Utumwa wetu ni wa akili. Nimekutana na wazungu wengi nchini na nje wasiojua kiingereza vizuri. Anakazana kuhakikisha umeelewa anachomaanisha. Kama kiingereza unachojua kinatosha kumuelewesha mtu unachomaanisha inatosha labda kama unafanya mtihani. Nasikiaga watu wanajitahidi hata kubadili 'tone' wakifikir huko ndiko kujua kiingereza. Msikilize Askofu Kilaini akiongea Kiingereza. Gramatically correct. Lakini kila mtu atajua mhaya huyu. Mkutano kama huo wa Obama ya nini kama hutaeleweka kujisumbua kuongea kiingereza? Wakalimani wafanye nini? Haikustahili kuwa sababu ya lugha waandishi wetu kukosa kuulizwa. Kama ni kunyimwa nafasi ya kuuliza kwa sababu ya itikadi, CIA itakuwa ilimwambia Obama jambo hilo na atakuwa alitudharau. Kwake kumsikiliza mpinzani ni afya.
--- On Thu, 7/4/13, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> Subject: [wanabidii] ZIARA YA OBAMA - YAWAHUSU WAANDISHI WA HABARI To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> Date: Thursday, July 4, 2013, 1:59 AM
Kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii, watu wamekuwa wakiwakashifu sana waandishi wa habari wa Tanzania eti "Kwa kushindwa kuuliza maswali mazuri" kwenye mkutano wa marais Obama na Kikwete. Ukweli ni kwamba, waandishi wa Tanzania hawakupewa fursa ya kuuliza. Mchagua waulizaji (pengine ndiye aliyepanga maswali pia !) hakutoa fursa kwa waandishi ambao pengine wangeuliza maswali magumu. Kulikuwa na nafasi ya maswali mawili na waulizaji waliteuliwa na Msemaji wa Ikulu ya Tanzania..... Mlitaraji nini kutoka kwa Wana Habari wa Tanzania kwenye mazingira hayo? Halafu kuna suala la Kiingereza, kwamba waandishi wa Tanzania hawajui lugha hiyo na hivyo hawafai. Tunapimana sana uzuri au ubaya wetu kwa kuangalia ni nani anazungumza Kiingereza kizuri. Tatizo ni kwamba hatujawahi kuchekana kwa kuzungumza BROKEN CHINESE wakati sote tunajua kuwa miaka 20 ijayo, CHINESE inaweza kuwa lugha muhimu ya mawasiliano kuliko hata hiki Kiingereza tunachojisifia kwa sasa. Labda kwa sababu mimi sijui Kiingereza lakini kuna sababu gani ya kuchekana au kudharauliana kwa sababu ya kuongea kiingereza kibovu? Nafananisha tabia hii na ile ya wakati wa utumwa ambapo mtumwa aliyepangiwa kazi ndani ya nyumba (domestic slave) alijiona bora kuliko yule wa nje. Kama ujumbe umefika, ya nini kuchekana? -- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
|
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment