Saturday 22 February 2014

Re: [wanabidii] URAIS 2015 - JANUARY YUSUF MAKAMBA

Yona na wengine,
 
Kugombea nafasi yoyote ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania maadam anavyo vigezo vinavyotakiwa. Kwa msingi huo, mimi sioni tatizo kwa Makamba kugombea urais. Wasi wasi wangu tu kuwa anaweza kuwa anatamani ikulu kwa vile alikuwa karibu na JK bila kujua ugumu wa hiyo nafasi yaani kuongoza zaidi ya milioni 43. Inahitaji uzoevu na ukomavu wa namna fulani mtu kuongoza. Siyo kuwa na digrii au kuwa mbunge inamtosheleza mtu kugombea urais maana siyo kila anayepata ubunge ni kiongozi kweli maana tunaona wengi ni wafuasi tu wala hawana ushawishi wala ajenda yoyote zaidi ya maslahi yao binafsi.
 
Pengine tuangalie kazi yake hadi leo. Ana ushawishi gani? Ameleta kipya gani? Tunaona vijana akina Zitto wakijaribu kufanya vitu hata kama wanaonekana wana udhaifu. Udhaifu ni ubinadamu ila kazi anafanya. Kwa upande wa CCM mimi sijaona kijana mwenye ushawishi na maono ukiacha wazee wenye uzoevu.


On Saturday, 22 February 2014, 12:20, Yona Fares Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
Ndugu zangu ,

Huyu kijana mwenzetu ameonyesha nia ya Kuutaka urais wa Tanzania , kuthibitisha hilo amehojiwa na kamati kuu ya CCM na akapewa adhabu ya miezi 12 .

Je kuna lolote la kujadili kuhusu Mhe January Makamba ? Au tumwache tu kwa sababu hatumjui na hatutaki kumjua zaidi ?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment