Wednesday 13 March 2013

[wanabidii] Kama wewe ni MUOGA acha Siasa - Mhe. Mbowe

...If you're a fearful get out of politics... Hii ni moja ya kauli ambayo nimeikubali sana kwa kuwa si tu imetamkwa na Mhe. Mbowe kwa kuwa ni mwenyekiti - CHADEMA (T) na mkuu wa kambi rasmi ya Upinzani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bali imetamkwa na mtu ambae ni kiongozi, na kama kiongozi anatakiwa kuwa jasiri kusonga mbele kukipeleka chama chake pale ambapo sera na itikadi za chama chake zinataka.

Kwa wasomaji wa biblia nakumbuka moja ya kauli ambayo Joshua aliambiwa na Mungu baada ya Musa kufariri... Be strong and of a good courage, fear not, nor be afraid of them... Josh 1:9

Uwoga wa kufanya kitu kwa kuwa watu wengine hawataki (au watakuonaje/watajisikia vibaya) si tu haufai katika medani za siasa bali hata katika ulimwengu wowote wa kuisaidia jamii ambayo kiongozi anaiongoza iweze kusonga mbele. 
Ni namna gani tutapata viongozi wenye kuwahamasisha wafuasi wao wajiamini kufanya yale wanayotakiwa kufanya maadamu yamo katika misingi ya sheria na yanalenga kuwasaidia walio wengi.

Swali? Je katika serikali iliyopo tuna viongozi wenye ujasiri wa kutenda mambo bila woga? Au tuna viongozi ambao kufanya maamuzi ni mpaka atazame wengine machoni wana-mwangaliaje?
Tunahitaji viongozi wenye ujasirika katika siasa, jamii na sekta zote ambazo zina lengo la kumhudumia Mtazania
Naomba kuwashirikisha namba ambavyo kauli hiyo imenivutia.
Wasalaam 
 
Fred 
MATURITY does not come with age, it begins with acceptance of Responsibility
Change is Essence to maturation 

0 comments:

Post a Comment