Thursday 6 September 2012

[wanabidii] Heri Kafiri Mkapa aliwapa waislamu chuo Kikuu cha Morogoro

Leo nimepita jirani na msikiti mmoja kwetu MBAGALA, nilivutiwa
Sana na mtoa hotuba ambaye alikuwa akitoa tathmini juu ya maraisi
wote walioweza kuiongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mdau huyo alikuwa anasema katika mimbari ya msikiti huo jirani na
nyumbani kwangu Rais Jakaya Kikwete japokuwa ni muumini katika
dini yetu hajawafanyia lolote waislamu.

Nilivutiwa sana nikatega sikio zaidi mtoa hotuba anasema heri
ya kafiri Mkapa aliweza kuwapa waislamu wa Tanzania chuo kikuu
cha Morogoro. Anamalizia kwa kusema yani hawa wanojihita waislamu
wenzetu mpaka sasa wanamaliza muda wao wa kuingoza Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania hakuna walichotufanyia.

Sasa jamani tufanye nini?Tuwachague makafiri au tuwachague ndugu
zetu walio katika imani yetu. Gafla Luku ya msikiti ilikwisha basi
na mimi nilishindwa kuyapata zaidi katika hotuba ile nikaelekea
kwangu kulala salama salimini.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment