Saturday 9 March 2013

[wanabidii] CCM YALAANI KUTEKWA NA KUTESWA KWA ABSALOM KIBANDA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kuvamiwa,
kupigwa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) na
Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ndugu Absalom Kibanda usiku wa
kuamkia Jumatano Machi 6, 2013.

Chama Cha Mapinduzi kinalaani kwa nguvu zote kilichotokea kwa Absalom
Kibanda, kwani ni unyama usiokubalika hata kidogo, unafaa kulaaniwa na
Watanzania wote.

CCM tunaitaka Serikali kuhakikisha inawapata waliofanya unyama huo na
kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake,
na kukomesha matukio ya namna hiyo.

Aidha, Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa Uongozi wa Jukwaa la
Wahariri, Afisa Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006, familia ya Ndugu
Kibanda, wanahabari na wadau wote wa habari nchini, na tunamwombea kwa
Mwenyezi Mungu apone haraka na kurejea katika kazi zake za Ujenzi wa
Taifa.


Imetolewa na:

Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UEENEZI
08/03/2013

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment