Tuesday 11 December 2012

Re: [wanabidii] “Sisi wana CCM tunapaswa kutambua kwamba Tanzania siyo mali yetu” – Deo Filikunjombe - Mwanzo

Ndugu Ezekiel
Mbona viongozi wa chama chenu wanapitapita kwa wananchi na kuwaeleza
kwamba watatoa Elimu bure hadi kidato cha nne? Ninakushangaa kwa
kupingana na kauli za viongozi wako kwa wapiga kura. Chadema nao
wanasema mumewaibia sera sera yao.

Maelezo yako ni sahihi kwamba hakuna elimu ya bure ata wakati wa enzi
za baba wa taifa Elimu haikuwa bure kwa maana ya bure ilikuwa bure (in
bracket) kwa mzazi kutolipa ada, gharama za chakula, malazi na vitu
vingine vidogo. Hivi navyo si kwamba mzazi alikuwa halipi kabisa.
Alikuwa analipa kwa kukatwa kwenye malipo yake halali anapouza mazao
yake ambayo angelipwa lakini pia alikuwa anachangiwa na watanzania
wengine ambao hawakuwa na watoto wanaosoma.

Zipo gharama kama kununua sare za shule na vitu kama pocket money
ambavvyo mzazi alilipa moja kwa moja. Kwa maana hiyo katika dunia hii
hakuna elimu ya bure na wala haijawahi kutokea. Si sahihi kwa vyama
vya siasa ikiwemo CCM kupita kwa wananchi na kuwaongopea kwamba kuna
Elimu ya bure. wawaambie ukweli kwamba ni kumpunguzia uzito mzazi kwa
kumsamehe kulipia baadhi ya vitu lakini hakuna elimu ya bure

Tukumbuke ata muda anaotumia mtu(mwanafunzi) kuwa shuleni ni pesa
maana angeweza kuutumia kwa kufanya kazi nyingine ambazo
zingempunguzia mzazi makali ya maisha( opportunity costs). Kwa
kuangalia gharama zote anazobeba mzazi hakuna elimu ya bure na hivyo
wanasiasa waache kuwaongopea watu na pia serikali isimamie utoaji wa
elimu bora siyo kutwambie elimu bure wakiwa na maana ya kwamba hakuna
elimu yoyote inayotolewa na badala yake watoto wanapoteza muda bure.
Ni vyema wawe wakweli kwa wazazi ikibidi wawaeleze wazazi wachangie
zaidi ili elimu inayotolewa mashuleni iwe elimu bora siyo bora elimu
ya kuwapotezea muda watoto wa nchi hii na hivyo kupoteza nguvukazi

2012/12/11 ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>:
>
> Hayo ni mawazo yake. Nadhani yuko sahihi kama na yeye anaona hivyo. Kwa hiyo nafikiri mabadiliko yanatakiwa kuanza na yeye.
>
> Hoja ambayo nadhani hakuiona sawa sawa kwa mtizamo wangu ni kisoma bure. Jambo hilo kama nchi tulijaribu tukashindwa ndipo tukaingia katika kilipia. Nafikiri kama kuna watu wengine tofauti na Mheshimiwa wanafikiri hivyo wanatakiwa kubadili mawazo hayo. Huku tuendako hayawezekani kabisa. Dunia hii siyo yetu wenyewe kuna watu wasio watanzania ambao wanaelekeza nini kifanyike kwa wananchi wetu. Mfano ni mfumo wa demokrasia ya magharibi ambayo tumeikumbatia utadhani tunaielewa kwa undani. Jambo lingine ni la mazingira pia linahusu ulimwengu mzima. Elimu pia inawngukia katika mfumo huu. Elimu inayokubalika katika ulimwengu mzima ni ile inayolipiwa (najua hapa nimezua hoja)
>
> KEMS
> ------------------------------
> On Tue, Dec 11, 2012 07:36 GMT Magiri paul wrote:
>
>>MBUNGE wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM) amekipasha chama chake, kwamba
>>kimewafanya Watanzania waamini kwamba rasilimali za nchi ni mali ya chama
>>hicho, jambo ambalo siyo sahihi.
>>
>>Filikunjombe alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana jijini Dar es Salaam
>>wakati wa kongamano lililoandaliwa na Kikundi cha Wanataaluma wa Chuo Kikuu
>>cha Dar es Salaam (UDASA).
>>
>>Alisema kwamba, kuna mitazamo imejengeka kwa wana CCM walio wengi, kwamba
>>Watanzania wote ni mali ya CCM.
>>
>>"Sisi wana CCM hasa wale ambao tumepewa ridhaa na wananchi kuwatumikia,
>>tunapaswa kutambua kwamba Tanzania siyo mali yetu, hivyo jambo la muhimu la
>>kufanya ni kutumia nafasi zetu kuwaongoza na kuwaletea maendeleo kwa
>>kutumia rasilimali za nchi. Kwa mfano, hawa maprofesa wa chuo kikuu wana
>>nafasi kubwa katika kulijenga taifa na kuandaa kizazi chenye elimu lakini
>>utashangaa kuona wasomi ndiyo wanaalikwa kwenye harusi na kuchangia
>>mamilioni lakini kwenye sekta ya elimu hawahudhurii. Leo kila mtanzania
>>akiamua kuchangia Sh 24,000 ni dhahiri wanafunzi wa vyuo vikuu vyote nchini
>>watasoma bure, hivyo tuungane tuijenge Tanzania,"alisema Filikunjombe.
>>
>>http://wotepamoja.com/archives/10857#.UMbiAw8_tds.gmail
>>
>>--
>>Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
>>nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>>Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>>DELL LATITUDE D 620 & D30
>>
>>80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
>>DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
>>
>>TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
>>
>>CALL : 0786 806028
>>Free Delivery in Dar es salaam
>>
>>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>>
>>Disclaimer:
>>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> DELL LATITUDE D 620 & D30
>
> 80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
> DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
>
> TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
>
> CALL : 0786 806028
> Free Delivery in Dar es salaam
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment