Monday 10 December 2012

[wanabidii] RE. UNAAMINI KATIKA USAWA WA KIJINSIA?


Hata kama unaamini, usikoroganishe mambo. Ukaufanya usawa sasa uwe sababu ya kukimbia majukumu yako na kuwa na utovu wa nidhamu na maadili. usawa wa kupata ajira na kulipwa mshahara sawa (tulipopata uhuru TZ ilizishinda nchi nyingi za Ulaya ambako wanawake hulipwa mshahara mdogo kuliko wanaume wenye elimu na ujuzi sawa nao); usawa ktk kumiliki na kurithi mali (matrilineal societies) warithio kwa mama wamejaribu. Baba na dada zake, kaka na dada zake kupata mgao wa ardhi na mali nyingine sawa. Ila, sehemu nyingine, utafiti umeonyesha, msichana akiolewa mume anaona tabu mke kuwa na mali, anamshawishi azinunue au ziandikwe kwa jina lake kama anampenda kweli. Na akina mama walivyo rahisi kurubuniwa, anaziandika kwa jina la Mrs au la Mume tu, mara anajikuwa anauza, talaka na mke mpya anaingia, mali kazikosa litigation ya miaka inaanza. 'Sidanganyiki' isaidie hapa. Mali ya ukoo kwa upande wake ya kuridhi wanae inauzwa, watoto wanakosa anakuwa mtumwa wa mali yake. Wazazi wanaona customary land na nyumba zaoi zimehama baada ya kugawa mgao sawa kwa watoto na mtoto kapewa talaka hana makazi. Usawa kijinsia haimaanishi ukiuke wajibu wa mama au baba kumtaka mama agharimie kila kitu cha familia eti wote sawa yeye zake kila kukicha anafanya biashara kwa mafao binafsi mama anazeeka na majukumu ya familia hiyo mali hana haki nayo ni ya akina wifi na watoto. haki sawa ni pamoja na kugawana majukumu kiwango cha kuridhisha, kupendana, kuaminiana, kulindana kiafya (usimuambukize kimakusudi); kuwa na mipango ya uzazi salama (usimzalishe kama mbuzi akijiunga na uzazi salama unaleta watoto wa nje kumkomoa). Msaidiane ktk shida na raha na muangalie majukumu ya nje ya familia yenu (ndugu pande zote mbili) kwa makubaliano (sio kila siku ni ndugu zako wewe upande mmoja tu wamejazana kufilisi mpaka inakuwa kero pia). Elimu na haki kwa watoto wa jinsia Me na Ke. Wenye vilema hata vya maumbile wasifichwe wasaidie. Hakuna kumtetea MBAKAJI ndani ya familia na ukoo na akibaka nje hata awe ndugu yako wa damu akale miaka 30 kosa ambalo halina msamaha wa Rais wewe unamfichaje?
Ukiwapa majukumu ya Jinsia watoto waelekeze mipaka yao na wafahamishe jinsi ya kuyatekeleza ama sivyo utakula Hasara. (angalia Video) Mtoto anatimiza wajibu kijinsia afanye kazi hata za teknolojia ya kisasa-anaikosha laptop kwa maji ya bomba. Itakuwa imeliwa kwako!! Utakapomtuma kaka asonge ugali-mwelekeze. atatafuta short-cut-ataweka maji na kuweka samaki, ataweka nyanya, vitunguu na chumvi kisha kuweka unga na kusonga ugali ili apunguze mzigo wa kazi eti kwanza apike mboga, kisha asonge ugali aweke mezani. Kwa nini asifanye vyote kwa pamoja akaokoa muda?

Unaamini katika usawa wa kijinsia ? unaamini kama mwanamke na mwanaume
ni sawa ?

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment