Friday, 21 February 2014

Re: [wanabidii] POSHO SH 300,000 KWA SIKU HAITOSHI!

Kumbe hakukuwa na haja ya kuwa na bunge la katiba kwani hawapo kule kuwakilisha maoni ya wanainchi-wamefuata pesa. Kama wanaweza kuanza kukaa nje wagombea wanajadiliwa na kujieleza-wapo nje mpaka mwenyekiti anaita waingie ndani kupigia kura waliogombea uenyekiti wa muda wa bunge hilo na wasiohudhuria hawatapewa posho-hakuna haja ya kulisema hata bunge la kawaida kuwa wengine hawahudhurii, tunaona viti vyeupe ktk TV. Nao wanafanya hivyo hivyo, na kuanzisha vurugu kukataa posho!! Kuna tofauti gani na wanaokataa mashine za TRA kulipa kodi na hawa wanaopewa mihela 21 milion kwa siku 70 wanataka zifike 50 milioni? Lodging gharama at most 40-50,000/= kwa siku, wanakula na kunywa kikaoni, kulala tu na mlo wa jioni? kukaa na kuongea ndio wapewe mshahara wa mwezi wa mtu ambaye anapata 300,000/= Masters degree, anapanga, ana familia, nauli ya bus na ajiwekee bima ya afya na makato mengineyo? Hawa watawakilisha maoni/mawazo ya watanzania kweli? Mungu atusamehe-mwanzo mbaya, Nyni haoni kundule.

 



On Thursday, 20 February 2014, 21:19, Sylvanus Kessy <frkessy@yahoo.com> wrote:
Ama kweli, ule usemi usemwao, mkuki kwa nguruwe.... umetimia. Ni kilio cha muda mrefu kwa watanzania kima cha chini cha mshahara walao kiwe sh. 300,000 kwa mwezi. Inakataliwa na inasemwa haiwezekani.

Kumbe jamaa zetu wenye rungu hilo wanasema 300,000 kwa siku haiwezekani. Je na yule anayepata 150,000 kwa mwezi, mwenye mahitaji kama wewe. Ana familia, anakula, anavaa, anajenga, anasomesha, anaumwa, anasafiri, ana ndg wanaomtegemea. Wengine wameachiwa watoto Yatima au wajane WASEME NIN? 

FIKIRI NA MCHUKUE HATUA!
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment