Kwa taarifa zisizo rasmi ni kuwa matokeo ya dara la saba kwa mwaka 2012 yakop tayari takribani wiki 2 zilizopita. Kuna tetesi zingine kuwa serikali imefanya juhudi kubwa kuzuia wizi na udanganyifu katika mitihani ni na huenda matokeo ya sasa yakatoa sura halsii ya uelewa wa wanafunzi. Kama wadau tuna hamu kubwa ya kujua nini kimepatikana na nini kinaendelea na lini matokeo haya yatapatikana?
Jmakongo
----------------------------------------------------------------
Japhet Maingu Makongo
Director, Ubunifu Associates Ltd
P.O. Box 32971, Dar es Salaam, TANZANIA
Website: www.ubunifu.co.tz, info@ubunifu.co.tz,
Tel: +255 22 2762027, Mobile:+255 754 571 256
Director, Ubunifu Associates Ltd
P.O. Box 32971, Dar es Salaam, TANZANIA
Website: www.ubunifu.co.tz, info@ubunifu.co.tz,
Tel: +255 22 2762027, Mobile:+255 754 571 256
From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, December 13, 2012 7:22 PM
Subject: RE: [wanabidii] KATA 7 SERENGETI HAZITATOA MAONI KATIBA MPYA
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, December 13, 2012 7:22 PM
Subject: RE: [wanabidii] KATA 7 SERENGETI HAZITATOA MAONI KATIBA MPYA
Mbegu, Nakushukuru kwa kunikumbusha hilo; nadhani nilisema ng'ombe zao badala ya ng'ombe wao. Ni kweli kwa kuheshimu ngeli tunapaswa kusema "ng'ombe wao" na siyo "ng'ombe zao" lakini pia kwa kuheshimu kanuni ya sauti ni sahihi kusema "ng'ombe zao" kama ilivyo kwenye kusema "mama zao" au "babu zao" au "kaka zao" na siyo mama wao, babu wao au kaka wao, kwa kuwa neno ng'ombe linakubalika kwenye kundi la N/N ambalo ndilo pia huchukua maneno kama mama, babu, kaka, n.k. Umuhimu wa kutumia "wao" unakuja kwa sababu ng'ombe anawekwa katika kundi la viumbe wanyama wanaoishi ambalo lina binadamu pia na huitwa "M/WA". Kwa madoido ya kuandika kwa kufuata sauti/maneno ambayo ungeyatumia kwenye mazungumzo yasiyokuwa rasmi, hii kitu haina mushikeli. Asante lakini! Matinyi. From: embegu@hotmail.comTo: wanabidii@googlegroups.comSubject: RE: [wanabidii] KATA 7 SERENGETI HAZITATOA MAONI KATIBA MPYADate: Thu, 13 Dec 2012 12:39:19 +0000
Matinyi,Nadhani kwa kiswahili sanifu hatusemi ng'ombe hii na uwingi ukawa ng'ombe hizi.Tunasema ng'ombe huyu na uwingi ng'ombe hawa.Hivyo ki-ngeli, nadhani si sahihi kusema kwamba Wakurya "walipenda kuangalia ng'ombe zao" bali "ng'ombe wao".Kama vile Mbuzi huyu, kuku huyu, nguruwe huyu na uwingi unakuwa ... hawa, na siyo hizi.
Date: Thu, 13 Dec 2012 10:54:34 +0000From: khildegarda@yahoo.co.ukSubject: Re: [wanabidii] KATA 7 SERENGETI HAZITATOA MAONI KATIBA MPYATo: wanabidii@googlegroups.com
Waswahili husema-'Nyani haoni kundule'' Kama mkuu wa wilaya kaacha maeneo wilaya si zina kamati za kumshauri? labda wameona huko mapambano ndio yameanza ya wizi wa mifugo na vinginevyo hakupitiki kwa usalama wa kamati kaona wakuache kupoe. Anayetukana kinyume na maadili ndiye tu si pumba ubongo bali mpira uliojaa upepeo kichwani. Wajichorao si wale wenye kucheza utupu majukwaani hata wale watukanao hovyo au kutoa lugha chafu siziso maadili-Mtu mzima hovyo. Hao ndio wanaonyesha pumba na ubongo wao ulivyo na tope na wakiwa viongozi si wepesi kupokea mawazo ya watu mbali mbali huwa dictators. Pengine mtu hakusoma email zote kuona hiyo katiba amesoma kichwa cha habari akaona -kata hazitotoa maoni' akaona labda wamekataa. Kupayuka na lugha chafu inasaidia nini katika karne ya demokrasia na ya kujifunza kutoka kwa wengine hata wenye mawazo usiyo yapenda? Mwenye ila yake haachi !! Hongera kwa matusi-ubarikiwe.Kristmas njema.Nimekaa mara hakuna kijiji nisichofika-ninawaelewa. --- On Thu, 13/12/12, Chacha Mairi <chachamairi@gmail.com> wrote:
|