Tuesday 18 December 2012

[wanabidii] Re: Serikali ya CCM kutumia ITV, Star TV na TBC1 Kueleza mafanikio ya Serikali - William Lukuvi

 
Ndugu zangu,
 
Jana nilikuwa mapumziko kidogo, nakapata nafasi ya kumsikiliza Waziri Lukuvi katika kipindi cha kumekucha ITV. Kwa ufupi alisema kuwa Serikali ya awamu ya nne imepata mafanikio makubwa sana ila wananchi hawayajui. Hivyo wameamua kuja na wazo la ubunifu, kuanzia siku chache zijazo, kutakuwa na vipindi maalumu kwa muda wa nusu saa ambapo Mawaziri mbalimbali watatumia muda huo kueleza mafanikio yaliyopatikana kupitia TV stations zifuatazo ITV, TBC1 na Star Tv. Hili ni zoezi endelevu mpaka 2015. Wazo hili ni moja ya maazimio yaliyotokana na Mkutano mkuu wa CCM uliofanyika hivi karibuni. Akawaomba wananchi wasikose kuangalia vipindi hivi.
 
Hivi kama kuna mambo mazuri si yanaonekana tu?? mpaka myatangaze?
 
Hivi wakati wananchi wanakabiliwa na changamoto lukuki kuwahubiria mafanikio si kuwadhihaki? watu hawana maji, hawana makazi ya mazuri, rushwa na ufisadi vimekithiri wewe unazungumza ujenzi wa barabara na majengo (wengine wanaita shule, lakini sio shule, yale ni majengo. Shule ni ile inayotoa elimu na ina mazingira ya kutoa elimu) ambayo hayana waalimu, hayana vitabu wala maabara!!! 
 
Jitayarisheni kuelemishwa juu ya mafanikio ya CCM.
 
Selemani

0 comments:

Post a Comment