Ludo, unachosema ni kweli kabisa lakini tusiangalie wa dada wa majumbani tu, tuangalie mfumo mzima wa ajira za vijana watanzania.
Kuna wavulana wadogo wanafanyishwa kazi za kusugua miguu ya akina mama salon, nenda mitaa ya makoroboi hapo mwanza uone rundo la wavulana wakisugua miguu ya akina mama tena bila gloves wala kutumia antiseptic.
Nenda vituo vya mabasi watoto wanauza karanga machungwa na biscuit na soda, tizama vijana wanaokokota baiskeli za azam.
Hii biashara ya kuwakopesha vijana bodaboda ndo nayo imeshika kasi, vijana usiku kucha wanakimbiza machangudoa kutoka bar moja hadi nyingine.
Tizama matokeo ya fom fo, watoto kumi bora saba ni wasichana tofauti na miaka ya nyuma tulizoea wavulana kuongoza, hii inaonyesha wavulana uwezo wao kimasomo unapungua kwa kasi ya kutisha,
----------
Sent from my Nokia phone
------Original message------
From: Joseph Ludovick <josephludovick@gmail.com>
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, February 21, 2014 9:20:47 AM GMT-0800
Subject: Re: [wanabidii] DADA WA KAZI ZA NYUMBANI SI NDUGU YAKO
Nilifikiri hatimaye utapinga ajira hizi za watoto.haukufika huko.hata hivyo
hoja yako murua na changamoto pevu.hat a wapigania haki wanawanyanyasa hawa
Dada zetu.hongera Kaaya,nakuunga mkono.nasubiri wanafiki watakavyojitokeza
hapa wakati wakiwatesa binti za watu majumbani kwao!
On Feb 21, 2014 3:07 PM, "Emma Kaaya" <emmakaaya@gmail.com> wrote:
> Naamini hakuna asiyefahamu ugumu wa kazi za ndani.Kinamama hapa najua
> mnanielewa zaidi.Kazi za ndani ni nyingi na kwa kawaida haziishi,ila
> tunaweka kikomo cha kiasi Fulani.
>
> Mabinti wa kazi au wasaidizi wa kazi za ndani wamekua watu muhimu sana
> kwenye familia za watanzania wengi.Uasilia wa hali ya maisha unaowalazimu
> wazazi kutokuwepo nyumbani muda mwingi wakitafuta kipato na hivyo kukosa
> muda wa kufanya kazi za ndani,umeongeza uhitaji wa mabinti hawa.
>
> Mabinti wa kazi za ndani hufanya kazi nyingi na kubeba majukumu mengi ya
> kifamilia:kupika,kuosha vyombo,usafi,kufua na kunyoosha,kulea watoto na
> vichanga,na shuguli zingine zote za nyumbani(wajua msichana wako unampa
> kazi gani).
>
> Pamoja na haya,mabinti hawa udharauliwa na hudhalilishwa na waajiri wao.
> Ni familia chache sana ambazo utakuta dada wa kazi
> anaheshimika,anathaminiwa na kupendwa.
>
> Leo NAVUNJA JUNGU,naweka mwiko pembeni navaa joho langu la sheria.Nasema
> nawe Baba na Mama msiowaheshimu wala kuwathamini Mabinti wa kazi.
>
> Binti wa kazi ni muajiriwa
>
> Kwanza kabisa,ieleweke kwenu kwamba msichana wa kazi si ndugu yako,bali ni
> muajiriwa kazini.wewe ni muajiri na nyumbani kwako ndiyo kazini
> kwake.Anahaki zote za msingi za mfanyakazi.
>
> Anahaki ya kulipwa ujira wake katika muda sahihi
> Anahaki ya likizo
> Anahaki ya siku moja ya mapumziko kwa wiki
> Anahaki ya kupumzika(kama mnavyopumzika saa moja la lunch makazini)
> Ana haki ya masaa kamili ya kazi (kama mfanyakazi mwingine yeyote)
> Anasiku za ziada anazoweza tumia kwa ugonjwa au matatizo yake mengine
> binafsi
> Asilimia kubwa ya mabinti wa kazi hawapati haki hizi,waajiri mmekua si
> wema hata kidogo,mnawaonea na kuwanyonya sana.
>
> Unyanyasaji,udhalilishaji na unyonyaji
>
> Waajiri wengi mnawanyanyasa na kuwadhalilisha mabinti hawa kwa kuwatukana
> matusi machafu,kuwasema vibaya na mbaya zaidi bila hata kuona haya
> mnawapiga wanapokosea.Kinababa nanyi hamuishi kuwanyanyasa mabinti hawa
> kijinsia.Wengi wenu mmewageuza mabinti hawa kua watumwa.
>
> Binti anaamka saa kumi na moja asubuhi ,analala saa tano usiku.Anafanya
> kazi usiku na mchana, asafishe nyumba,afue nguo za familia,apike chakula
> cha familia na alee kichanga,bado mama na baba mkirudi mnamgombeza na
> kumtukana pale alipokosea. Akivunja chombo kwa bahati mbaya unamlipisha kwa
> kumkata mshahara,watoto wako wasiokua na adabu nao wanamuamrisha na
> kumtukana binti huyu. Mambo ya aibu haya.
>
> Mbaya zaidi hamjali hata usafi na muonekano wa mabinti hawa,mtoto wa kike
> anamahitaji mengi sana,na hakuna binti asiyetaka kupendeza.lakini hata nguo
> nzuri tu hamuwanunulii.Hata marashi yakuondoa harufu ya kwapa
> humuwanunulii,mbona nyinyi makazini mnapewa bonus?.Cha kushangaza mnataka
> binti huyo ahakikishe watoto ni wasafi na wanapendeza wakati
> wote.Inawezekana kweli?
>
> Wengine mnawanyima mabinti hawa chakula au laa,mnawapa chakula tofauti
> nakile familia yako inachokula.Cha ajabu ni binti huyu huyu mwenye jukumu
> la kuiandalia familia yako chakula,na tena unataka apike vizuri na
> ahakikishe watoto wamekula vizuri.
>
> Ukweli wa mambo
>
> Mabinti hawa wamekua na sifa mbaya miaka hii ya karibuni,lakini ki ukweli
> si mabinti wote wabaya.Matendo na tabi zisizopendeza za waajiri
> huchangia kuwajengea mabinti hawa tabia na sifa mbaya walizonazo.
>
> Ivi unawezaje kumdharau,kumdhalilisha,na kutompenda binti ambae unamuachia
> watoto wako,nyumba yako,na majukumu ya kuipikia familia?Upendo,heshima na
> kuthaminiwa ni jambo ambalo kila mwanadamu analipenda na anataka
> afanyiwe.Unapomuonyesha mtu chuki,kutokumthamini na kumdhara basi hata yeye
> hana sababu yakukufanyia mema.
>
> Unalotakiwa kujua
>
> Itambulike kwenu leo kwamba mabinti hawa si watoto wenu, wala ndugu zenu.
> Ni watu walioko kazini, Kama wewe ulivyokazini huko uliojiriwa. Huna haki
> yakumchagulia maisha, wala kumfanyia maamuzi. Wengi mmewageuza mabinti hawa
> kua watoto wenu na kuwachagulia maisha, mnawalazimisha kusali dini zenu,
> mnawalazimisha kushiriki mambo yenu ya kifamilia na hata kuwapeleka likizo
> vijijini kwenu. Hawa mabinti wanafamilia zao, wana kwao, wanamaisha
> wanayotaka kuishi, hawatakaa majumbani kwenu siku zote. Ni vyema na haki
> kuwashauri na kuwapa miongozo bora ya kimaisha kama walezi, lakini si
> kuwachagulia maisha.
>
> Badilika
>
> Ifike mahala mbadilike,muwe watu wenye utu. Mjifunze kuishi na mabinti
> hawa kwa upendo ili nao wawapende na kuwapenda watoto wenu. Muwape haki zao
> kama wafanyakazi na zile za kibinadamu pia.Mabinti hawa ni binadamu kama
> wewe na Wanaitaji kupumzika na kupata muda binafsi.
>
> Binti wa kazi ni msaidizi wako nyumbani,zingatia neno "msaidizi". Wewe
> muajiri ambae ndio mwenye familia unanafasi yako ya yale unayotakiwa
> kufanya, na hata watoto wako wananafasi yao katika kazi za nyumbani.Binti
> wa kazi hawezi kufanya kila kitu.Kama wewe mwenyewe umeshindwa kufanya yote
> peke yako ndiyo maana umemuajiri,unadhani yeye ataweza kufanya yote?
>
> Mbadilike, wewe muajiri shika nafasi yako,na watoto wako washike nafasi
> yao ili utendaji kazi wa binti wa kazi uwe mzuri.Msipowashirikisha watoto
> wenu kwenye kazi za nyumbani watajifunzaje? Mwisho wasiku watatia aibu na
> wataona maisha ni magumu.
>
> Heshima zangu kwa waajiri wanaoishi vizuri wa mabinti hawa, na pongezi
> kubwa sana kwa wale ambao wamewaendeleza, wamewasomesha na hata kuwaoza
> mabinti wao wa kazi,Ni mifano ya kuigwa.huu ndio utu.
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment