Tuesday 11 December 2012

[wanabidii] KATA 7 SERENGETI HAZITATOA MAONI KATIBA MPYA

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Serengeti
na kusainiwa na Katibu Tawala Wilaya Mr. M.C. Zonzo zaidi ya Kata 7 za
Wilaya ya Serengeti hazitashiriki kutoa maoni mbele ya Tume ya
kuratibu maoni ya Wananchi kuhusu mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.

Miongoni mwa Kata ambazo Wananchi wake hawatafikiwa na Tume ni:
Kisangura, Sedeko, Mbaribari, Machochwe, Nyamoko, Rung'abure na
Geitasamo. Kwa wale wanaoifahamu geografia ya Serengeti, wataona
ukanda wote wa mashariki ya Wilaya ya Serengeti, hautashiriki katika
zoezi hili la kutoa maoni.

Ratiba hiyo wameandikiwa Maafisa Tarafa, Rogoro, Ikorongo, Grumeti na
Ngoreme. Pamoja na habari, hapa naambatanisha nakala ya ratiba hiyo
kwa manufaa ya wasomaji wa habari hii. Aidha, nitumie fursa hii
kuwarai wote wanaohusika kulitazama jambo kwa upya na kuona ni kwa
namna gani waishio Serengeti na kwingineko ambako kumetokea hali ya
aina hii, watakavyoshiriki katika uandaaji wa katiba mpya.

Chacha Mairi
MWANASERENGETI

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment