Wednesday 19 December 2012

RE: [wanabidii] Re: Serikali ya CCM kutumia ITV, Star TV na TBC1 Kueleza mafanikio ya Serikali - William Lukuvi

 
Kingwangalla,
 
Hivi mafanikio gani hayo mnayaona nyinyi tu mlioko ndani ya CCM? Acheni upofu huo. Na nina kuhakikishia mkakati wenu huo utafeli kama ilivyofeli mikakati mingine. Nakumbuka Shujaa, kamanda, Dr. Slaa alipotoa ile list of shame, Aggrey Mwanri alitoa taarifa kuwa CCM itazunguka nchi nzima kuzima hoja ile. Je mlifanikiwa? kuna wakati eti Mawaziri walitakiwa kutembelea nchi nzima kueleza uzuri wa budget!! wala hamkufika popote pale, kwani mliishia kuzomewa na wananchi.
 
Juzi Lukuvi ameongea katika kipindi cha Tuongee asubuhi, mwananchi mmoja akampinga kwa hoja na data ambazo alishindwa kuzijibu. Akabaki kusema kuwa eti aliyepiga simu ni Kamanda Lema na eti anawaigiza maofisa wa Wizara yake wafuatili ili kumjua huyo aliyepiga simu. Kwa taarifa tu Kamanda Lema alikuwa safirini wala hakuwa anajua kuna Lukuvi anaongea. Hapa ndipo unapojua kuwa elimu ni kitu cha maana sana. Lakini mbona hata mtu kama wewe, msomi una upofu? nadhani there is more than that.
 
Mkakati wenu huu unaitwa ni non starter, yaani umekufa kabla haujaanza. Kama huamini tusubiri na tuone. Na kama ni majasiri basi katika vipindi hivyo, mruhusu maswali na maoni kutoka kwa wasikilizaji, muone cha moto. Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza.
 
Selemani
 

Subject: Re: [wanabidii] Re: Serikali ya CCM kutumia ITV, Star TV na TBC1 Kueleza mafanikio ya Serikali - William Lukuvi
To: wanabidii@googlegroups.com
From: hkigwangalla@gmail.com
Date: Wed, 19 Dec 2012 03:48:51 +0000

Watu wote waliokuwa na jitihada za kuipinga CCM na serikali yake kwa kutumia uongo, udanganyifu ama hoja dhaifu wamechoka sana sasa, CCM inazidi kusonga mbele, inafanya kazi yake vizuri, na sasa inataka wananchi waone mafanikio yake! Pole sana Babu yangu 'Selemani'
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: Selemani Rehani <srehani@hotmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 18 Dec 2012 11:25:38 +0000
To: mabadiliko Tanzania<mabadilikotanzania@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Cc: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii] Re: Serikali ya CCM kutumia ITV, Star TV na TBC1 Kueleza mafanikio ya Serikali - William Lukuvi

 
Ndugu zangu,
 
Jana nilikuwa mapumziko kidogo, nakapata nafasi ya kumsikiliza Waziri Lukuvi katika kipindi cha kumekucha ITV. Kwa ufupi alisema kuwa Serikali ya awamu ya nne imepata mafanikio makubwa sana ila wananchi hawayajui. Hivyo wameamua kuja na wazo la ubunifu, kuanzia siku chache zijazo, kutakuwa na vipindi maalumu kwa muda wa nusu saa ambapo Mawaziri mbalimbali watatumia muda huo kueleza mafanikio yaliyopatikana kupitia TV stations zifuatazo ITV, TBC1 na Star Tv. Hili ni zoezi endelevu mpaka 2015. Wazo hili ni moja ya maazimio yaliyotokana na Mkutano mkuu wa CCM uliofanyika hivi karibuni. Akawaomba wananchi wasikose kuangalia vipindi hivi.
 
Hivi kama kuna mambo mazuri si yanaonekana tu?? mpaka myatangaze?
 
Hivi wakati wananchi wanakabiliwa na changamoto lukuki kuwahubiria mafanikio si kuwadhihaki? watu hawana maji, hawana makazi ya mazuri, rushwa na ufisadi vimekithiri wewe unazungumza ujenzi wa barabara na majengo (wengine wanaita shule, lakini sio shule, yale ni majengo. Shule ni ile inayotoa elimu na ina mazingira ya kutoa elimu) ambayo hayana waalimu, hayana vitabu wala maabara!!! 
 
Jitayarisheni kuelemishwa juu ya mafanikio ya CCM.
 
Selemani

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment