Monday 24 December 2012

[wanabidii] RE: Mawaziri wa JK wagongana

Ndg, Wanamabadiliko,
Wiki chache zilizopita waziri wa Mazingira Dr. Theresa Uvisa alizifungia Hotel 2 za Double Tree na Girafee Ocean View baada yakugundua kua hazizingatii usalama wa mazingira zinapoendesha shughuli zake. Kabla yahapo watumishi waliochini yake walifanya ukaguzi wa kushitukiza nakubaini uchavuzi mkubwa unaofanywa na hizio hotel, hasa kutiririsha mojakwamoja baharini bila kufanyiwa treatment maji taka na vinyesi. Waliwapa maagizo kua warekebishe mifumo yao ya majitaka, lakini wamiliki wa hotel hawakufanya chochote chamaana. Kwa maneno mengine walizizarau mamlaka zilizowekwa kisheria na kikatiba. Baada ya ukaguzi mwingine waziri Uvisa akaamua kuzifungia hizo hotel.
 
Chaajabu ajabu leo waziri wa Utalii Mr. Kaghasheki amekuja juu na kuuita uamuzi wa Wairi mwenzake kua ni uamuzi hatari sana na finyu wenye haraka, nausio kua na maslahi kwa taifa. Sababu kubwa anayotoa nikwamba hiki ni kipindi cha high season. Kwamaana kua nikipindi cha sikuku nyingi na watalii wengi wankuja kuitembelea Tz, kwahiyo huo uamuzi wa Dr. Uvisa utaikosesha nchi mapoto. Nimemshangaa sana huyu waziri Kaghasheki. Inamaana yeye kwake kinacho matter ni pesa hata kama zinapatikana kwa gharama ya mazingira na afya za watu? Kitu kingine cha hatari anasema kabla Dr. Huvisa hajachukua huo uamuzi alipaswa kuwasiliana na wizara yake, kwangu naona hayo pia nimawazo hatari sana. Maana kila wizara ana mandate yake amabayo amepewa, kwahiyo chamsingi nikusimamia hayo maagizo uliyopewa kwakufuata sheria. Kama kilawaziri atafanya maamuzi baada ya consultaion na wizara nyingine hata mahala amabapo mambo yako wazi hii nchi itaenda kweli???
 
Mr. Kaghasheki pia anasema wageni wataacha kuja Tz baada ya kufungia hizo hotel, kwakua hizo habari zakufungiwa hizo hotel zimewekwa kwenye mitandao. Haya ni mawazo ya ajabu na hatari sana. Inamaana hao wageni wangependa kuishi Katika hotel zisizo zingatia sheria za mazingira? Au tushidwe kutekeleza majukumu yetu kwakuogopa watu wengine wataquetion juu ya hayo maamuzi?? Mimi nasema kama nihivyo hao watalii nawapotelee mbali na fedha zao. Wengi tulikua tunamuona huyu Waziri Kaghasheki kama mchapa kazi lakini kwa mwendo huu nihatari sana kwataifa hili na ustawi wa mazingira ambao ndio hasa msingi wa Utalii huo anaoupigia upatu. Kweli jamani tuache uchafu ukiendelea kisa ni HIGH SEASON?
 
Nafikiri tunahitaji mawaziri watakao fanya kazi kwakufuata sheria na miongozo waliyopewa, Mimi naona Dr. Uvisa ametekeleza majukumu yake na mama kaza buti. Nakushauri kama itaonekana uamuzi wako siomzuri nawakubwa zako (kitu ambacho siamini) nakushauri ujiuzuru maana watakua hawana dhamira yakulinda mazingira. Mji wa Dar es salaam umekua mchafu kwasababu ya kupindisha sheria za mazingira.
Alexander

0 comments:

Post a Comment