hata kama ni kwa kubebwa ndio wabaki kwenye mfumo kwa sababu tu wao wanajulika
  2. Pili, limezuia mawazo mapya na changamoto mpya ambazo ni mzingi sana katika kuleta mabadiliko ya kweli
  3. Tayu, limefanya uongozi uwe wa kujuana zaidi na wanaojulikana ndio wanaobaki kwenye uongozi hata bula tija
  4. Nne, tumebaki kukumbatia wazee au majina fulani kwa miaka nenda rudi huku tukiwa na malalamiko na maumivu yaleyale
  5. Tano, imechangia sana kujenga taifa la watu waoga kuleta mabadiliko...waoga kufanya kitu cha tofauti na mazoea yetu. Sio tu vijana kama akina Makamba na wengine wanaogopwa kupewa nafasi kwenye vyama vyao kwa kuwa eti hawana uzoefu, bali hili limechangia sana hata katika kuogopa kukubali vyama pinzani kuwa vinaweza kubadilisha hali iliyoko...huku tukilemewa na msemo wa zimwi likujualo halikukuli likakwishwa (sikumbuki vema maneno halisi)

Nirudie tu kusema kuwa, tuna vigezo vingi vingine vya msingi ambavyo twaweza kuvitumia kuhukumu aina ya watu wanaotaka kutuongoza zaidi ya uzoefu, umri, na mafanikio ambayo mwombaji keshayapa kabla ya nafasi anayoitaka sasa.

Nitarudi nikipata upenyo

MM

2014-02-22 18:21 GMT+03:00 Nico Eatlawe <eatlawe@yahoo.com>:
Yona na wengine,
 
Kugombea nafasi yoyote ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania maadam anavyo vigezo vinavyotakiwa. Kwa msingi huo, mimi sioni tatizo kwa Makamba kugombea urais. Wasi wasi wangu tu kuwa anaweza kuwa anatamani ikulu kwa vile alikuwa karibu na JK bila kujua ugumu wa hiyo nafasi yaani kuongoza zaidi ya milioni 43. Inahitaji uzoevu na ukomavu wa namna fulani mtu kuongoza. Siyo kuwa na digrii au kuwa mbunge inamtosheleza mtu kugombea urais maana siyo kila anayepata ubunge ni kiongozi kweli maana tunaona wengi ni wafuasi tu wala hawana ushawishi wala ajenda yoyote zaidi ya maslahi yao binafsi.
 
Pengine tuangalie kazi yake hadi leo. Ana ushawishi gani? Ameleta kipya gani? Tunaona vijana akina Zitto wakijaribu kufanya vitu hata kama wanaonekana wana udhaifu. Udhaifu ni ubinadamu ila kazi anafanya. Kwa upande wa CCM mimi sijaona kijana mwenye ushawishi na maono ukiacha wazee wenye uzoevu.

On Saturday, 22 February 2014, 12:20, Yona Fares Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
Ndugu zangu ,

Huyu kijana mwenzetu ameonyesha nia ya Kuutaka urais wa Tanzania , kuthibitisha hilo amehojiwa na kamati kuu ya CCM na akapewa adhabu ya miezi 12 .

Je kuna lolote la kujadili kuhusu Mhe January Makamba ? Au tumwache tu kwa sababu hatumjui na hatutaki kumjua zaidi ?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment