Manyerere, Hilda,
Ahsanteni kwa michango yenu murua. Tatizo ninaloliona ni michango hii kuwa ya jumla sana, na kama vile inawalaumu watanzania wote kwa ujumla kuwa tumesababisha hali hii tuliyo nayo leo hii.
Hili mimi sikubaliani nalo. Kuna watanzania wenzetu wanabidi kulaumiwa kuliko watanzania wengine.
Viongozi ni "Role Models". Watu wa kawaida wanawaangalia viongozi kutoa mwelekeo wa Taifa au dira. Leo tunaongozwa bila kujua dira ni ipi. Elimu haijulikani tunasoma ili kama taifa tufanye nini. Tutafanya nini kama elimu imeachwa iwe shaghalabagala. Wanaotakiwa kusimamia elimu ya umma, wanamiliki elimu binafsi. Hakuna mitaala. Wote tunasikia kila siku shule za "watakatifu", baadhi zina eti silabasi ya "cambridge, mara Afrika ya Kusini, mara Kenya, mara London, wendawazimu mtupu.
Vyuo vya Kilimo, kilikuwepo kimoja kule kwetu Maruku, na vingine vyote vimekufa. Vyuo vya mifugo, ufundi kadhalika. Hakuna anayejali.
Tazama viongozi wetu wanavyojadili bajeti kuhusu masuala nyeti "kihuni kihuni".
Lipo hili la mikataba mibovu. Watu wanaojua wanapohoji baadhi ya mikataba, au kuomba kuiangalia ili kuitolea viingizi (inputs) kwa nia ya kuiboresha, wanabezwa. Mahali pengine hatuambiwi ukweli, lakini kilio huja kutuumbua. Kwa mfano, alipokuja Rais wa Chuina, aliingia mikataba 17. Yaliyomo au ina=husu nini, hatujui. Rais wa Marekani ametoka hapa. Power Africa, inayosemwa kusambaza umeme katika nchi 6 za Afrika, hatujui utasambaa vipi ikiwa kwenye uzinduzi, Marais/wawakilishi wao hawakuwepo hapa?
Mambo ni mengi. Hivi mbona tunasoma wakubwa waliojigawia vilivyokuwa viwanda vya umma ambao baadhi wamesheheni Bungeni na kwenye Taasisi nyingine "nyeti"? Hawa wamewatupa watanzania wengi mtaani, kwa sababu hata hivyo viwanda hawakuvilipia, angalau ingepatikana hela ya kulipa hata "terminal benefits". Watanzania hawa wamefuatilia mafao, wamekufa, wattoto wao wamefuatilia, nao wamekufa, ad infinitum.
Wanafunzi ambao wanafundishwa kwa amri ya mahakama, hawapati elimu bora, kwa hiyo hawawezi kuzalisha. Wanajipooza kwenye vijiwe. Hawa ndio tunawalaumu. Ukikaribia uchaguzi, tunawatetea na kuwaruhusu kutundika bendera za vyama vyetu. Uchaguzi ukiisha tunaanza kuwabeza, na kuwaswaga kama mifugo, toka sehemu moja hadi nyingine. Sisi hatutaki kuhamia Dodoma tulikojiamulia.
Kwa ufupi, kutandaza lawama za jumla ni unafiki, ambalo nalo ni jinamizi kubwa, linalotuhusisha sisi wasomi tuliotekwa(elite capture). Tunashindwa kutumia elimu na taaluma zetu kuleta mabadiliko, tunajipendekeza kuona kama wakubwa wanaweza "kutuona".
Watanzania tuko kama tulivyo kwa sababu viongozi wetu hawako kama wanavyopashwa kuwa. Wanapoacha kwa makusudi kukusanya kodi, kusamehe wahahlifu na udhaifu mwingine kama huo, mimi ninahusika vipi?
Mwisho, niseme kuwa Tanzania hakuna "wealthy people" anaowataja Hilda. Kuna "rich people". Tabia moja inayowatofautisha watu hawa ni kwamba wealthy people ni wale wenye kuwekeza katika mitaji na kupata utajiri kupitia uwekezaji huo. Na hii huchukua muda mrefu. Mpaka 1991, kwa sababu ya Azimio la Arusha, wote tulikuwa hatuna kitu. Wenzetu wametajirika vipi haraka haraka?
Tumewahi kujiuliza, inakuwa vipi kwa matajiri wetu kutoa michango kwenye kila shughuli ya kijamii wakiwa wamebeba hela kwenye rambo?
Tuhoji hayo na yushirikiane kutatua matatizo yetu.
MJL --
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment